RAMA DEE: BEST ARTIST UNDERRATED

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
21,033
64,842
Jamani kiukweli huyu kaka mkubwa namuelewa sana.
Ana kipaji kikubwa sana. Ni mtunzi na muimbaji mzuri sana, vitu ambavyo wasanii wetu wengi hawanavyo. Labda inaweza ikawa ni mimi tu nionaye hiki kitu, lakini nyimbo za Rama huwa hazichuji na zinazama hadi kwenye mtima na kukufanya ufikiri sana.

Lakini kinachonitatiza ni kwanini Rama Dee hapai sana kama hawa wasanii wetu wengine?
Je, Watanzania hatupendelei sana aina yake ya muziki anaofanya?
Je, Vyombo vya habari havimpigi Promo (Chapeo) huyu msanii?
Au, kuimba kwa kiswahili ni lazima mtu ucheze ili wasikilizaji (Hadhira) wa nchi nyingine wazipende kama wafanyavyo wakina Diamond Platnumz, Ali Kiba na wengineo?

Lakini kwa hili la tatu mbona wakina Khadija Nin, Salif Keita, Lokua Kanza, Fela Kuti, Habib Koite, Yoossou N'dour na wengine wanaimba bila hata kucheza sana lakini wameuza sana nyimbo na wanapiga Concert kubwa kimataifa na wanapata sana pesa. Wengi kati ya hawa ni matajiri wakubwa.

Kiukweli kuna wasanaii wana vipaji vikubwa sana hapa Tanzania lakini wanapotea sana na mpaka sasa wamefifia. Mfano mzuri tu ni Q-Chillah, Steve RnB, Barnaba, Enika, Banana Zorro, Maunda Zorro na wengine wengi tu.
Hili linanipa sana shida mimi binafsi kwasababu kuna nchi kama Nigeria na South Africa wasanii wanatoka sana kama wanakipaji cha kuimba, lakini hapa kwetu sijuin kwanini wasanii hawafiki mbali.

Naomba tusaidiane ile nielewe.
Nawasilisha.
 
Sure..Rama Dee anajua sana..Nadhani kitendo cha yeye kukaa sana nje ya tz kinachangia kumrudisha nyuma..Na sidhani kama anauchukulia muziki serious kihivyo..Pia huyu naye alikuwa ni member wa vinega, so baadhi ya wadau kwenye soko la muziki bongo hawaivi...Uenda hicho nacho kinachangia
 
Hivi huyu naye alikuwa na wale majamaa waliofanya Anti Virus?
 
Duuh, basi hii nayo ni moja ya sababu.
Clouds walikuwa na tabia ya kutopiga baadhi ya ngoma za mahasimu wao.
Hadi leo sidhani kama ngoma zake zinachezwa clouds..Na unajua wasanii wengi wa kibongo walivyo waoga..Ukiwa na bifu na clouds hata wao wanakuwa wanajifikiria mara mbili kukupa support
 
Hadi leo sidhani kama ngoma zake zinachezwa clouds..Na unajua wasanii wengi wa kibongo walivyo waoga..Ukiwa na bifu na clouds hata wao wanakuwa wanajifikiria mara mbili kukupa support

Wanazingua sana.
Wanasahau kama mziki ni biashara.
 
Back
Top Bottom