G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,486
- 39,965
Hatimaye rasimu ya Samwel Sitta ambayo inaitwa 'rasimu ya tatu' imeleta maumivu makubwa kwa wanaotaka mamlaka kamili ya Zanzibar, nimethibitisha.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo ambayo kesho inatolewa kwenye bunge maalum la katiba ambalo CCM ndiye kiongozi, imependekeza kuwa rais wa Zanzibar awe makamu wa rais wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano huku rais atakayeongoza Tanzania bara ndiye atakayekuwa rais wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano na hivyo rasimu hiyo inatambua uwepo wa rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ana makamu wa kwanza wa rais( Rais wa Zanzibar) na makamu wa pili wa rais(waziri mkuu wa Tanzania bara) ila vyeo hivyo vimepewa hadhi ya 'umuungano' yaani makamu wa rais.
Kwenye hadhi hiyo ya 'umuungano' kuna rais, makamu wa kwanza na makamu wa pili kama ilivyoonyeshwa kwa mtiririko wa madaraka.
Ikiwa rasimu hiyo itapita, basi ni dhahiri itakuwa imeisambaratisha vibaya katiba ya Zanzibar inayomtambua rais wa Zanzibar kama mkuu wa nchi ya Zanzibar na hivyo italazimika kuundwa upya kwa katiba ya Zanzibar itakayoridhia Zanzibar kuongozwa na mkuu wa nchi wa Jamhuri ya Muungano.
Aidha rasimu hiyo ya tatu imeshindwa kuondoa mkanganyiko uliopo ambao unashindwa kuainisha nchi mbili zinazounda muungano na mamlaka ya kila nchi na hivyo kuendeleza wingu zito linaloonekana kwenye muundo huo.
Ikiwa Wazanzibar wataridhia kuipitisha basi watakuwa wameridhia kuishusha hadhi ya mamlaka ya nchi yao ambayo walianza kuipigania.Na ikiwa Watanganyika wataipitisha basi watakuwa wameridhia rasmi kuendelea kiiua Tanganyika na kuendelea kubeba mzigo wa Zanzibar.
Aidha rasimu hiyo inatarajiwa kuibua mgogoro mkubwa wa ardhi hasa kwa Zanzibar kwani inapendekeza kuwa ardhi ni ya watu wote wanaounda muungano na hivyo kutoa mamlaka kwa Watanganyika kumiliki ardhi Zanzibar.