RASIMU Katiba Mpya: CHADEMA yaitisha Kamati Kuu ya dharura, yamtega Waziri Mkuu Pinda


Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Likes
310
Points
180
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 310 180
CHADEMA wamtega Pinda

Katika hatua nyingine, CHADEMA imemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutimiza ahadi yake ya kuleta muswada wa marekebisho ya sheria iliyounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya ili kuepusha mkanganyiko kwenye mjadala wa rasimu iliyotolewa.

Msimamo wa kambi hiyo, ulitolewa jana mjini hapa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akisema kuwa Pinda ameshindwa kusimamia maneno yake, hivyo kuruhusu Bunge kupoteza muda wa siku tano tangu Juni 7 hadi 12 pasipo kuleta muswada huo.

“Mtakumbuka Aprili 4 mwaka huu, Kiongozi wa kambi, Freeman Mbowe katika hotuba yake kwa ofisi ya Waziri Mkuu alitangaza mambo mawili akitaka yatekelezwe, vinginevyo CHADEMA ingejitoa kwenye mchakato wa katiba mpya,” alisema.

Mnyika aliyataja mambo hayo kuwa ni kufutwa kwa mabaraza ya katiba kutokana na uchaguzi wake kugubikwa na rushwa na hila, pili ni kuletwa kwa muswada wa marekebisho ya sheria iliyounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Alifafanua kuwa hata Msemaji Mkuu kwa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu kwenye hotuba yake Aprili 30 mwaka huu, alisema wanaipa muda serikali ilete muswada huo kabla ya rasimu kutolewa.

“Waziri Mkuu aliahidi kutimiza sharti la pili la kuleta muswada, lakini hadi rasimu inatolewa ameshindwa kusimama katika maneno yake. Rasimu imetoka, lakini imeibua mjadala na ubovu wa mchakato ukiachwa utaathiri upatikanaji wa katiba mpya,” alisema.

Aliongeza kuwa rasimu hiyo imezua mjadala kuhusu muundo wa muungano kwa wananchi kuhoji ni kwanini rasimu inaleta muundo huo pekee pasipo kueleza mustakabali wa katiba ya Tanganyika.

Mnyika alieleza kuwa ubovu huo waliubaini mapema ndiyo maana viongozi wa chama hicho walipokutana na Rais Kikwete Ikulu mwaka jana, walimweleza kuwa sheria iliyounda tume ya katiba ibadilishwe ili hatima ya Tanganyika iingizwe kwenye mchakato ili maoni yaguse vyote kwa pamoja.

Mnyika alisema kuwa CCM wanajipanga katika mabaraza kujadili rasimu kwa vile wanajua kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo mbovu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatambua kwamba maoni yote ya mabaraza yana uzito sawa, hivyo tume inaweza kuchakachua.

Alisema CHADEMA kwa sasa hawataki kutoa maoni ya jumla kuhusu rasimu hiyo bali waipitie kwanza neno kwa neno pamoja na wanachama wao nchi nzima wakilinganisha na waraka namba moja wa mapendekezo yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya.

“Baada ya hapo, Kamati Kuu itakutana mwanzoni mwa Julai na kutoa uamuzi. Hata Bunge likimaliza muda wake bila serikali kuleta muswada huo, sisi kama kambi tutalirudisha suala hilo kwa Kamati Kuu ili kulitolea uamuzi,” alisema.

Akigusia kwa uchache maeneo yenye kasoro kwenye sheria hiyo, Mnyika alisema mamlaka na madaraka ya wananchi kwenye kura ya maoni yataporwa ikiwa Tume ya Uchaguzi inayolalamikiwa itaendelea kusimamia mchakato huo.

Pia alitaja mamlaka ya uwakilishi wa wananchi kwenye Bunge la Katiba ambalo kwa mujibu wa sheria hiyo ukiacha wabunge wa sasa, rais ndiye atateua wajumbe wengine baada ya kupokea mapendekezo ya makundi mbalimbali akisema yanapokwa.

Mbowe aitisha Kamati Kuu

Katika hatua nyingine, CHADEMA imeitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC), ili kujadili na kutoa msimamo wa chama hicho juu ya rasimu ya katiba mpya, iliyotolewa hivi karibuni, huku kikiwataka wananchi wote kuendelea kuichambua kwa makini na kutoa maoni yao kwa ajili ya kuiboresha.

Chama hicho kimesema kuwa kikao cha Kamati Kuu kitafanyika Jumamosi ya wiki ya kwanza, Julai mwaka huu, ambapo kwa muda wote uliobaki kimesema kitaendelea kuichambua rasimu hiyo 'neno kwa neno' kikisema kuwa ni muhimu kufanya hivyo kwani 'shetani hujificha kwenye maelezo'.

Mbali ya kuwataka wananchi kuisoma kwa makini rasimu hiyo, chama hicho pia kimewaagiza wanachama wote nchi nzima kupitia kwenye mfumo wake wa uongozi kuanzia ngazi ya chini ambayo ni misingi katika ngazi ya vitongoji, kuichambua rasimu kwa kuzingatia waraka namba moja wa chama hicho juu ya maudhui ya katiba mpya ya Tanzania, kisha wawasilishe maoni yao ili yazingatiwe kwenye maamuzi ya kikao hicho cha Kamati Kuu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe juzi mjini Ifakara, kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Ifakara, alipokuwa akimnadi mgombea wa chama hicho, Peter Lijualikali.

Mbowe alisema kuwa tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya itoe rasimu hiyo, chama hicho hakijatoa kauli yoyote, ili kupata muda wa kuisoma na kuichambua kwa makini 'neno kwa neno' nyaraka nzima, kisha kufanya mashauriano ya kitaalamu ndani ya chama, huku kikifanya maandalizi ya vikao kwa ajili ya maamuzi na hatimaye msimamo wao kwenye hatua hiyo ya mchakato wa katiba mpya.

“Ndugu zangu wananchi wenzangu wa Ifakara, katika mkutano huu wa kampeni za kumnadi mgombea wetu, naomba pia nitumie fursa ya kutoa tamko la kitaifa kuhusu suala muhimu sana na nyeti la katiba mpya. Tangu Tume imetoa rasimu ya katiba mpya, chama chenu kimekuwa kimya, kwa maana hakijazungumza, hii ni kwa sababu kadhaa.

“Kwanza kabisa tangu siku ya kwanza hadi leo, tumekuwa tukiipitia rasimu hiyo neno kwa neno, kipengele kwa kipengele, maana wanasema 'the devil lies in the details' yaani mzimu hujificha kwenye maelezo, sasa sisi kama mnavyojua tumekuwa chanzo na chachu kubwa ya mchakato huu hadi kufikia hapa ulipo, lazima tuwe makini katika msimamo wetu kama ambavyo imekuwa mara zote.

“Ilikuwa lazima pia tufanye mashauriano, wataalamu wetu waangalie mambo yote ya kitaalamu, neno kwa neno, kisha tukae vikao na kutoa msimamo wa chama chenu. Kama mnavyojua CHADEMA si Mbowe, si Slaa, wala si mtu mwingine yeyote, chama ni vikao. Hivyo tumeitisha kikao cha Kamati Kuu siku ya Jumamosi, wiki ya kwanza ya mwezi wa saba, kisha tutatoa tamko na msimamo wa CHADEMA katika rasimu hii ya katiba,” alisema Mbowe.

Aliongeza: “Wakati tunaendelea kuipitia rasimu hii hadi Kamati Kuu ikae, tunawataka Watanzania wote waendelee kuisoma kwa makini na kutoa maoni yao, lakini pia kwa msisitizo mkubwa kabisa, tunawaagiza wanachama wote wa CHADEMA katika ngazi ya msingi, kwenye vitongoji nchi nzima kukaa vikao, kuisoma na kuichambua rasimu kwa makini, kisha watuletee maoni yao kabla ya kikao hicho ili tuyazingatie kwenye maamuzi na utoaji wa msimamo wetu kama chama.

“Tunawakata wanachama wetu kuipitia rasimu yote kwa kurejea Waraka Namba Moja wa mwaka 2013 uliopitishwa na Baraza Kuu la chama mapema mwaka huu, hasa sehemu ya pili ambayo ilikuwa inaelezea maoni ya CHADEMA juu ya maudhui ya katiba mpya ya Tanzania.”

Mbowe akirejea kwa kutoa mifano namna chama hicho kilivyosukuma agenda ya katiba mpya kwa ajili ya mabadilio ya kimfumo na kiutawala kwa muda mrefu na kuweka msisitizo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, alisema kuwa watu wengi, hasa walioko madarakani leo, waliibeza CHADEMA, lakini leo wanakubali kuwa kiliona mbali.

Akitumia kaulimbiu maarufu ya chama hicho 'nguvu ya umma', Mbowe aliwataka Watanzania kuendelea kukiunga mkono katika kusimamia na kuhakikisha nchi inapata katiba mpya, huku akisema hawako tayari kuona wakuu wa wilaya na mikoa wakiendelea kuwemo kwenye katiba mpya.

