Ray C Alipotushukuru Ikulu

Ray C Alipotushukuru Ikulu

Rais wangu JK kwa mara nyingine sikuungi mkono katika suala hili. Ningekuona umefanya la maana kama ungetengeneza mifumo ya kudhibiti uingizwaji, usambazaji na matumizi ya mihadarati. Kumtibu muathirika tungechangishana wenyewe kama tunavyofanya kwa wagonjwa wetu wengine waliopo mahospitalini na majumbani mwetu.

Wewe tungekushukuru sana kama ungetuwekea mifumo ya kuhakikisha huu uchafu hauingii nchini na ma don wa madawa ya kulevya wote wanafikishwa mahakamani na sheria inachukua mkondo wake.

Hivi Rais wangu utajisikiaje ukisikia kwamba wale watu uliopewa majina kuwa ndio vinara wa kuingiza na kuuza madawa ya kulevya ndio hao wamemuuzia Ray C hizo cocaine?
 
Tulichagua tui la nazi tukifikiri ni maziwa, sasa tunayaona.
 
Jana hii ilizua mjadala mkali sana "mezani" kwetu......watu wanadai Rais kafanya la maana sana katika hili.....mimi sikuchangia mjadala ule


Tusikose kuwa wakosefu wa shukrani msada ni msada ashukuriwe kwa msaada wale , lakini ingekuwa ni bora zaidi kama ange wakazia sura askari polisi na pia kushirikiana na wananchi wenye uchungu na jamii zao kuwafichuwa wauzaji na waingizaji madawa kwa kupewa adhabu ya kutisha hapa tungeona maendeleo juu ya kadhia hii lakini kumsaidia mtu individual bado safari itakuwa kubwa, kwani ukweli hawa mateja ni ngumu sana kupowa ila huwa wanaacha kwa muda tu , lakini Mola amsaidie Ray C awe mwenye kupona moja kwa moja na wale low profile wa mitaani nao Mola awasaidie kuepukana na hii kitu.

Huyu dada Ray C kama kweli yupo katika kutaka kuachana na madawa angwataja wale waliokuwa wanamuuziawakatiwa nguvuni.

Hongera Rais ila na sisi tunaomba msaada huu uwafikirie na jamii na sio individuals.
 
Labda Ray C kampa list ya ma-pusher wote waliokuwa wanamletea mzigo wa unga halafu mkulu akawapigia na kuwaambia waache wenyewe kuuza unga la sivyo wataburuzwa mahakamani na kuchukuliwa hatua kali.
waache!! atawaambia wampelekee auze na ila ikipatikana itaenda kununua madawati na kwenye mradi wa kilimo kwanza
 
bora sura ya mwaikibaki 100 times!! matunda yameonekana. kuliko huyu HB wetu, lakini matatizo na vituko kila kukicha! UMASIKINI WA NCHI UMEONGEZEKA KWA 100% tangu kuingia kwake madarakani.

Wewe unaujuwa umaskini uliokuwepo Tanzania wakati wa Nyerere au unajisemea tu? makatambuga ndio yalikuwa fashe ukupenda usipende, magari chini yana matundu ukiingia na gari kwenye dimbwi la maji inabidi wewe uliomo ndani ya gari unanyanyuwa miguu. Nchi haina fedha kabisa benki, watu wote taabani, ukibeba kikapu unafunguliwa na mgambo kuona umebeba nini. Ashaakum si matusi mpaka "modess" za kina dada zilikuwa hazipatikani. Umeikuta neema wakati wa Kikwete unaona kuwa ni umaskini? unaendesha gari gani? muulize bibi'yako aliota kuendesha gari hata siku moja?
 
Back
Top Bottom