RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

hizi ndizo gharama za muungano; serikali 3 hazikwepeki unless muamue kujunja muungano kila mtu abakie ki-vyake.
 
hii itakuwa nzuri kwanini tuwabebe tuuuuu na kuleta mlundikano wa vilaza bungeni??tunataka wanawake wenye uwezo kama akina Prof Tibaijuka, anna Kilango, halima Mdee....etc sio kwasababu ana matiti na anavaa sketi basi apewe free ride kuenjoy kiyoyozi na kodi zetu bungeni......

Hapo kwa anna kilango sipo kwani haeleweki kakaa kiushabiki zaidi.
 
Watanzania wakati umefika ni lazima tuondokane na mawazo mgando ya serikali mbili, ambazo utekelezaji wake ni mgumu sana kwa nyakati zetu hizi. Lazima tuambatane na fikra mpya na chanya za kuwa na taasisi zilizojengewa misingi ya kikatiba ya uwajibikaji. Demokrasia inayosemwa, sasa inatakiwa iingie kwenye matendo, kuliko kubaki nadharia tuu.

Mfumo huo mpya wa dola utapunguza sana gharama za uendeshaji wa Serikali na Bunge la Muungano kwa kiasi kikubwa, hivyo kuwapunguzia wananchi mzigo. Mfumo huo mpya wa serikali tatu ni cheaper(una gharama nafuu) kuliko mfumo wa sasa, kwasababu:
1.Mfumo mpya una mawaziri wachache(15) kuliko wa sasa(56).
2.Mfumo mpya una wabunge wachache(75) kuliko wa sasa(375).
3.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye wizara husika kuliko wa sasa.
4.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye ofisi za bunge kuliko wa sasa.
5.Mfumo mpya utakuwa na uwajibikaji mkubwa kuliko wa sasa, ambao mamilioni ya pesa za walipa kodi yanapotea.
6.Mfumo mpya hauna ofisi ya wazili Mkuu, hivyo gharama zote zilizopo sasa za kuiendesha ofisi ya PM na makandokando yake hazitakuwepo.

Hivyo basi, mfumo mpya wa dola unapunguza kwa kiasi kikubwa gahrama za uendeshaji wa dola.
Huu mfumo mpya ni mzuri na unaotekelezeka kirahisi, bila kuhitaji gharama kubwa. Mfumo huo upo Ujerumani,Marekani, Afrika kusini, Uingereza, India Nk

Mfumo huu mpya utatoa ajira nyingi kwa vijana wetu wasomi, kwasababu upatikanaji wa fursa za kazi hautakuwa unatawaliwa na mfumo wa kikilitimba, miungu watu, na kupendeleana kama ulivyo sasa. Kwani kwa sasa kupata kazi lazima uwe ulizaliwa ktk familia ya mwanasiasa fulani au unafahimia na mtu fulani maarufu, au utoe rushwa.

Naipongeza tume kwa kufanya kazi kisayansi.
Serikali ya muungano bado kubwa na imebeba mambo mazito tunataka wazanzibari tuyapunguze,kwanza

Uraia - kila mtu na uraia wake, tanganyika na zanzibar
Mambo ya nje-kila mtu na yake tanganyika na zanzibar,
Usalama na ulinzi - Yaondolewe.
Sarafu na Bank kuu
Vyama vya siasa-
ushuru -

Jina la muungano libadilishwe- nembo ya muungano ibadilishwe , muchukuwe wenyewe watanganyika- tunataka nembo mpya ambayo itakayo wakilisha pande zote za muungano, bendera mpya hio ni ya tangnyika, wimbo wataifa mpya.

Wabunge wapungue kutoka 70 mpaka 40, 20 zanzibar 20 tanganyika,na mawaziri hatuhitaji wengi inategemea na mambo tutakayo shirikiana 15 ni wengi sana ni mzigo .
 
Napenda nitoe hoja kuwa suala la kusema ili mtu awe waziri lazima awe na shahada ya chuo kikuu, ni uoza mkubwa.

Kwanza ifahamike nchi ya TZ ni ya watanzania wote, waliosoma na wasiosoma, wenye digrii na wasionazo. Mbaya zaidi walisionazo ni wengi kuliko walionazo, kama kwamba haitoshi waliona digrii hizo, hadi 2 au 3, wengine wamekuwa maprofesa ktk historia ya nchi hii ndo wamesaliti taifa kwa kiwango kikubwa. Ni kuendelea kuingia mtego iwapo tutaweka kiwango cha digrii kama entry marks za kuwa waziri. Vyeti kwa TZ imekuwa tatizo kubwa watu wanaveti tena visafi sana lakini hawana taaluma hata chembe, je tukabidhi nchi kwa wenye vyeti bila taaluma wapo wengi hadi baraza liliopo tunao.

Pili huu mfumo wa kuandaa mazingira kuwa waliosoma ndo watafaidi keki ya taifa ni uupuzi mtupu. Ni ubaguzi wa hali ya juu, hata wasio na digrii ni watu tena wanafaa sana ktk maendeleo ya taifa hili wapo wengi, Sokoine, Kawawa, Mrema na wenzao walifanya makubwa bila ya madigrii yenu.

Kama baada ya watu kupata elimu hasa ya digrii ndo taifa linaibiwa sana kwa mikataba mibovu, je tunawezaje kuweka mayai yote kwenye kikapu cha digrii au zaidi? Je elimu hii imetuandaa ili tuweze kutapelika au kutukomboa? tunaifahamu elimu tunayoisema hapa au tunadandia karandinga breki ya kwenza mahabusu?

Kama ni vema kujaribu kutumia madigrii ya vyeti kuendesha nchi, basi ni zamu ya wasio na digrii kuendesha nchi. wasomi wa TZ wametuangusha sana kiasi hizo digrii zenu hazina maaana kabisa.

TUNATAKA WAZIRI AWE MCHAPA KAZI NA MKWELI, pengine ni muhimu kujua kiingereza, Kifaransa, Kichina na SIO LAZIMA AWE NA DIGRII. SIO MUHIMU KABISA.

Naomba kuwasilisha
 
I can see Zanzibar separating under the 3-government arrangement. The separatists have all the reasons to be happy.
 
Haina shida ndugu ni vizuri kuwa mchapakazi LAKIN ni vizuri zaidi akiwa mchapakazi na msomi pia. Lakini pia huyo mchapakazi asiye na digrii anaweza kupewa kazi nyingine kwani kazi ni uwaziri peke yake?? Na kumbuka mawaziri hawatakuwa wabunge kwa hiyo Rais atakuwa na uwanja mpana wa kuchagua wataalamu wasomi na wachapakazi pia. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mimi ningependa iwe kinyume cha yote uliyosema! Ujinga kamwe hauwezi kutoa wachapakazi. Ujinga ni adui mkubwa na kipimo cha kumshinda adui huyu ni elimu, tena elimu ya juu.
 
Tusitegemee la maana. Sanasana ni kukamilisha ratiba tu, maana ni kama bora liende!
Kama Tundu Lissu anaundiwa mzengwe wa kumwagwa Bungeni kwaajili ya katiba hii, unategemea kuna jema lolote kwa Mtanzania humo?
Its sadenning, maana nchi zingine kama zinatokea kuwa makini kupita kiasi, basi ni wakati wa kuandaa katiba. Lakini hawa wenzetu issue ni kuangalia maslahi ya makundi katika katiba!
The move is Kill Them Before They Grow!

Acha upumbavu wewe tundilisu ni mpuuzi tuu,mnamtukuza wapuuzi wenzake,Chadema ni wehu sana masanuri yanawabana baada ya kuona umakini wa time,mnapenda ushetani na uzushi,Tundu lisu ni nani aundiwe zengwe acheni ushenzi wenu,,mmekaa umbea kama wana wakike,na subirini kama mtapata jumbo hata moja kwenye bunge la Jamhuri,sasa hivi masaburi yanapwita,angalia kazi ya tume ilivotukuka,kila mtanzania mzalendo ukiacha magaidi chadema ameguswa
 
Its a wastage of resources kuwa na serikali tatu.

