*Tukio la kutekwa Ludovick ladaiwa kuwa ni 'feki'
*RB yake yazua utata, Polisi washikwa kigugumizi
Joseph Ludovick
IMEIBUKA hofu ya kuwepo mpango mahususi unaoratibiwa naSerikali kufichua njama za kigaidi, ambazo zinadaiwa kutekelezwa na baadhi yaviongozi wa kisiasa wanaoheshimika katika jamii, MTANZANIA Jumapili limebaini.
Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa,kukamatwa kwa mtuhumiwa namba mbili katika kesi ya ugaidi iliyofunguliwaMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ludovick Joseph, ni utekelezaji wa mpango huo.
Imedaiwa kuwa, kuna utata mkubwa wa usahihi wa taarifa zatukio la Ludovick kutekwa na watu ambao hawajafahamika hadi sasa na hatataarifa za kutekwa kwake alizodai kuzifikisha katika kituo kidogo cha polisiKigogo, nazo zina utata.
Kwa mujibu wa wapasha habari wetu, taarifa za kutekwa kwaLudovick na kunyanganywa vitu vyake vyote alivyokuwa navyo, zikiwemo nguoalizokuwa amevaa na hata madai kuwa aliripoti tukio hilo katika kituo chaPolisi Kigogo siyo za kweli, bali zimetengenezwa ili kufanikisha mpango huo.
Ludovick alidai kutekwa usiku wa Jumanne ya Machi 5, mwakahuu, akiwa eneo la Sinza ambako alisema alitoa taarifa zake katika Kituo chaPolisi cha Kigogo na kufunguliwa RB yenye namba KIG/RB/318/2013.
Taarifa ya kutekwa kwake aliiandika mtandaoni na ilisomekahivi; Leo usiku, yapata saa tano na nusu, niliachana na Maggid Mjengwa maeneoya Shekilango tukitokea Rose Garden. Yeye alielekea hotelini alikofikia sehemufulani Kariakoo nami nikasubiri kigari kuelekea nyumbani kwangu.
Hapo Shekilango, magari yalichelewa kidogo, pembeni ilipakibajaji ikiwa na watu wawili na dereva ndipo wakaniambia twende tuchangie miatano tu kwenda Ubungo Mataa, nikakaa katikati ya hao jamaa.
Ghafla wakakata kona na kuanza kuelekea Mabibo hukuwakiulizana kama wako kamili na mwinginekujibu yuko kamili. Nikajua tayari niko mikononi mwa majambazi na sikujua wakokamili namna gani, kwa hiyo nikaamua kuwa mtulivu.
Tulipofika relini karibu na Mabibo wakanipokonya begilakini, hawakulifungua. Ndani yake kulikuwa na laptop, toshiba kubwa na chajiyake, kamera ndogo ya digital na USB yake, modem ya zantel na card reader.Tulipofika maeneo ya Loyola Sekondari, nikawasihi wanishushe ili nirudimwenyewe, wakaniambia safari ile inaishia Jangwani.
Nikaingiwa na wasiwasi mkubwa na nia yao hasa, maana wameshanipokonya begi kwanini wasiniachie? Lakini niliendelea kuwa mtulivu ili kutowaprovoke.
Tulipovuka Kigogo mwisho kwenye giza karibu na msikiti, wakasimama pembeni yabarabara na kuniamuru kushuka, nikashuka na kuanza kuwadai begi langu, ndipommoja akasema wamekuwa wastaarabu mimi naanza kuwadharau. Ghafla akanivuta kwanguvu kunirudisha kwenye kibajaji akamwambia mwenzie wanisachi kama nina vitu vingine, wakanisachi na kuchukua pesa,nilikuwa na elfu 35 na simu mbili ndogo za nokia moja yenye line mbili.
Kisha mmoja akatoa order nivuliwe nguo. Nikavuliwa viatu,T-shirt na suruali nikabaki na nguo za ndani pekee. Wakanishusha na kuniachahapo.
Kurudi nyuma kama hatua kumi tu ndipo kituo kidogo chapolisi Kigogo nikaanza kutoa maelezo hapo kwa zaidi kamaya saa mbili nikiwa uchi na nguo za ndani tu. Nikiwa hapo nikasikia polisiwakiwasiliana juu ya tukio la kupigwa vibaya Absalom Kibanda, kwenye rediocalls.
Ilikuwa yapata saa nane, baada ya kuchukuliwa maelezo polisiwalinipatia gari nikaelekea hotelini kwa Maggid, ambaye saa kumi aliamshwa nakunichukulia chumba hapo nikapumzika. Ameniazima nguo zake ndizo nimevaa badohadi sasa naelekea kituo cha Polisi Magomeni kwenda kupewa mpelelezi wa kesiyangu. Namba ya kesi yangu Kigogo ni KIG/RB/318/2013, wizi kutoka maungoni.
Wakati Ludovick akiwa ametoa maelezo hayo kwa jamii kupitiamitandao ya kijamii, polisi wameshindwa kuthibitisha taarifa za kutekwa,kuporwa na kupokea taarifa yake aliyodai kuitoa kituo kidogo cha polisi Kigogo.
Polisi katika kituo kidogo cha Kigogo waliohojiwa naMTANZANIA Jumapili kuhusiana na taarifa za Ludovick, walionekana kurushianampira kuzizungumzia.
Askari aliyekutwa kituoni hapo alipoulizwa kuhusu taarifahizo alisema taarifa za matukio mbalimbali hufunguliwa hapo, lakini huhamishiwaKituo cha Polisi cha Magomeni kutokana na udogo wa kituo hicho, hivyo kumtakaMwandishi kufuatilia suala hilo katika Kituo cha Polisi Magomeni.
Gazeti hili lilipofika Kituo cha Polisi Magomeni, kwa AskariMpelelezi liliyeelekezwa kuwa anahusika na kesi ya Ludovick aliyetajwa kwa jinamoja la Chuki hakuwepo bali lilipewa namba ya simu yake ya kiganjani naalipotafutwa, naye alikana kuhusika na suala hilo na kuelekeza atafutwe askaripolisi aliyetajwa kwa jina la Lukwamba Sanga.
Alipopigiwa Sanga na kuulizwa kuhusu sakata hilo, kwanza alikiri kuwa yeye ndiyempelelezi wa kesi hiyo na kueleza kuwa ni kweli Ludovick alifungua RB katikakituo cha Polisi cha Kigogo lakini hakuwa tayari kutoa namba ya RB hiyo.
Alieleza kuwa mwenye mamlaka ya kutoa namba hiyo ni Mkuu waUpelelezi wa Kituo ambaye hata hivyo hakupatikana, lakini ofisa mwinginekituoni hapo alieleza kuwa namba hiyo inaweza kutolewa kwa idhini ya Kamanda waMkoa wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela.
Kamanda Kenyela alipotafutwa, alisema anahitaji muda kuipatanamba hiyo, kwa sababu ana majukumu mengi hivyo atafutwe baadaye. Lakinialipotafutwa tena simu yake ya kiganjani ilikuwa haipatikani.
Hata alipopigiwa simu tena jana iliita mfululizo pasipomajibu.
Wachambuzi wa masuala ya saikolojia wanadai dalilizinaonyesha kuwapo kwa uwezekano wa Ludovick kushiriki tukio la kutekwa nakupigwa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, ambayepia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Wanasema ni kawaida kuwa watu wanaojihusha na matukio yaaina hii, baada ya kuyatekeleza huchanganyikiwa, hivyo hata kitendo chaLudovick kukimbilia kuandika katika mtandao wa facebook kuwa naye alitekwakinaweza kuchukuliwa katika mtizamo huo.
Maswali ya kujiuliza
Ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja sasa baada ya kuvamiwa nakuteswa kwa Kibanda na siku chache baadaye kukamatwa kwa Ludovick akihusishwana tuhuma za kupanga ugaidi, yapo maswali mengi miongoni mwa jamii ambayohayajapata majibu kuhusu matukio hayo.
Swali kubwa linaloumiza vichwa vya wengi hivi sasa ni namnaambavyo Ludovick alifanikiwa kujipenyeza na kufanikiwa kujenga mtandao wamasiliano ya simu za mkononi na katika mitandao ya kijamii na Waharirimbalimbali wa Vyombo vya Habari.
