mkuu ni kweli ninayo lakini tangu saa kumi na mbili najitahidi kuitumbukiza inagoma sijui kama ni mtandao uko down au la.
Watanzania wakati umefika ni lazima tuondokane na mawazo mgando ya serikali mbili, ambazo utekelezaji wake ni mgumu sana kwa nyakati zetu hizi. Lazima tuambatane na fikra mpya na chanya za kuwa na taasisi zilizojengewa misingi ya kikatiba ya uwajibikaji. Demokrasia inayosemwa, sasa inatakiwa iingie kwenye matendo, kuliko kubaki nadharia tuu.
Mfumo huo mpya wa dola utapunguza sana gharama za uendeshaji wa Serikali na Bunge la Muungano kwa kiasi kikubwa, hivyo kuwapunguzia wananchi mzigo. Mfumo huo mpya wa serikali tatu ni cheaper(una gharama nafuu) kuliko mfumo wa sasa, kwasababu:
1.Mfumo mpya una mawaziri wachache(15) kuliko wa sasa(56).
2.Mfumo mpya una wabunge wachache(75) kuliko wa sasa(375).
3.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye wizara husika kuliko wa sasa.
4.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye ofisi za bunge kuliko wa sasa.
5.Mfumo mpya utakuwa na uwajibikaji mkubwa kuliko wa sasa, ambao mamilioni ya pesa za walipa kodi yanapotea.
6.Mfumo mpya hauna ofisi ya wazili Mkuu, hivyo gharama zote zilizopo sasa za kuiendesha ofisi ya PM na makandokando yake hazitakuwepo.
Hivyo basi, mfumo mpya wa dola unapunguza kwa kiasi kikubwa gahrama za uendeshaji wa dola.
Huu mfumo mpya ni mzuri na unaotekelezeka kirahisi, bila kuhitaji gharama kubwa. Mfumo huo upo Ujerumani,Marekani, Afrika kusini, Uingereza, India Nk
Mfumo huu mpya utatoa ajira nyingi kwa vijana wetu wasomi, kwasababu upatikanaji wa fursa za kazi hautakuwa unatawaliwa na mfumo wa kikilitimba, miungu watu, na kupendeleana kama ulivyo sasa. Kwani kwa sasa kupata kazi lazima uwe ulizaliwa ktk familia ya mwanasiasa fulani au unafahimia na mtu fulani maarufu, au utoe rushwa.
Naipongeza tume kwa kufanya kazi kisayansi.
Nashukura sana kwa comment yako isiyo na utafiti na yenye woga, mawazo mgando yasiyozingatia hitaji la wakati.
Zanzibar toka mwaka 1964 wanayo serikalia yao ambayo inaendesheka mpaka leo.
Tanzania bara(Tanganyika) inatakiwa iunde serikali yake kadiri ya uwezo na hitaji la kweli, siyo kupeana vyeo kwa hoja za kirafiki au kisiasa. Katika ulimwengu wa leo ambapo mambo mengi yanaendeshwa na private sector huhitaji kuwa na serikali kubwa.
Unless unataka kuwapa kazi ndugu na rafiki zako. Kwa Tanzania bara mawaziri 12 watosha kabisa. Idara katika wizara zepewe mamlaka makubwa ya kuamua mambo. This to me is the best solution.
Kwasasa halipo ila linakuja.Mabunge ni mangapi jamani? Je bunge la tanganyika lipo?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Ni lini wananchi walikuwa na mzigo mwepesi? Zanzibar, bon voyage and God bless youRasimu ya katiba iliyozinduliwa jana inatupa matumaini bali binafsi naona serikali tatu ni mzigo kwa wananchi. Serikali ya muunganoitakua na wabunge 75 na mawaziri wasiopungua 15. Lakini serikali hii itategemea mapato yake kutoka serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar. Watakaoumia zaidi kuibeba ni Tanzania Bara. Sielewi kabisa bunge na mawaziri wa muungano watakua wanafanya nini wakati kila upande wa hizo serikali mbili kuna wabunge na mawaziri wao. Naona pengine tuchague tu rais wa muungano halafu kila upande kuwe na waziri mkuu mtendaji atakaechaguliwa na wabunge wa serikali hiyo. Kwa staili hiyo tutaepuka mzigo mkubwa.
Mkuu acha kuwapotosha watu! tulia soma vizuri rasimu! hao 15 ni wa shirikisho tu, bado wa Tanganyika! upo hapo?
Sio kweli Kuwa serikari Tatu ni nafuu ebu toa mfano wa taifa changa lenye serikari tatu lenye maendeleo? ZNZ akiongoza Gavana na Huku Tanganyika akaongoza Gavana mmoja tu huku Rais Akiwa mmoja anayekaa Dodoma Hakuna gharama unakuwa muungano nafuu kuliko Nchi masikini Kuwa na Marais Watatu.Demokrasia ina gharama zake. Mfumo huo mpya wa serikali tatu ni cheaper(una gharama nafuu) kuliko wa sasa kwasababu:
1.Mfumo mpya una mawaziri wachache kuliko wa sasa.
2.Mfumo mpya una wabunge wachache kuliko wa sasa(375).
3.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye wizara husika kuliko wa sasa.
4.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye ofisi za bunge kuliko wa sasa.
5.Mfumo mpya utakuwa na uwajibikaji mkubwa kuliko wa sasa, ambao mamilioni ya pesa za walipa kodi yanapotea.
Hivyo basi, mfumo mpya wa dola unapunguza kwa kiasi kikubwa gahrama za uendeshaji wa dola.
Naipongeza tume kwa kufanya mambo kisayansi.
Zipo Rasimu mbili?