Rayvanny anatengeneza direction sahihi ya Bongo Fleva. Wasanii muifate

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,522
7,368
ya leo leo.png

Kuna siku niliweka thread nikisema Rayvanny ndio Mangwea wa kizazi cha sasa, wakatokea watu wakanishambulia sana.

Sasa niwaambie movement za sasa za Ray ndio standard tunayopaswa kwenda nayo kama tunataka kutoboa soko la international.

Ukisikia EP yake mpya inaitwa New Chui unaona kabisa hii ndio njia ya kutobolea bongofleva. Ni EP ambayo amejaribu kuunganisha muziki wetu na muziki unaofanya vizuri duniani na bado ukisikia unasema yes hii ndio sanaa yenye quality tunazotaka.

Kuna kasumba kwamba ukiimba kizungu sana utoboi soko la bongo, ila mniamini mimi kama wasanii wakifanya kwa namna ya Rayvanny kwenye new chui mbona watu wataelewa na tutatoboa kotekote nyumbani na mbele.

Btw hongera kwa Rayvanny kupiga show kwenye stage ya MTV Europe.... history uliyoweka ni wajukuu zetu ndio watakuja kukuappreciate.

Wewe ni international level artist, dunia inakuelewa.
 
Usiku wa kuamkia leo, mtu mbadi V vanny boy, half chui half animal, kapiga bonge la show huko Hungary kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za MTVEMA akiwa na Maluma

Hii inamfanya Rayvanny kuwa MSANII WA KWANZA TOKEA TANZANIA NA AFRIKA kwa ujumla kupiga show katika jukwaa la ugawaji wa tuzo hizo. Haijawahi tokea!

Hii inaonesha kuwa Vanny boy ni next big thing kwenye industry ya muziki bongo. Hana mbwembwe, hana papara, yeye bize na kazi zake tena kimyakimya...

EP ya New chui hata hatukuitarajia lakini ndo inayokimbiza huko kwenye madigito platifomu kwa album na ep zote zilizotolewa mwezi huu wa 11. (Mwendo wa chui mawindoni)

Hakika vijana wengine wana la kujifunza kwa huyu mwamba wa kusini. Wakiacha mihadarati na kuwavimbia washikadau watafika mbali. La si hivyo hata macvoice atawaacha mbali sana. Mziki unahitaji watu wenye nidhamu

Once again, congrats Rayvanny
 
shida asipofumbua macho yeye atatengeneza nyimbo/jina ila Domo, tale,sallam na saidi fella wao ndio wanatengeneza hela, maana mikataba ya WCB ina walakini wale watoto wanakufa na tai shingoni ila kiukweli wanaumia hawapati kile wanachostahili kutokana na jasho lao
 
Mzee hakuna anayejua mikataba yao ipoje na inawataka wafanye nini... Maadamu hakuna aliyewahi lalamika basi wananufaika kutoka kwny hiyo mikataba!

Kumbuka hata mmakonde hakulalamika popote hasa mahakamani kuwa alinyonywa na alipotakiwa kulipa 600M aliilipa... Hiyo inaonesha alipata faida ya kuwa WCB mpaka akapata hiyo hela na zaidi. Kumbuka hakuna mtu anayeweza kuilipa hiyo hela from nowhere. Ni lazima alipata faida ndo maana alilipa na hela nyingine akafungulia lebo

Kumbuka, hata US, asilimia 95 ya wasanii wapo chini ya lebo
 
hujui unachokiongea unaweka ushabiki mbele hivi unajua nyimbo zao wanzotoa wakiwa WCB zote sio mali yao, unajua mpaka hizo account zao za social media sio mali, wao ni kama wafanyakazi wengi pale kitu ambacho ni tatizo kwenye sekta ya sanaa na ubunifu. rejea kesi ya konde na rich mavocal, konde alisaidiwa na jembe ni jembe lakini wapi ruch mavoko.
sikatai hata ulaya hayo mambo yapo mfano TLC yalishawakuta hayo walikua wanaingiza mpunga mwingi ila wao waliishia kununuliwa magari, nguo na pesa kidogo ya matanuzi lakini badae wastuka wakaenda mahakamani kudai haki zao sema badae wakapotea baada ya left eye kufa
 
Show za michongo hizo hamna kitu usikute wao ndo wamelipa ili waonekane wapo vizuri kimataifa.
 
shida asipofumbua macho yeye atatengeneza nyimbo/jina ila Domo, tale,sallam na saidi fella wao ndio wanatengeneza hela, maana mikataba ya WCB ina walakini wale watoto wanakufa na tai shingoni ila kiukweli wanaumia hawapati kile wanachostahili kutokana na jasho lao
Hao wasanii wengine waliokuwa chini ya label nyingine wamemzidi nini Rayvanny? au nao wanaibiwa manake wana miaka miwili mfululizo wanatoa nyimbo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom