Rasimu ya Katiba inayopendekezwa 2014

Rasimu ya Katiba inayopendekezwa 2014

Profesa

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
903
Reaction score
627
Ndugu wana jf... Kilichosomwa bungeni tayari kwa kujadiliwa na bunge kabla ya kupigiwa kura hiki hapa....
 
Attachments

Asante sana Mkuu. Hata hivyo kabla sijaipakua, naomba kufahamishwa kama Kadhi yumo au hayumo.
 
Asante sana Mkuu. Hata hivyo kabla sijaipakua, naomba kufahamishwa kama Kadhi yumo au hayumo.
Soma ibara ya 40

Uhuru wa imani ya
dini
40.-(1) Kila mtu ana uhuru wa mawazo, dhamiri, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani
yake au kutokuwa na imani na dini.
(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni
huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ilimradi hakiuki sheria za nchi.
(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli
za mamlaka ya Serikali.
 
Mkuu, kadhi wa nini, hatumtaki hapa nchini kwetu. Aende huko wanako chinjana
 
Rasimu hii ikipitishwa na wananchi itakuwa karata ya kupitishwa kugombea kiti cha Urais kwa Mh Samwel J Sitta.
 
Ndugu wana jf... Kilichosomwa bungeni tayari kwa kujadiliwa na bunge kabla ya kupigiwa kura hiki hapa....

RASIMU ya CCM imetengenezwa pasipo kuangalia BANGO KITITA ni majanga
 
Rasimu hii ikipitishwa na wananchi itakuwa karata ya kupitishwa kugombea kiti cha Urais kwa Mh Samwel J Sitta.

Mtu mwenyewe kajizeekea anatembea kama ana nyata..hes 76 i guess..mwache ajifie..hatutaki kijeba kama Shimon Perez
 
Nashindwa kuelewa pale wanaposema 'Serikali ya Jamhuri ya Muungano' na 'Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar'. Sasa hiyo serikali ya Jamhuri ya muungano ni ya muungano wa nchi gani nyingine maana zaidi ya hapo tumeelezwa kuwa kuna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katiba ni kitu muhimu sana ambapo kila kitu kinahitajika kuwekwa bayana bila kuwa na utata. Naona hili hawakutaka kuliona na kulizingatia.
 
TUME HURU YA UCHAGUZI
(a) Tume Huru ya Uchaguzi
Kuundwa kwa
Tume Huru ya
Uchaguzi
211.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya
Muungano itakayoitwa "Tume Huru ya Uchaguzi".
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya
kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa
kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
 
Hivi hii ni tume huru kama wajumbe wanateuliwa na raisi
 
g) Wakuu wa Mikoa
Wakuu wa Mikoa
118.-(1) Kutakuwa na Mkuu wa Mkoa kwa kila mkoa katika Jamhuri ya
Muungano ambaye, bila kuathiri ibara ndogo ya (3), atakuwa ni kiongozi katika
Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Wakuu wa Mikoa katika Tanzania Bara watateuliwa na Rais baada ya
kushauriana na Waziri Mkuu.
(3) Wakuu wa Mikoa katika Zanzibar watateuliwa na Rais wa Zanzibar.
(4) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (5), kila Mkuu wa Mkoa,
atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano katika Mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo,
atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria
kama ni kazi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote
yatakayotajwa na Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
(5) Pamoja na wajibu na madaraka yake yaliyotajwa kwenye masharti
yaliyotangulia ya Ibara hii, Mkuu wa Mkoa wa mkoa wowote katika Zanzibar
atatekeleza kazi na shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
atakazokabidhiwa na Rais wa Zanzibar, na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya
1984 au sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
 
Lengo la katiba mpya ni pamoja na kupunguza madaraka
 
HII naona kama sawa na ile ya mwaka 1977 au nimekosea...sioni jipya

b) Baraza la Mawaziri
Baraza la 109.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano
Mawaziri ambalo litakuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Rais;
(b) Makamu wa Kwanza wa Rais;
(c) Rais wa Zanzibar ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais;
(d) Waziri Mkuu ambaye ni Makamu wa Tatu wa Rais; na
(e) Mawaziri wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais ataongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri, na endapo Rais
hayupo, mikutano itaongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais na kama wote
wawili hawapo, Waziri Mkuu ataongoza Mikutano hiyo.
 
Nakubaliana kwa mara ya 75 na Prof. Kabudi kuwa kama hawa jamaa wangelikubali kuwa ni wajinga na kutafuta uelewa kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba basi wangeliweza kuelewa ni kwa nini mchakato wa Katiba ulianzishwa wakati tunayo katiba tayari.
Kwa hiyo up.umba.vu ilikuwa ni kujifanya hawaitaki kabisa rasimu kwa maana haitaki mawaziri kuwa wabunge, wakuu wa mikoa, ukomo wa ubunge nk, sasa hii si ndio ile ile ya 1977!?
Pesa na muda vyote vimeshapotea na askari wanaongeza gharama kwa kuwatisha UKAWA/cdm wasieleze ukweli huu!
 
SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
SEHEMU YA KWANZA
JINA, MIPAKA, ALAMA, LUGHA NA TUNU ZA TAIFA

Alama na Sikukuuza Taifa
3.-(1) Alama za Taifa zitakuwa ni:
(a) Bendera ya Taifa;
(b) Wimbo wa Taifa; na
(c) Nembo ya Taifa,
kama zitakavyoainishwa katika sheria za nchi.
(2) Sikukuu za kitaifa zitakuwa:
(a) S
iku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe
9 Disemba;
(b) Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe
12 Januari;
(c) Siku ya
Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar, itakayoadhimishwa
tarehe 26 Aprili; na
(d) sikukuu nyingine zitakazoainishwa na sheria za nchi.
(3) Kila sikukuu ya kitaifa itakuwa ni siku ya mapumziko
 
Back
Top Bottom