Rangi ya viti kwa Mkapa imeleta giza uwanjani

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,966
Reaction score
51,107
Mpangilio wa rangi za viti na rangi zenyewe umeleta giza ndani ya uwanja wa Mkapa.

Hata Mpira unapooneshwa na kamera kuelekezwa kwenye maeneo ya vitu visivyo na watu au watu wachache unaona kabisa ule mvuto wa uwanja umepungua kabisa.

Inawezekana lengo la kuweka rangi za bendera yetu ya Taifa uwanjani lilikuwa jema, lakini sidhani mpangilio wake na hizo rangi zenyewe zilifaa kuwepo uwanjani kwa Mkapa.
 
Hiyo ndiyo reflection ya akili za wasomi wa Tanzania.Kama akili zina giza vitu vingi ,miradi mikubwa utaona giza tu.
Nikiangalia Zanzibar naona huko kuna watu wenye akili.
Nikiangalia Rwanda naona wenye akili pia.Tazama tu uwanja wao utajua.
Nikiangalia Kenya naona watu wenye akili,ndio maana ya kusoma haswaa.
Nahisi hapa kwetu kuna matatizo mengi sana maana nikiona hiyo Mkapa eti imetumia bilioni 30 kukarabati,halafu hali yenyewe ndio hiyo,nabaki tu kushangaa hiki kizazi
 
Mkuu umenena vema sana.
Uwanja wetu wa Taifa umepoteza Mvuto wamejaza Viti vyeusi tiiiiiii Uwanja umekuwa giza totoro. Ndio shida ya Kumpa mtu kama KABUDI wizara ya Michezo! Hili ni aibu sana
 
Hiyo ndiyo reflection ya akili za wasomi wa Tanzania.Kama akili zina giza vitu vingi ,miradi mikubwa utaona giza tu.
Nikiangalia Zanzibar naona huko kuna watu wenye akili.
Nikiangalia Rwanda naona wenye akili pia.Tazama tu uwanja wao utajua.
Nikiangalia Kenya naona watu wenye akili,ndio maana ya kusoma haswaa.
Nahisi hapa kwetu kuna matatizo mengi sana maana nikiona hiyo Mkapa eti imetumia bilioni 30 kukarabati,halafu hali yenyewe ndio hiyo,nabaki tu kushangaa hiki kizazi
Ni kweli mkuu ukitaka kujua huko kuna uozo ukimuangalia tu yule mwanasheria wa jamhuri kwenye kesi ya lisu unaona wasomi wetu wanashida.
 
Ukweli ni kuwa nchi hii kuna shida kubwa kuliko tunavyodhani. Kuna ombwe kubwa la kiuongozi na katika wafanya maamuzi. Hatuongozwi tena na taaluma wala weledi wa kazi bali na maamuzi ya kumfurahisha mtu, kuonekana mzalendo (ingawa tafsiri ya uzalendo imechakachuliwa mpaka sasa haina tena sura) au tunafanya "kuonekana tumefanya".

Hiki ndiyo niliwahi kusema kuhusu hizo rangi 》》》》》》

Hawa watu wanaamka na kufanya maamuzi tu ya kutuhadaa ili waonekane wazalendo zaidi.

Uko sahihi kabisa, wamepaka hayo marangi Sheikh Amri Abeid, Arusha na nadhani Dodoma, uwanja haupati muonekano mzuri kwa hayo marangi, hawajashtuka wanaendelea na kosa hilo hilo. Siasa nyingi kuliko weledi.

Naona dalili huu uwanja wa Mkapa unaenda kufa na kupotea kabisa.
 
Back
Top Bottom