If we are seriously into our Union, tuwe na serikali moja.

I see this as a diversion into the facts that need be addressed.

Mambo yote ambayo ni controversial na tyalionekana na wazee wetu hapo mwanzo, (Karume na Nyerere) yamo humu ndani).

I see a clear and crystal intwntion to diversify us from facts such as poverty and natural resources.

Tutaachwa tukijadili haya mambo watu wakifanya yao.

I suggest katika rasimu mpya neno Tanzania Bara be removed and replaced by Tanganyika, Hakuna kitu kama TANZANIA BARA bali kunaTanganyika.
 
Demokrasia ina gharama zake. Mfumo huo mpya wa serikali tatu ni cheaper(una gharama nafuu) kuliko wa sasa kwasababu:
1.Mfumo mpya una mawaziri wachache kuliko wa sasa.
2.Mfumo mpya una wabunge wachache kuliko wa sasa(375).
3.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye wizara husika kuliko wa sasa.
4.Mfumo mpya utakuwa na wafanyakazi wachache kwenye ofisi za bunge kuliko wa sasa.
5.Mfumo mpya utakuwa na uwajibikaji mkubwa kuliko wa sasa, ambao mamilioni ya pesa za walipa kodi yanapotea.

Hivyo basi, mfumo mpya wa dola unapunguza kwa kiasi kikubwa gahrama za uendeshaji wa dola.

Naipongeza tume kwa kufanya mambo kisayansi.

Hayo yote uliyoyasema ni kuhus serikal ya Shirikisho vp kuhus serikal ya Tanganyika na mwenzake Zanzibar? Ukubwa wa serikal utapungua au ndo utazidi ikizingatia kuwa serikal zote zinapaswa kugaramiwa na sis walipa kodi,hii rasmu ni ya shirikisho la Tanzania yaan hawa jamaa wameacha mambo mengi sana ya muhim kwa kujificha ktk hilo la Shirikisho!
 
Kama tutakuwa na serikali tatu, Zanzibar wajitegemee kwa kila kitu wenyewe, hatutaki pesa za watanganyika zitumike kuendesha serikali Yao, wasiruhusiwe kumiliki ardhi Kama wabara hatuwezi kumiliki ardhi Zanzibar,Mia.
 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imependekeza katika rasimu ya Katiba Mpya ukomo wa wabunge na kufutwa kwa nafasi za Viti Maalumu bungeni.(MWANANCHI)
haya (HASA WAKINAMAMA) sasa muanze kujifunza kujieleza kwenye halaiki ya watu, sio kusubiri HISANI.
 
lakini umeona pendekezo kuwa wabunge wawili wawili wakiume na wakike? bado namba ya wabunge wa ccm itakuwa kubwa sana bungeni kwa style hii.... mark my word.. this has to be fought by all means....
 
Nafikiri Hakuna sababu ya kuwa na marais watatu, tuwe na mawaziri wakuu wawili yaani waziri mkuu wa bara na waziri mkuu wa Zanzibar ambao watakuwa na mamlaka kamili ya nchi zao wanazoziwakilisha kwenye serikali ya shirikisho na tuwe na raisi mmoja wa shirikisho tu.
 
Unaweza kuna na jambo la maana la kujadili lakini tumia Kiswahili kwa sababu neno "diversify" hapo juu halina maana uliyokusudia. You seem to have serious issues with the Queen's lingua franca. Look at your third phrase, just too out of conventional thinking.
 