Tayari Wahariri wawili, Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo,wamekwishatajwa kuwa na mawasiliano ya muda mrefu na Ludovick na kwamba kunabaadhi ya taarifa muhimu za waandishi na wahariri ambazo Ludovick alikuwaakizipata kupitia mawasilino yake hayo.
Kutajwa kwa wahariri hao kuwa washirika wa karibukimawasiliano na Ludovick, kuliibua hisia kuwa Wahariri hao, waliingizwa katikamtandao wa Ludovick na kuanza kufanya kazi zake pasipo wao wenyewe kujua auwakiwa na ufahamu huo.
Lakini pia wadadisi wa mambo wamekuwa wakihoji nguo za Ludovickzilipo baada ya kile kinachodaiwa kuwa tukio hilo la kudai kutekwa ni feki.
Hali kadhalika hatua ya Ludovick baada ya kuachana na Mjegwana kupanda bajaji iliyokuwa na watu wawili kisha akakaa katikati kwa nauli yashilingi mia tano huku akiwa na pesa taslimu shilingi 35,000, begi lenye laptoptoshiba kubwa, chaja yake, kamera ndogo ya digital na USB yake, modem ya zantelna card reader, jambo linaloonyesha kuwa alikuwa na uwezo wa kuchukua usafirisalama zaidi.
Aidha, mkanganyiko wa maelezo ya Ludovick na yaleyaliyotolewa na Mjengwa ambako yeye (Ludovick) alidai kupewa gari na polisikumpeleka hotelini kwa Maggid, huku Maggid akidai alifika hapo kwa usafiri wateksi, nayo yanazidi kuacha swali gumu la kupata ukweli wa sakata hili zima.
Kuhusishwa kwake na tukio la Kibanda Siku na wakati ambaoKibanda alitekwa na kuteswa, Ludovick naye alidai kutekwa na majambazi akiwaeneo la Sinza, jirani na mahali ilipo ofisi ya Kibanda. Ludovick alidai kutekwana watu wasiojulikana majira ya saa tano usiku siku ya Jumanne ya Machi 5,mwaka huu, ambapo watekaji wake walimnyanganya vitu vyake mbalimbali na kumvuanguo zote pamoja na kuchukua simu zake mbili.
Ingawa katika uchunguzi wake gazeti hili liliambiwa kuwasimu yake iliendelea kutumika katika maeneo ya mnara wa Sinza karibu na ofisianakofanyia kazi Kibanda siku mbili mara baada tukio la kuteswa kwa Mharirihuyo. Pamoja na hilo,siku mbili kabla Kibanda hajatekwa, anadaiwa kufanya mawasiliano na kiongozimmoja mkubwa wa chama cha siasa.
Ahusishwa na video yaLwakatare
Yuko mikononi mwa sheria na alishafikishwa Mahakamani pamojana Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare, kutokana na mipango ya kudhuru watu, wakiwemowaandishi wa habari pamoja na suala la ugaidi.
Inaelezwa kuwa watu hao wamekuwa karibu kwa muda mrefuambapo wote ni wenyeji wa Mkoa wa Kagera, na kwa mujibu wa watu wa karibu namahusiano yao, walisema kuwa Ludovick amepata kumsaidia kufanya kampeni zakuwania ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini mwaka 2000.
Ludovick ni nani?
Ludovick, mbali na kuwa na ukaribu na Lwakatare, pia alikuwamtu wa karibu na Mjengwa, akimsaidia katika shughuli za blog yake, pamoja nawahariri mbalimbali wa habari.
Ludovick pia wapo wanaomtambua kamamtu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Mjengwa pia aliwahi kukiri kutofahamu kazi halisi aliyokuwaakiifanya Ludovick mtaani, lakini katika maelezo yake aliyoandika kupitiakwenye mtandao wa Jamii Forum, Mjengwa alisema anamfahamu Ludovick tangu akiwaChuo Kikuu (DUCE) na kwamba ni mmoja wa Watanzania wengi waliomfahamu kupitiakazi zake magazetini.
source Mtanzania