Source; Tanzania Daima
 
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,249
Likes
4,696
Points
280
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,249 4,696 280
Source Tanzania Daima, teh teh teh...

Chadema wanamtega Pinda kwa mtego gani wa panya.
 
Tume ya Katiba

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
4,898
Likes
755
Points
280
Tume ya Katiba

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
4,898 755 280
Tanzania daima!!!! loh

Hivi cdm, kama ccm wakiamua kupitisha jambo bungeni wanashindwa nini ilihali wao ni majority! mbowe kweli janga la kitaifa.
 
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Likes
310
Points
180
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 310 180
Tanzania daima!!!! loh

Hivi cdm, kama ccm wakiamua kupitisha jambo bungeni wanashindwa nini ilihali wao ni majority! mbowe kweli janga la kitaifa.
Ndivyo unavyojidanganya. Kweli huna kumbukumbu. Nini kilitokea kwenye mswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Kama mnaweza kutumia wingi wenu bungeni, hasa wenye hili suala la katiba mpya, msingefanya mkutano wa hadhara Morogoro na kulia lia dhidi ya CHADEMA, baada ya ile hotuba kali ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Tunashukuru umekuwa wa mwanzi kupata taarifa hapa, wafikishie na wenzako.
 
Amiliki

Amiliki

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Messages
2,086
Likes
24
Points
135
Amiliki

Amiliki

JF-Expert Member
Joined May 6, 2011
2,086 24 135
Kwani anatofauti gani na panya? Kwanza ni hesima kubwa kuwa panya kuliko kuwa CCM. Inahitaji use na akili ya misukule kuweza kuendelea kuishabikia CCM.
 
PISTO LERO

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Messages
2,821
Likes
12
Points
135
PISTO LERO

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2011
2,821 12 135
Tumekusoma tumekuelewa tuyalifanyia kazi ipasavyo
 
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Likes
310
Points
180
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 310 180
Source Tanzania Daima, teh teh teh...

Chadema wanamtega Pinda kwa mtego gani wa panya.
Ritz

Kwa sentensi yako ya mwisho, maana yake unataka tuanze kukusaidia kusoma...hata kujua contextual meaning...kaka ni wewe kweli wa siku zote! Basi bora useme hivyo, uombe ieleweke.

Siamini pia kuwa uko fallacious kiasi hicho. Shambulia hoja. Lakini tunashukuru umekuwa mtu wa mwanzo kupata taarifa na utawafikishia wenzenu.
 
P

pembe

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
2,057
Likes
77
Points
145
P

pembe

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
2,057 77 145
Tunashukuru kwa ufafanuzi unaoeleweka. Nimekuwa nikijiuliza tutakuwaje na serikali tatu bila kuwa na katiba ya Tanganyika? Zanzibar tayari wanayo na waliipitisha kwa kura za maoni ya wananchi. Sasa sisi Watanganyika tutapitishaje katiba ya Muungano kabla ya kuwa na katiba ya Tanganyika? Kumbuka muda ni muhimu sana katika shughuli hii nyeti. Haraka haraka haina baraka.

Wananchi wakipitia waraka no. 1 wa CDM watakuwa wamejifunza mengi na itawafumbua macho kutoa maoni na katika upigaji kura yenyewe ya maoni ya katiba mpya. Je tume huru ya uchaguzi vipi?
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,914
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,914 2,483 280
Tanzania daima!!!! loh

Hivi cdm, kama ccm wakiamua kupitisha jambo bungeni wanashindwa nini ilihali wao ni majority! mbowe kweli janga la kitaifa.
suala la kupitisha au kutopitisha hoja bungeni kwa kuangalia wingi (chama) au nani kaleta hoja badala ya kuangalia uzito wa hoja ni tabia ambayo ilifaa itumike kipindi cha "Primitive Communalism' lakini sio katika zama hizi za "kidigitali".
 
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,914
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,914 2,483 280
Ritz


Siamini pia kuwa uko fallacious kiasi hicho. Shambulia hoja. .
Mkuu Tumaini Makene ;sina uhakika kama huyu ndugu yetu Ritz anaweza kuelewa neno ulilotumia hapo kwenye bold.Ni bora ungetumia lugha nyepesi.
 
