Rasimu ya Katiba inayopendekezwa 2014

Rasimu ya Katiba inayopendekezwa 2014

Wadau nimepitia Rasimu iliyowasilishwa kwa Mwenyekiti wa BMK kwa kweli ni kituko. Yaani ni kama ilani ya CCM wamejiandalia na si Katiba. Rais amebaki na Mamlaka yale yale ya kuteua hadi wakuu wa wilaya bila kudhibitishwa na chombo kingine. Kwa kifupi nakala ya rasimu hiyo ipo wadau msome then mje mtuambie kama kweli hii ndo rasimu ya katiba au ilani ya CCM.
 
Baba wa Taifa alifanya mengi mazuri. Lakini sijapata jibu ni kwanini alitokea kuchukia kiasi hicho neno Tanganyika! Kwamba ukitamka neno Tanganyika unaonekana kama Shetani! Eti Uhuru wa Tanzania Bara; kwa hili Mwalimu alikosea sana.
 
nimemsikia chenge, dhamira za ccm ndo zinafanya kazi. nashauri waachwe waendelee na ratiba zao ila wataumbuka.
 
Katika jambo ambalo nyerere alichemka ni kuiua tanganyika na kuacha hai zanzibar. Jambo hili litatishia au kuvunjika kwa muungano kabisa!
 
Wadau nimepitia Rasimu iliyowasilishwa kwa Mwenyekiti wa BMK kwa kweli ni kituko. Yaani ni kama ilani ya CCM wamejiandalia na si Katiba. Rais amebaki na Mamlaka yale yale ya kuteua hadi wakuu wa wilaya bila kudhibitishwa na chombo kingine. Kwa kifupi nakala ya rasimu hiyo ipo wadau msome then mje mtuambie kama kweli hii ndo rasimu ya katiba au ilani ya CCM.

- Hata mngekuwepo msingebadili anything CCM ndio Chama TAWala ok!!

Le Mutuz
 
Binafsi nitaendelea kudai mamlaka ya nchi yangu TANGANYIKA kwa namna yoyote ile,na December baba yetu ametuita kwenda kugawiwa ardhi;Mimi nitaita sehemu ya ardhi nitakayopewa na dingi "Nchi ya Tanganyika"Maana naona 'waswahili' wanatemea mate ardhi hii ya maziwa,asali,almasi ya babu yangu.
 
Si nia yangu ya kuzungumzia tabia binafsi ya mtu, lakini linapokuja suala kubwa na la kitaifa kama hili la kuandika Sheria Mama ya Nchi, hivi ndiyo CCM ilikosa mtu mwenye mikono misafi ya kutuandikia Katiba Mpya? Nimeipitia katiba yake mpaka nimeona aibu kama mtanzania kwa sababu imeandikwa huku mtu akijitazama dhamira yake na kuweka vitu ambavyo havita mgusa kwa sababu tayari amesha "chafuka mikono"!

Kama Taifa tujitazame, hivi Chenge anaweza kutuandikia Katiba ya Nchi....Kweli? HAPANA tumepotea! Vifungu vingi vinamuajibisha moja kwa moja mwananchi na inaelekeza sheria nyingine zitatungwa kumuwajibisha mwananchi. Haitofautiani na Katiba hii ya sasa, ambayo madaraka aliyopewa mwananchi ni kupiga kura kumchagua kiongozi kisha akae mita 200, asisogelee hata sanduku la kura mpaka baada ya miaka mitano!

Katiba ya Sitta na mwandishi wake Chenge, inatoa madaraka makubwa kwa viongozi na watendaji wa umma na wasiwajibishwe moja kwa moja na wananchi kwa mujibu wa katiba hii. Kama mwananchi tumenyimwa nguvu ya kikatiba ya kumuwajibisha kiongozi au mtumishi wa umma, basi wananchi tutaendelea na tabia ya "KULALAMIKA" kama awali, kwa maana hatuna nguvu ya kikatiba ya kutenda! Na tukisema "tutende", virungu, maji ya kuwasha na risasi zitatuangukia.

Hii ni Katiba iliyoandikwa na Viongozi kwa wananchi na si Katiba iliyotungwa toka maoni ya wananchi kwa viongozi. Tumerudi miaka 50 nyuma!
 
Ardhi maliasili na mazingira yamewekwa kuwa mambo ya muungano katika sura ya tati lakini nashangaa hayapo katika orodha ya mambo ya muungano. Je ni muendelezo wa ardhi ni ya wote ila yao ya kwao?
 
Hii katiba hamna jipya. Ni kama walichukua ya zamani na kuongeza vijisehemu kadhaa basi!
 
Chenge: uzalendo sio tunu ya taifa kwasababu mtu hazaliwi akiwa mzalendo, uzalendo unatengenezwa tena kwa muda mrefu. Chenge tena: moja ya uzalendo ni lugha ya taifa. My take. hivi mtu anazaliwa akiwa anajua lugha ya taifa, nisaidieni jamani nyie ambao angalau mlimaliza darasa la saba, mi hali yangu mbaya kielimu
 
Chenge na waliokuwa wanamgongea meza ni wa kupuuzwa
 
Back
Top Bottom