RC Arusha: Dola haitakubali Arusha kutokutawalika

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo ameonya kuwa vyombo vya dola havitakubali kuwaacha baadhi ya watu kuigeuza Arusha sehemu isiyotawalika akisema kuanzia sasa, yeyote atakayejaribu kuvuruga amani na utulivu kwa njia au sababu yoyote atadhibitiwa kikamilifu bila kujali cheo wala itikadi yake kisiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mulongo alisema: “Mtu yeyote atakayechezea amani na utulivu wa Arusha atakiona cha mtema kuni. Huu ni uamuzi wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama. Hatuwezi kukubali baadhi ya watu wafanye Arusha isitawalike.”

Mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, pia alizungumzia tuhuma kuwa anaingilia utendaji wa baadhi ya idara ikiwamo polisi na mahakama akisema hizo ni tuhuma zisizomnyima usingizi kutekeleza wajibu na majukumu yake kiutendaji na kuongeza kwamba, uwepo wa shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ya vyama, hauwezi kuvuruga mipangilio yake ya kazi.

Alitoa kauli hiyo baada ya juzi kudaiwa kuonekana maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha asubuhi kabla ya ombi la kutolewa kwa hati ya kumtoa Lema mahabusu, ili awekewe dhamana kukataliwa na hakimu Judith Kamara na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema.

“Kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa Mbowe au shughuli zozote za kisiasa Arusha. Nilikwenda kumsalimia Jaji Mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo Lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa Mahakama,” alisema Mulongo.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi wa Serikali, watendaji na wale wa vyama vya siasa Arusha kujikita katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuendeleza siasa hata baada ya uchaguzi mkuu kumalizika huku akitamba kuwa pamoja na madai kuwa Arusha haitawaliki, bado anaamini mji na mkoa huo kwa ujumla uko shwari baada ya dola kuimarisha ulinzi.
 
Ni muongo huyo, inaelekea anahusika kwa 100% lakini iko siku haki itatendeka, kwani hata Libya walianza hivi hivi.
 
"Dk. Slaa tulimkamata akiwa ndani ya gari la matangazo katikati ya spika uwanjani hapo."
 
RC,mahakama na jeshi la polisi ndio wa kuonywa kuhusu hilo.
Naona kafanya Preemptive Strike.
 
Magessa Mulongo bado hajaijua Arusha vizuri. Si muda mrefu atakula matapishi yake.
Ukombozi wa Tanzania unaanzia Arusha.
 
"Dk. Slaa tulimkamata akiwa ndani ya gari la matangazo katikati ya spika uwanjani hapo."

Siyo kila kitu kushabikia, after all you were not there. you can just keep silence for knowing nothing.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo ameonya kuwa vyombo vya dola havitakubali kuwaacha baadhi ya watu kuigeuza Arusha sehemu isiyotawalika akisema kuanzia sasa, yeyote atakayejaribu kuvuruga amani na utulivu kwa njia au sababu yoyote atadhibitiwa kikamilifu bila kujali cheo wala itikadi yake kisiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mulongo alisema: "Mtu yeyote atakayechezea amani na utulivu wa Arusha atakiona cha mtema kuni. Huu ni uamuzi wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama. Hatuwezi kukubali baadhi ya watu wafanye Arusha isitawalike."

Mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, pia alizungumzia tuhuma kuwa anaingilia utendaji wa baadhi ya idara ikiwamo polisi na mahakama akisema hizo ni tuhuma zisizomnyima usingizi kutekeleza wajibu na majukumu yake kiutendaji na kuongeza kwamba, uwepo wa shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ya vyama, hauwezi kuvuruga mipangilio yake ya kazi.

Alitoa kauli hiyo baada ya juzi kudaiwa kuonekana maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha asubuhi kabla ya ombi la kutolewa kwa hati ya kumtoa Lema mahabusu, ili awekewe dhamana kukataliwa na hakimu Judith Kamara na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema.

"Kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa Mbowe au shughuli zozote za kisiasa Arusha. Nilikwenda kumsalimia Jaji Mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo Lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa Mahakama," alisema Mulongo.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka viongozi wa Serikali, watendaji na wale wa vyama vya siasa Arusha kujikita katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuendeleza siasa hata baada ya uchaguzi mkuu kumalizika huku akitamba kuwa pamoja na madai kuwa Arusha haitawaliki, bado anaamini mji na mkoa huo kwa ujumla uko shwari baada ya dola kuimarisha ulinzi.

Tafasili ya jina la huyu jamaa ni hili .

Alizaliwa wakati watu wanavuta akaitwa Magesa means nyakati za mvuno si ni mvivu huyu kwa nature ya jina la kwanza.Mulongo wote mnajua Kenya wanita muongo kwamba ni Mulongo the same applies here .Ni muongo.Nadhani ameanza kuhaha kama katamka kamba Arusha haitawaliki basi kaanza kupata joto na atajuta .Amani s yeye mkuu wa mkoa wala dola .Amani ni Watanzania waArusha na imani na maish yao na haki zao .Hivi wakinyimwa hakuna amani .
 
"Dk. Slaa tulimkamata akiwa ndani ya gari la matangazo katikati ya spika uwanjani hapo."

what is the issue,kwa anayeyajua magari yale hawezi kushangaa.Ndani ya yale magari kuna chumba chenye magodoro,na siku zote watu wanalala humo hsta siku moja gari halilali ila mtu.

Sikiliza wapelekee wenzako taarifa siasa inasonga huu ni mwanzo mzuri kwetu.tunasonga.
 
Mwache huyu mshamba hajui kuwa ndiyo kwanza tumeaanza....

Haitatawalika hadi CCM itoke kabisa Arusha....

Just want to tell the leaders of this Nation.... From Kikwete and his allies.. that

"We cannot solve our problems with the same thinking we used when we created them"

think of that.............
 
........................hata hawa (Gaddafi, Mubarak, Sadaam-kwa uchache) walikuwa na dola
 
kutotawalika kwa arusha kunaletwa na vyombo vya dola vyenyewe, serikali isidhanie watanzania wa sasa ni sawa na wa miaka 50 iliyopita, wananchi wanatambua haki zao na wanazielewa na ndio maana wanazidai na kuzipigania, mimi binafsi naamin hata kama kuna watu watafungwa kwa ajili ya kupigania haki na usawa, KIVULI CHAO KTAISHI DAIMA na watatokea wanaharakati wengine ambao watakua na ndoto zilzile
 
Back
Top Bottom