Last edited by a moderator:
T

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,335
Likes
339
Points
180
Age
28
T

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,335 339 180
Mtakaa kutega watu mpaka lini,mkuu molemo hizi siasa za kutegana hizi mpaka lini sisi tunataka sera na hoja wala siyo mitego ya kutega watu mmetega watu wengi sana mbona matokeo chanya hatuyaoni? Tumechoka na mitego mkuu.
 
Chadema Diaspora

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Messages
479
Likes
220
Points
60
Age
30
Chadema Diaspora

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2010
479 220 60
Ritz

Kwa sentensi yako ya mwisho, maana yake unataka tuanze kukusaidia kusoma...hata kujua contextual meaning...kaka ni wewe kweli wa siku zote! Basi bora useme hivyo, uombe ieleweke.

Siamini pia kuwa uko fallacious kiasi hicho. Shambulia hoja. Lakini tunashukuru umekuwa mtu wa mwanzo kupata taarifa na utawafikishia wenzenu.
Huna haja ya kubishana naye wala kumuelewesha. Ni faraja kuona ame reply huu uzi, in other words- "amepata message."
 
S

Selungo

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2009
Messages
1,272
Likes
1
Points
0
S

Selungo

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2009
1,272 1 0
suala la kupitisha au kutopitisha hoja bungeni kwa kuangalia wingi (chama) au nani kaleta hoja badala ya kuangalia uzito wa hoja ni tabia ambayo ilifaa itumike kipindi cha "Primitive Communalism' lakini sio katika zama hizi za "kidigitali".
Kiongozi!

Umenikumbusha mbali wakati nasoma somo la Historia A- Level. Kwa maana hiyo MAGAMBA bado wana chembe za UJAMAA WA UJIMA, kitu ambacho kimepitwa na muda, eti? Pokea 5 yako.
 
N

Njaare

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2010
Messages
1,080
Likes
6
Points
135
N

Njaare

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2010
1,080 6 135
Kwani anatofauti gani na panya? Kwanza ni hesima kubwa kuwa panya kuliko kuwa CCM. Inahitaji use na akili ya misukule kuweza kuendelea kuishabikia CCM.
Ni kweli kabisa kwani hata kuwaza tu kuwa CCM itakaa ifanye jambo la maana inabidi uwe na akili ya ushetanishetani!
 
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined
Jan 6, 2012
Messages
2,619
Likes
310
Points
180
Tumaini Makene

Tumaini Makene

Verified Member
Joined Jan 6, 2012
2,619 310 180
Mkuu Tumaini Makene ;sina uhakika kama huyu ndugu yetu Ritz anaweza kuelewa neno ulilotumia hapo kwenye bold.Ni bora ungetumia lugha nyepesi.
Nimekusoma Kamanda betlehem.
 
Last edited by a moderator:
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
2,524
Likes
6
Points
135
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
2,524 6 135
Hizi katiba sasa polepole jamanii.
 
zumbemkuu

zumbemkuu

JF Bronze Member
Joined
Sep 11, 2010
Messages
9,458
Likes
1,371
Points
280
zumbemkuu

zumbemkuu

JF Bronze Member
Joined Sep 11, 2010
9,458 1,371 280
Source Tanzania Daima, teh teh teh...

Chadema wanamtega Pinda kwa mtego gani wa panya.
ikiwa tatizo ni source, toa habari ya uongo kwenye hiyo taarifa.
aisee mtu ukiwa na akili za kiliberali ni tatizo sana.
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
57,912
Likes
54,814
Points
280
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
57,912 54,814 280
Mtakaa kutega watu mpaka lini,mkuu molemo hizi siasa za kutegana hizi mpaka lini sisi tunataka sera na hoja wala siyo mitego ya kutega watu mmetega watu wengi sana mbona matokeo chanya hatuyaoni? Tumechoka na mitego mkuu.
Wewe Msukuma ndiyo bure Kabisa , hoja zako ni Dhaifu mno ! Mimi ningekuwa Nape nisingekulipa hata nauli , Achilia mbali hizo buku 7 !
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
57,912
Likes
54,814
Points
280
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
57,912 54,814 280
Hivi kwanini Pinda amekuwa Muongo sana ?
 
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2011
Messages
2,013
Likes
80
Points
145
MNAMBOWA

MNAMBOWA

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2011
2,013 80 145
Mnahangaika na nn mbona mlishasema mnajitoa kuhusu mambo ya katiba? Leo mnawashwa mara mnaunga mkono mara mnamtega pinda yaani hamueleki kbs kama kuku anataka kutaga yai vinza vile.
 

Forum statistics

Threads 1,272,334
Members 489,924
Posts 30,447,889