Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Usinunue ramani kwa mtu ambaye mkishamalizana tu kwenye malipo, anafuta namba yako jumla (ukimpigia simu baada ya siku mbili, anakuuliza nani mwenzangu). Utaingia gharama tena kutafuta mtu wa kukushauri kwenye ujenzi wakati ulishamuungisha mtu kununua ramani kwake
 
Zege ya lenta ya nyumba ya kawaida kwa kutumia cement za 32.5 inaweza kuwa kwa ratio gani mkuu
 
Ramani, Makadirio, na Ushauri tuwasiliane +255(0)624068809
Mkuu
Kuna apartments zinatakiwa kuezekwa
Sasa Kuna fundi kanishauri ili kuokoa gharama pamoja na ubora niezekee bati ya Alaf nyeupe halafu nipake PVA ya plascon au kiboko...kuliko kuezeka bati nyingine ya rangi

Ushauri wako wa kitalaamu tafadhali
 
Ni sahihi, fundi amekupa ushauri mzuri sana...ALAF wako vizuri kwenye suala la ubora na ndio maana hata miradi ya serikali huwa inatumia bidhaa zake.
 
Katika ujenzi wa kuta, kitaalam inatakiwa usizidishe kozi 6 kwa siku ili kuruhusu kozi za chini zianze kukomaa kabla kozi za juu hazijajengwa juu yake
 
Ili kuepuka madhara ya nyumba kuungua, ni muhimu kuweka kifaa cha kuhisi kupanda kwa joto (fire detector) ama smoke detector ambapo kifaa hicho kitapiga alarm pale kunapokuwa na dalili yoyote ya moto
 
Ili kuepuka madhara ya nyumba kuungua, ni muhimu kuweka kifaa cha kuhisi kupanda kwa joto (fire detector) ama smoke detector ambapo kifaa hicho kitapiga alarm pale kunapokuwa na dalili yoyote ya moto
Hahaha bongo hii hii au unaongelea wapi mkuu, Sasa alarm ikilia moto ushashika mbao za juu alarm inaufanyaje huo moto? Gari la zima moto Dar es salaam hii linafika baada ya nyumba kuwa imeungua. Alarm labda za kutoa taarifa kwa ongezeko la carbon monoxide, za moto kuibiana tu nchi yetu hii.
 
Ni sahihi, fundi amekupa ushauri mzuri sana...ALAF wako vizuri kwenye suala la ubora na ndio maana hata miradi ya serikali huwa inatumia bidhaa zake.
Kwanini unasema ALAF wako vizuri kwa ubora? Ubora tunaangalia nini kwenye bati?
 
Hahaha bongo hii hii au unaongelea wapi mkuu, Sasa alarm ikilia moto ushashika mbao za juu alarm inaufanyaje huo moto? Gari la zima moto Dar es salaam hii linafika baada ya nyumba kuwa imeungua. Alarm labda za kutoa taarifa kwa ongezeko la carbon monoxide, za moto kuibiana tu nchi yetu hii.
Nadhani ingekuwa vizuri ungeuliza mechanism ya hizo detector zinavyofanya kazi, ingekuwa zinatoa alert baada ya moto kutokea hakuna mtu ambaye angeweka hizo detector. Mimi huwa namjibu mtu kulingana na namna alivyouliza, ukijifanya much know kama hivi nakuacha kama ulivyo
 
Katika ufungaji wa taa na feni katika dari, feni ikiwa chini ya taa chumba kinakuwa kinakosa utulivu wa mwanga. Feni inapokuwa inazunguka, vivuli cha mapanga ya feni vinakuwa vinatembea tembea. Unaweza ukaona ni jambo la kawaida lakini kwa wengine hiyo hali inaweza ikapelekea hata kichwa kuuma

Kama utaweka hizo taa za dari kama urembo, basi weka hata taa moja ukutani ambayo itakuwa chini ya feni ili kuua/kufuta hivyo vivuli na kufanya kuwe na utulivu wa mwanga katika vyumba

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane +255(0)624068809

Huduma ya kutembelea site na kupatiwa ushauri kulingana na hali ya eneo lako, udongo, ukubwa wa kiwanja n.k pia inapatikana
 
Wakati mwingine sio lazima sana kuchukua vifaa vyote vya ujenzi vikiwa ktk hali yake ya uzima mfano unapoenda kununua tiles, unanunua box za tiles ambazo ni nzima na ukifika site tiles zingine unazikata ili upate vipande vya kujazia na wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa

Hii pia unaweza ukaapply kwenye gympsum board ktk uwekaji wa dari, tofali n.k kwa lengo la lengo kupunguza gharama

Kabla ya kufanya uamuzi inabidi ufanye mahesabu ili upate makisio kwamba nyumba yako itahitaji vitu vizima vingapi, ili uweze kujua sehemu iliyobaki itahitaji kiasi gani cha material ambazo sio nzima (hapa simaanishi ubovu, namaanisha utimilifu)
Kwahiyo kuna watu wanauza vipande vya tiles vipya?
 
Kwahiyo kuna watu wanauza vipande vya tiles vipya?
Hapana, tiles zinakuwa mpya isipokuwa zinakuwa zimevunjika kwenye angle kutokana na usafirishaji, upakiaji na ushushaji kwa hivyo muuzaji hawezi kuuza kwa bei ile ile ya tiles nzima

Panapohitajika vipande, usikate tiles ambazo ni nzima...tumia hizo ambazo umenunua zikiwa zimemeguka angle
 
NIMEKWAMA NAUZA ENEO LANGU KIBAHA KWA MFIPA.

LIKO SEHEMU NZURI HUDUMA MUHIMU ZIPO.
NGUZO MBILI ZA UMEME MPAKA SAITI.
MCHANGA UKO HAPO HAPO
TOFARI MAPAKA SITE TSH. 750
MAJI YAPO JIRANI TUPO KWENYE MCHAKATO WA KUYAINGIZA
KUTOKA MAIN ROAD KM. 1.5

Square mita 300
Bado sijapata mteja sahihi.
NATAKA MIL. 1.5

0685223804
 
Hivi dhumuni la kuweka nguzo kila kona ya nyumba ni nini? nyumba za kawaida
Mzigo unaobebwa na mkanda huwa unatawanywa sawa sawa kutokea katikati na kuupeleka pembeni, yaani mfano kama mkanda una mita 4 basi uzito uliobebwa na nusu ya huo mkanda (mita 2) unapelekwa kushoto, na uzito wa nusu iliyobaki unapelekwa kulia.

Katika makutano yoyote ya kuta, kunakuwa na mkusanyiko wa uzito kutokea kati kati ya hizo kuta zinazounda hiyo kona kwa hivyo ni muhimu sana kuweka nguzo katika kona ili kuongeza uimara zaidi kwa sababu ndipo mahali ambapo mzigo mkubwa unapokelewa ili kuupeleka ardhini (japo wakati mwingine mkusanyiko huo wa uzito unaweza ukabebwa na tofali tu bila shida yoyote lakini ukiweka nguzo inakuwa imara zaidi)
 
inasaidiaje nyufa kwa maeneo yenye ardhi ya kupasuka (ardhi inachanika chanika kipindi cha jua)
 
Back
Top Bottom