Rasmi Bodaboda wana nguvu kuliko Mamlaka?

Rasmi Bodaboda wana nguvu kuliko Mamlaka?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
16,979
Reaction score
26,081
Boda wana hela sana kwa siku wanaingiza pesa nyingi sana ushahidi upo kwenye mahojiano na vyombo vya habari wamesikika waking'aka kujenga majumba, kusomesha watoto shule Bora kabisa na kuwashangaa vijana wanaosema hakuna ajira wakiwaita wazembe na vilaza.

Sasa kama wana vipato hivyo kwa nini wasilipe kodi kujenga nchi?. Hawana uzalendo kabisa watu hawa. Wapewe kesi za uhujumu uchumi ikibidi uhaini kabisa kwa kukosa uzalendo na nchi yao.

Kwanza Bodaboda walirasimishwa lini kama vyombo vya usafiri mijini na hasa katikati ya Majiji?.
Kampeni ilikuwa ni kupunguza vyombo vingi vinavyobeba abiria wachache na kuongeza vikubwa vinavyobeba abiria wengi.

Tukaondoa Hiace tukaleta ya kuanzia abiria 30+ Haikutosha tukajenga na tukaanzisha Treni daladala, na mwendo kasi.

Sasa serikali hii ya mafisadi na kuhujumu mali za umma, zimefumbia macho Bajaj na Bodaboda huku zikihujumu huduma za sekta binafsi hasa mabus na malory, tena bila kujali adha wayoipata wananchi.
Bandari imebinafsishwa bila sababu za msingi, na zaidi jiji limefanywa bandari kavu mpaka kwenye makazi ya watu na maeneo ya Jeshi.

Hii haikubaliki kwa sababu bandari haina hasara, na kuna bandari kavu ya KWALA ambayo ikiungana na TRC ufanisi utakuwa ni mkubwa na tatizo la foleni litaisha Dar Es Salaam.
Mfikishieni CHALAMILA hii..

Soma Pia: Kuna rushwa kubwa na utaratibu usiofuatwa katika ukamataji wa Bajaj na Bodaboda

Latra hawana shida, wanakusanya kodi, kwenye bodaboda, mimi mwenyewe ni boda, watu wenye shida, ni wale askari wa jiji aisee hawa watu watatufilisi, yani wanavizia ukishusha abiria au ikipakia wanakukamata wanakupa kesi ya kupaki sehemu ambayo sio sahihi unawauliza hapa nimepaki au napakia abiria hawakueliewi lazi wakupeleke jiji na ukifika huko jiandae kulipa elifu 70, hawa ndio tunapaswa kuungana bodaboda tupambane nao.



 
Kuna maswali mengi tu huyo boda hawez jibu mf kijiwe chake kipo wapi,mshtukize muulize sasaivi boda sh ngp?,muulize amejengea wapi,mulize mtoto wake anasoma shule gani kwajina ada sh ngp then muulize pato lake kwa siku sh ngap na ukimaliza tembelea sehemu alipokutajia waulize boda wenzie,majirani,shule (mara nyingi hao wanaohojiwa ni watu wasiojulikana ila bodaboda waukweli wana hali ngumu,wanakesha adi usiku wa manane ili kupata marejesho,kodi na matumiz)
 
Ili boda upate 30k kwa siku inabidi ubebe abilia 30kwa1000,15kwa 2000,10 kwa 3000 au 6 kwa 5000 apo hujanunua mafuta,hujala,hujakopwa safari,hujaenda safar hewa, hilo jumba utalijengaje,mtt utamlipiaje ada ya 2m+ (au wanabeba mizigo ya moto,bangi,magendo)
 
Ila Boda balaa
Yaani ukifika jiji la Chalamila ndio utajua nao hawana tofauti na magari ya viongozi wakubwa tena wana ubabe wa ziada

Yaani Boda kwenye Traffic lights yeye hazimuhusu kabisa
Kupita wrong way hata jeshi hawafanyi ila wao ndio wenye nchi kutuzidi.
Na hakuna wa kuwafanya kitu, je wao ni nani kuwazidi serikali?

Huwa nikifika Dar najiuliza hawa wana nguvu kiasi gani mpaka wameshindwa kudhibitiwa?
Nimechomekea tu haka
 
Back
Top Bottom