'unajua bwana mdogo,mwenye ujuzi hawezi kuwa sawa na asiye na ujuzi hata siku moja bwana mdogo...............halaf pia,we unachotaka kutuletea hapa ni suala la ONE IN A MILLION bwana mdogo hatukatai kuwa wapo wenye vipaji na upeo wa kuongoza ilhali hawajasoma saaaaaana hilo skatai ila kati ya milioni moja yupo mmoja bwana mdogo.

Unachomaanisha ni tofauti kabisa na unachowasilisha kwa maana hii hapa;umesema watu wana vyeti lakini taaluma hawana kwa mana ni vyeti feki si ndio bwana mdogo?,hivyo hukutakiwa kuiweka mada yako hivyo ulivyoiweka dogo ulitakiwa kusema wenye (vyeti feki sasa wasipewe madaraka) kwa kifupi ungezungumzia vyeti na sio digrii bwana mdogo.

Siwezi kujua wewe ni dini gani lakini hata kama utakuwa ni dini gani ukitazama historia ya mitume na manabii waliokuongoza walikuwa wanapewa elimu na kufundishwa na MUNGU ili na wao wakawafundishe watu wengine na kuwaongoza na sio vinginevyo la sivyo hautaweza kuwaongoza dogo sasa ukisema mawaziri wasiwe wasomi ndio utawakaribisha wakina JUMA NATURE na kina DIAMOND wawe mawaziri,acha wawe wabunge tu kwa mana wanawatetea hao wafuasi wanaowapenda ndo mana wakawapa [COLOR=#f0000]KULA[/COLOR] bwana mdogo lakini sio uwaziri acha mawazo mtindi yamechacha hayo kuwa na mawazo tanga fresh bwana mdogo usirudie tena,sawa?'
 
Jana wakati jaji warioba anawasilisha hotuba yake kwa wananchi kuhusu rasimu ya katiba mpya, alipofika kwnye kipengele cha umri unaofaa kugombea urais na kutaja kuwa tume inapendekeza umri ubakie kama ulivyo hivi sasa wa miaka 40, zitto kabwe, mbunge wa kigoma kaskazini, naibu katibu mkuu wa chadema nusura alie..alinuna, akakunja uso na mbaya zaidi kamera ya tv ilimmulika na kuonekana na taifa zima lililokuwa likifuatilia tukio hilo..

my take: katiba mpya ni mwanzo wa mwisho wa zitto kisiasa? Mana alisema hatgombea tena ubunge hope alikuwa na malengo flani
 
Mtoa mada siungi mkono hoja yako .. kwa dunia ilivyo sasa wangeka kabisa minimum postgraduate degree.. elimu ndio kila kitu ..

Nchi kama China viongozi hawateuliwi wala hawapigiwi kura bali kuna mitihani maalumu mnafanya baada ya kukidhi vigezo flani ikiwemo elimu..

Nchi inaongozwa na wasomi tena sio waliomeza wakabahatika kupata hako ka degree bcz kuna mchujo wa paper .. ndio unapewa ukuu wa wilaya ..

Tanzania tungekuwa na system hii tungefika mbali sana
 
Naona hii itatupunguzi mzigo wa watu kupeana madaraka kama hawana akili nzuri. Hawa design ya Vick Kamata hakuna tena 2015 waanze kuaga sasa.

Mkuu sio Vikiy Kamata pekee......! Wako wengi kiasi kua wengine baada ya kusikia jana hizi taarifa walichanganyikiwa. Safi sana. Wengi wa Wabunge wa Viti maalum especialy wale "MAYALA" wa CCM hakuna wanachofanya zaidi sana ni kupeleka Ushabiki na NGONJERA bungeni.

Mfano mdogo tu huyo VIKIY KAMATWA! Huwa anaongea nini Bungeni zaidi ya Mipasho na kujipendekeza kwa waliompa huo Ubunge.
Wale wote ambao walikua mstari wa mbele kuwazomea wabnge wa CDM imekula kwao. Wananchi huku nje tunawajua vizuri kua nani mmshabiki bungeni na nani Mtetea wananchi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom