RAIS SAMIA AZINDUA CHUO CHA VETA MKOA WA KAGERA.
- Ni chuo Cha kisasa kilichogharimu
Shilingi Bilioni 22 ikiwa ni ufadhili kutoka Serikali ya China.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo mezindua chuo Cha ufundi stadi na huduma
VETA Mkoa wa Kagera ambacho Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi
Bilioni 22 ikiwa ni ufadhili kutoka
Serikali ya China.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Rais Samia amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Albert Chalamila, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha
Asilimia 10 ya Fedha za mkopo kwaajili ya Vikundi vya
Vijana kinamama na Wenye ulemavu zinawanufaisha pia
wahitimu wa chuo hicho kwa kuwapatia
fedha taslimu au kuwanunulia Vifaa na kuwatengea maeneo ili waweze kujiajiri.
Aidha
Rais Samia amesema Chuo hicho kina uwezo wa kuchukuwa
wanafunzi 1,400 wa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi ambapo ameahidi kukipatia chuo Shilingi
Bilioni 1 kila mwezi kwaajili ya uendeshaji ili
kupunguza makali ya ada huku akijitolea
kusomesha Vijana 20 ambao familia zao hazina uwezo.
Ili kuhakikisha
kila Wilaya inakuwa na chuo Cha VETA,
Rais Samia amesema Serikali itaendelea kutenga Shilingi
Bilioni 100 Kila mwaka kwaajili ya Ujenzi wa Vyuo hivyo na kuhakikisha
Wilaya zote 62 ambazo hazina chuo Cha VETA zinakuwa na chuo hicho ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa chuo Cha
VETA Mkoa wa Songwe.
Rais Samia amesema lengo Ujenzi wa Vyuo hivyo ni
kuongeza thamani na ujuzi kwa vijana wanaohitimu kuanzia Elimu ya Msingi mpaka chuo wapate ujuzi wa kuwasaidia
kujiajiri wenyewe ili kukabiliana na tatizo la
ukosefu wa ajira ambapo tafiti zinaonyesha
Asilimia 12 ya Vijana hawana Ajira.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania,
Balozi Cheng Mingjian amesema Ujenzi wa chuo hicho ni matokeo chanya ya
ushirikiano baina ya Serikali ya China na Tanzania katika Mambo mbalimbali.
Chuo Cha VETA Mkoa wa Kagera kilichozinduliwa leo kina Madarasa 19 na Karakana 9 ambapo kitaanza kutoa Elimu mwezi January mwakani ambapo miongoni mwa masomo yatakayofundishwa ni Computer, ufundi wa umeme wa majumbani na viwandani, Ufundi Makenika, uchongaji vyuma, uchomeaji na uungaji vyuma, ufundi Bomba, ufundi umeme na mitambo, upakaji rangi, Ujenzi, ufundi seremala.