RC Anna Mghwira: Mtu asijenifuata ofisini kuniambia masuala ya ACT Wazalendo

Uhalisia wa binadamu yeyote unategemea tabia zake, na mtu yeyote anayesema maneno asiyoweza kuyatimiza (uongo) kutokuishi kwake ni bora kuliko kuishi kwake.
Vivyo hivyo kuwa mwenyekiti wa chama fulani wakati uhalisia wako ni ccm unaangukia kundi la waongo!
 
Eti anaitumikia serikali ambayo siku chache alituhubiria hao ndio wametufikisha hapa..
Alipokubali kuteuliwa ina maana amekubali kucheza nyimbo za CCM. Aliyoyasema huko nyuma kwa sasa ni historia.
Hivyo ni halali akisema anaitumikia serikali.
 
Hana jipya huyu mama mbona yeye ni CCM miaka mingi? Huyu alikuwa mpinzani wa kupandikizwa na ndiyo maana kwenye hafla nyingi za CCM alikuwa anahudhuria.
 
Mtu hata kama alikuwa na akili au elimu kiasi gani,ila akihamia tu ccm anawehuka anakuwa na akili kama za akina Lusinde.kweli ccm kuna laana,ukiingia tu unadata na uwezo wa kufikiri unapungua na kutoweka kabisa
 
Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghirwa amesema kwa sasa yeye anaitumikia serikali na anapokuwa ofisini anakuwa ana deal na mambo ya serikali tu na mtu asij ofisinikwake kuzungumzia masuala ya ACT kwani kama anataka kuzungumzia maswala hayo itakuwa ni kwenye ofisi za chama hicho


Laiti haya anayosema huyu mama yangekuwa yanatekelezwa pia na walio mteua! Tusingeona vikao vya chama vikifanyika Ikulu! Tusingeona ndege ya Raisi ikimpeleka W/kiti wa chama kuhudhuria shughuli za chama popote nchini! Na kuanzia kwa mkuu ingeshuka mpaka kwa ma RC na ma DC
 
Yani hata ule uwezo wake wa kufikiri umepungua sana anaongea blah blah tu hapo, njaa kitu kibaya sana.
 
Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghirwa amesema kwa sasa yeye anaitumikia serikali na anapokuwa ofisini anakuwa ana deal na mambo ya serikali tu na mtu asij ofisinikwake kuzungumzia masuala ya ACT kwani kama anataka kuzungumzia maswala hayo itakuwa ni kwenye ofisi za chama hicho

Yes Ma'am.
 
Huyo mama mnayemlaumu ni mtanzania tu kama sisi ana njaa zake kama mtamzania wewe na mimi. Hakuna mtu angeweza kukataa uRC na masharti yake humu. Kama yupo aseme.
 
Hakuna mpinzani ambaye aliwahi kupewa cheo ndani ya serikali ya sisiemu akakataa kushirikiana na ccm kutekeleza ilani ya CCM au akipewa cheo atakataa.
 
KWELI ZITTO YUPO SAHIHI.
Aisee ningependa kutoa pole kwa wafiwa mliopata msiba huu wa kisiasa

Rest in peace vijana na makamanda wote wa act wazalendo mliopoteza muda wenu kukipigania chama chenu cha act katika uchaguzi mkuu 2015.

Mungu azilaze roho zenu mahala pema peponi amina.
 
Back
Top Bottom