RC Anna Mghwira: Mtu asijenifuata ofisini kuniambia masuala ya ACT Wazalendo

Umeongea vizuri mama. Sisi ACT tumekupa go ahead katekeleze majukumu yako.
Tunaendelea kujenga chama makini.
Ccm ni chama hovyo kabisa hakina watendaji makini, sisi chama makini tutawapa wataalam kwa nia njema ya taifa letu.
wew ni act kumbe? mcubic yuko wapi sikju hizi?
 
Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghirwa amesema kwa sasa yeye anaitumikia serikali na anapokuwa ofisini anakuwa ana deal na mambo ya serikali tu na mtu asije ofisini kwake kuzungumzia masuala ya ACT kwani kama anataka kuzungumzia masuala hayo itakuwa ni kwenye ofisi za chama hicho.

Simshangai sana maana ukisha weka ahadi na ccm akili zinapungua Fulani hivi
 
Hv isingekuwa ACT huyu mama angepata spotlight aliyoipata mpk Mkulu kamteua??Kama ndio, bas wanasiasa ni watu wa ajabu sana.
Ndivyo, walivyo wanatumia wananchi, halafu wakiteuliwa wanakuacha nje .... Kweli kabisa usiamini wanasiasa.
 
Mkuu una uhakika gani kuwa hana kadi tayari?! Ataendesha vipi vikao vya chama kama yeye si mwanachama?!
Kwa kweli sina maana siasa za bongo wanaziweza wenyewe tu ndo maana akana Slaa and co licha ya kuwa CHADEMA walikuwa na kadi za kijani kibindoni
 
Shortly umechemka we mama,hata kama una dhiki kiasi gani si kwa kugeuka kuwa jiwe la chumvi unafiki utamhukumu huyu. Alitudanganya waziwazi jukwaani usitegemee kuiona mbingu
 
March 21, 2019
Dodoma Makao Makuu / Makao ya Bunge la Taifa

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghirwa ameshindwa kujizuia kuongelea ACT-Wazaledo ingawa alishaomba watu wasimuulize kabisa masuala ya chama hicho alichokua mwanachama kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Hata hivyo baada ya Maalim Seif kujienga toka CUF. Mh. Anna Mghirwa alifunguka kuhusu yeye kushinda mbele ya TV na Redio kufuatilia habari hii ya Maalim Seif na hali mpya ya kisiasa Tanganyika na Zanzibar

ANNA MGHWIRA: SIJASHTUSHWA NA MAALIM SEIF KUHAMIA ACT - MSIKILIZE
Anna Mghirwa ni nani : aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Change and Transparency Tanzania, ACT wazalendo.

Source: A-FMRadio Dodoma
 
March 21, 2019
Dodoma Makao Makuu / Makao ya Bunge la Taifa

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mghirwa ameshindwa kujizuia kuongelea ACT-Wazaledo ingawa alishaomba watu wasimuulize kabisa masuala ya chama hicho alichokua mwanachama kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Hata hivyo baada ya Maalim Seif kujienga toka CUF. Mh. Anna Mghirwa alifunguka kuhusu yeye kushinda mbele ya TV na Redio kufuatilia habari hii ya Maalim Seif na hali mpya ya kisiasa Tanganyika na Zanzibar

ANNA MGHWIRA: SIJASHTUSHWA NA MAALIM SEIF KUHAMIA ACT - MSIKILIZE

Source: A-FMRadio Dodoma

Mama Mghwira hebu tueleze, kama usingepewa cheo CCM ungehama ACT?
Je ulihamia CCM kwa kufuata itikadi "nzuri" ya CCM?
 
Kuna jambo ameligusia kuhusu itikadi ya vyama na umuhimu wa hizo itikadi katika kufanya maamuzi ya mrengo ambao mwanachama anatakiwa kuuamini nimemsifu sana. Ametoa ufafanuzi mzuri sana. Anauliza je Maalim ameacha kuamini kwenye uliberali? Au ACT Wazalendo wameacha kufata itikadi ya Ujamaa wa Kidemokrasia?
Kwa wale wanaomfata Maalim ipo haja wakaelimishwa kule wanapokwenda kuna itikadi gani? Na viongozi wa chama cha ACT Wazalendo wanatakiwa wawafafanulie wanachama wao ni itikadi gani wayoendelea nayo kwa hivi sasa. Ila kwa mbaaaaali bado anaonekana kuamini itikadi ya ACT Wazalendo.
 
Back
Top Bottom