Rasimu ya Samweli Sitta yalisambaratishia mbali taifa la Zanzibar

Rasimu ya Samweli Sitta yalisambaratishia mbali taifa la Zanzibar

Nashanga wapuuzi wachache wamekuwa wa kwanza kulipoteza taifa lao ambalo Mzee warioba amelipigania kulirudisha tena ambaye siyo mzanzibar Hakka watajuta Sana na kumkumbuka warioba
Poleni sana wadau. Tanzania yenye neema yaja
 
inamaana rais wa muungano hatakuwa na mgombea mwenza?
 
Hakika kwa hili warioba atakumbukwa tu
 
Itakuwaje Rais wa Muungano akiwa Mzanzibar ? Makamu wa kwanza naye Mzanzibar ? Huyu makamu ambaye watanganyika hawamchagui itakuwaje ?

Mkuu, maswali yako Ni ya msingi Na hawatakujibu, ila subiria Maneno machafu.
Kama nimeelewa vyema, rais wa JMT Ni lazima atoke Tanganyika Ili kusudi muundo Na mfumo vitekelezeke. Vinginevyo Ni move ya kufanya afanyavyo ngisi baharini hali inapokuwa tete... Mungu atupe uhai tuione hii hekima Na busara za bmk.
 
hii rasimu ya ccm inaendeleza tanganyika kuvaa koti la muungano siamini kama wanzazibari watauliwa taifa lao kirahisi na watanganyika kama watakubali
 
Kwa madaraka rais wa znz atauwa baada ya rais wa jamhuri ya muungano!. Maswali haya naomba tujiulize?
1. Atakaimu vipi urais wa muungano wakati huku bara hatukumchagua?
2.Kama rais ajaye wa muungano akawa kama wa sasa (kiguu na njia) je, huyo rais wa zanzibar atakuwa anaiacha ikulu yao na kuhamia magogoni?
3.Itakuaje makamu wa tanganyika awe wa pili kimlaka wakati tanganyika ni kubwa hivyo?
4.kwa utaratibu huo! Je inamaanisha tusahau kupata rais wa muungano toka zanzibar?
 
Mkuu, rais wa muungano haitajalisha kuwa ni mzanzibar au mtanganyika, huyu atakuwa anaongoza jamhuri ya muungano kwa mujibu wa hiyo rasimu. Cha kushangaza ni hapo kwa makamu wa rais ambao wanatoka pande tofauti na kuchaguliwa na watu wao kwa kila upande ila wamepewa hadhi ya kuongoza jamhuri ya muungano! yani ni full vihoja!

Kwa maana hiyo Ni serikali 3, siyo?
 
Kwa madaraka rais wa znz atauwa baada ya rais wa jamhuri ya muungano!. Maswali haya naomba tujiulize?
1. Atakaimu vipi urais wa muungano wakati huku bara hatukumchagua?
2.Kama rais ajaye wa muungano akawa kama wa sasa (kiguu na njia) je, huyo rais wa zanzibar atakuwa anaiacha ikulu yao na kuhamia magogoni?
3.Itakuaje makamu wa tanganyika awe wa pili kimlaka wakati tanganyika ni kubwa hivyo?
4.kwa utaratibu huo! Je inamaanisha tusahau kupata rais wa muungano toka zanzibar?
Subirini mbona haraka? Rasimu ya Tatu ina majibu ya maswali yako
 
Poleni sana wadau. Tanzania yenye neema yaja

Yaja wapi? Nawatakao ileta ni wakinani? Kama imejengewa MSINGI mzuri ambao ni rasimu ya warioba Lakini ccm wameshindwa kuutumia msingi huo sasa Tanzania ipi hiyo ya Neema yaja? Ndugu tuache tu.
 
Mkuu, maswali yako Ni ya msingi Na hawatakujibu, ila subiria Maneno machafu.
Kama nimeelewa vyema, rais wa JMT Ni lazima atoke Tanganyika Ili kusudi muundo Na mfumo vitekelezeke. Vinginevyo Ni move ya kufanya afanyavyo ngisi baharini hali inapokuwa tete... Mungu atupe uhai tuione hii hekima Na busara za bmk.

Mkuu kwenye hiyo rasimu kama nilivyodokezwa ni hivyo. Ila kwa kutumia tu akili zetu tunaona kuwa rais wa muungano hajatambuliwa kwa sehemu ya nchi atokapo ila ametambuliwa kama mkuu wa nchi wa jamhuri ya muungano hivyo hata akitoka zanzibar mwisho wa siku atakula kiapo kuongoza muungano na hivyo atakuwa magogoni...Ninachoshangaa ni muundo wa muungano kuimeza sana Zanzibar na ndiyo maana kukimbia serikali tatu ni kitendo cha uwenda wazimu walichokifanya!!
 
Hatimaye rasimu ya Samwel Sitta ambayo inaitwa 'rasimu ya tatu' imeleta maumivu makubwa kwa wanaotaka mamlaka kamili ya Zanzibar, nimethibitisha.

Kwa mujibu wa rasimu hiyo ambayo kesho inatolewa kwenye bunge maalum la katiba ambalo CCM ndiye kiongozi, imependekeza kuwa rais wa Zanzibar awe makamu wa rais wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano huku rais atakayeongoza Tanzania bara ndiye atakayekuwa rais wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano na hivyo rasimu hiyo inatambua uwepo wa rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ana makamu wa kwanza wa rais( Rais wa Zanzibar) na makamu wa pili wa rais(waziri mkuu wa Tanzania bara) ila vyeo hivyo vimepewa hadhi ya 'umuungano' yaani makamu wa rais.

Kwenye hadhi hiyo ya 'umuungano' kuna rais, makamu wa kwanza na makamu wa pili kama ilivyoonyeshwa kwa mtiririko wa madaraka.

Ikiwa rasimu hiyo itapita, basi ni dhahiri itakuwa imeisambaratisha vibaya katiba ya Zanzibar inayomtambua rais wa Zanzibar kama mkuu wa nchi ya Zanzibar na hivyo italazimika kuundwa upya kwa katiba ya Zanzibar itakayoridhia Zanzibar kuongozwa na mkuu wa nchi wa Jamhuri ya Muungano.

Aidha rasimu hiyo ya tatu imeshindwa kuondoa mkanganyiko uliopo ambao unashindwa kuainisha nchi mbili zinazounda muungano na mamlaka ya kila nchi na hivyo kuendeleza wingu zito linaloonekana kwenye muundo huo.

Ikiwa Wazanzibar wataridhia kuipitisha basi watakuwa wameridhia kuishusha hadhi ya mamlaka ya nchi yao ambayo walianza kuipigania.Na ikiwa Watanganyika wataipitisha basi watakuwa wameridhia rasmi kuendelea kiiua Tanganyika na kuendelea kubeba mzigo wa Zanzibar.

Aidha rasimu hiyo inatarajiwa kuibua mgogoro mkubwa wa ardhi hasa kwa Zanzibar kwani inapendekeza kuwa ardhi ni ya watu wote wanaounda muungano na hivyo kutoa mamlaka kwa Watanganyika kumiliki ardhi Zanzibar.

kuna wakati nashindwa kuelewa watu uwa wanafikiri kwa kutumia nin kipengele cha rais wa znz kuwa makamu kilikuwepo kwenye katiba na ni hawa hawa wakina sita waliokiondoa 1995 baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza ilibidi kitolewe kutokana na hali ya mfumo huo na mwl alilisimamia hili, na sababu kubwa ilikuwa pale nchi2 zinapokuwa zinaongozwa na vyama tofautiinaweza ikaleta tatizoingawa c raisi kuona kwa haraka
 
UMERIPOTI UONGO! Mfano jambo la ardhi litakufa chini ya Rais Kwa Tanzania Bara na chini YA Rais wa Zanzibar KWA Zanzibar!
 
Back
Top Bottom