Ratiba ya chakula kwa bachela

Asubuh: Chai andaz
Mchana :Chips yai
Usiku : Chips yai na salad ya kabeji.
 
Ukifikia level za juu za ubachelor kama ufield martial hayo mambo ya ratiba za kula hayatakusumbua ...

Uliza mabachelor wazoefu kama le mutuz
 
Inatakiwa useme na kazi yako au kipato chako(kwa mimi ipo hivi)

Asubuhi(mtaani)
Supu na chapati mbili

Mchana(ofisini/mishemishe)
Ugali na mboga mboga au Samaki/kitimoto

Jioni(kabla ya mazoezi)
Kahawa na washikaji

Usiku(ghetto)
Wali/Ndizi mboga yoyote

Hapo utaona mambo yalivyomepesi mkuu lakini unaweza kubadili kulingana na kipato chako.......
 
Huwezi pata ushauri bora juu ya hili kama ratiba yako ya majukumu hujaisema. Je unatoka asubuhi unarudi jioni? Au unapopatia hela ni karibu na nyumbani kwamba unaweza rudi muda wowote? Una jiko? Unajua kupika?

Toa maelezo ya kutosha.
 
Kama una friji na sio mtu wakufanya shopping mara kwa mara,unafanya hv
-unanunua mikate miwili unaifunga minne minne kwenye vile vifuko transparent,af unaeka kwenye freezer.ukiamka asubuhi umtoa kimoja ukitoka kuoga kishayeyuka unakunywa
chai.
Ko hiyo ni 2000 kwa wiki kwa ajili ya kitafunio.
Unaweza pia ukala usiku njaa ikikushika

-Nunua nyanya za 3000 au 5000 unazikatakata au kukwaruza af unazichemsha unaeza ukaeka vinegar,pilipili,chumvi ka unataka,depends na your preferences.Unachemsha mpaka maji yanakauka af ikishapoa unaeka kwenye container unaeka kwenye friji.
unakuwa unachukua kidogokidogo ukipika mboga.Inakaa mwezi mzima.

-Nunua chai masala,tangawizi,ili chai iwe na mvuto.

- mchana ukiwa hauli nyumbani utaspend average amount kama 3000 per meal.15000 per week.60000 per month.

-nunua kuku wawili chemsha.Nyama nyingine funga kwenye container,nyingine unga weka kwenye container ndogo ndogo.
Budget:Kipisi kimoja per day.
(hata restaurant unapewa kipisi ko ukijiongezea unaharibu budget)
mimi nanunuaga wa kisasa 7000@

-Kama unependelea nyama ya ng'ombe pia chemsha gawa kwenye containers.uki defrost container moja usile mboga yote unakula kama unavokula home.sije ukamaliza kilo within two days.

-mboga za majani unanunua unachemsha na carrot unafunga kwenye containers au plastic bags zile transparent unafreeze.

-ukiondoka hom unatoa container la kuku/nyama na mboga kwenye freezer unaeka kwenye temperature ya kawaida.
ukirudi hom unabandika wali kwenye rice cooker unaoga unapasha mboga unakula,no mateso.

- jioni unanunua matunda,sometimes unaeza ukawa umechoka ukala tu matunda na kiporo cha wali wa jana.
unaeza pia ulanunua mihogo umachemsha unakula jioni na asubuhi.

- unaeza pia ukanunua sausage au mayai for luxury uwe unakula asubuhi pamoja na mkate.

- weekend hamnaga timetable.
These are the days napikaga ugali na chakula cha kula throughout the week kama ndizi,viazi,kutengeneza juice n.k

- Kujipikilisha ni jambo linalo evolve depending na mtu.Af pia idea nyingine za kusurivive unazipata ukifulia.
Nilikuwaga sio mtu wa budget naspend 10000 per day on food wakati nimepanga na kodi natoa nkaona huu upuuz.
Nulinunua friji,jiko,vyombo nikajipanga taratibu.
initial costs zinaweza kuwa kubwa ila its worth it.
Saiv i spend less than 70,000 per month on food.Na nakula vizuri.Compared na mara mbili yake na zaidi ukinunua chakula.
Mda wa kupika naupoteza tu sanasana jumamosi,kununua vitu na kuandaa menu.
Kila kitu kina cost yake.
 
Habari za jioni wakuu,mimi ni kijana niliyehamua kukimbia nyumbani na kwenda kuanza maisha,tatizo langu kubwa nashindwa kupangilia ratiba ya chakula,naomba tujulishane hapa ratiba nzuri asante
Kwa swali lako hili bora uludi kwenu tu,wewe bado ni mtoto hujakua.
 
Mayai mawili yasikosekani jikoni, nyanya na vituguu. Ni mboga ya chapchap na ugali ukibaki ni mkate wa asubuhi .Ukipata nafasi badilisha msosi. Hayo ni maisha ya kawaida kwa bachela
 
Kama huja yaishi maisha ya u bachelor huwezi kumuelewa jamaa... wanaume tulio wengi upikaji kwetu ni uvivu hivyo hufanya hata ratiba yakula isi eleweke... chai uta inywa saa 5 ambalo ni kosa, lunch uta ila saa 10 kosa tayari, dinner ni saa 4 usiku hadi saa 5. And the chain repeats!

1. Mkuu kwanza kabisa kale ka uvivu kaku pika kaondoe.
2. Acha kula hotelini.
3. Tafuta mtu waku kuoshea vyombo ( hapa ndio huwa mtihani hasa ukisha jua vyombo vifachu hata jiko hutaki kuliona bora ukale hotelini).
 
Back
Top Bottom