MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,783
Wazungu husema hivi "Once is an accident, twice is a coincidence and thrice is a pattern
Ule ukanda wa Afrika Magharibi wana kitu cha ziada ambacho nadhani hakionekani lakini kipo tu. Ukifuatilia historia utatambua kwamba watu wenye asili ya ukanda ule ndiyo wanaotawala sehemu kubwa ya tasnia ya burudani hapa duniani, hasahasa muziki. Historia inatuambia wao ndiyo hupeperusha bendera ya muziki wa Afrika tokea vizazi.
Wasanii wakubwa duniani kama Fela Kuti, Youssou N'Dour, Mory Kante, Angelique Kidjo, Salif Keita, Baaba Maal ambao wana mchango mkubwa kwenye muziki Afrika na duniani kote wametokea ule ukanda. Lakini zaidi ya haya, yapo ambayo yananishangaza zaidi. Mosi, baada ya kizazi cha wakina Fela Kuti kuondoka kimezaliwa kizazi kingine kipya ambacho kinaendelea kupeperusha bendera kwa nguvu sana kuliko kile cha kwanza.
Pili, wamegundua vifaa vingi vya muziki ambavyo vinatumiwa sana duniani mfano Akoting limegunduliwa Senegal, Balafon inatumika sana Ghana, Udu limegunduliwa Nigeria, Alagaita imegunduliwa Nigeria, Ngoma ya Djembe imegunduliwa kule Burkina Faso, hata Shekere nazo zimegunduliwa ule ukanda. Kiufupi ukifuatilia sana dhana nyingi za muziki za wabantu zimeanzia kule Afrika Magharibi.
Tatu, hata wale ndugu zao wa karibu ambao waliuzwa utumwani barani Marekani wamekuwa ni ndiyo vinara wakubwa kwenye tasnia nzima ya burudani na michezo. Kama unafuatilia muziki vizuri utatambua kwamba wamarekani weusi wamegundua na kuchangia vipengele (Genres) nyingi za muziki ambazo tunazikiliza leo hii. Muziki wa Jazz (Jazz Music) ndiyo ulizaa Blues, Soul, Rock and Roll, pamoja na Pop ambazo tunazipenda leo. Utafiti wa kisayansi (DNA/ Ancestry Tracing) unasema kwamba wale wasanii wametokea ule ukanda.
Nawapenda sana wasanii wetu kutoka huu ukanda, lakini kila nikifuatilia muziki wao kwa ukaribu halafu nikalinganisha na kile wenzetu wanatengeneza huwa nabaki nawaza sana. Ushawishi wa ukanda wa Magharibi umekuwa mkubwa sana kwenye muziki wa Afrika Mashariki hadi kupelekea sisi kuwaiga wao bila hata kufahamu kwamba tunawaiga, Kuanzia kwenye midundo hadi aina ya uimbaji.
Jambo kubwa ambalo mimi nimefanikiwa kulitambua kidogo ni kwamba sanaa hasa muziki na burudani nyingine ni sehemu za utamaduni wa kila jamii. Hivyo jamii yoyote ambayo hupenda sana utamaduni wake huweza kuwa na muziki wake na hata hufanikiwa sana kuusambaza. Kabla ya mkoloni muziki ulitumika kama sehemu ya ibada, sehemu ya masimulizi na sehemu ya burudani: Hata sasa iko hivi japo muziki ambao huwa tunatumia ni ule wa Magharibi na Mashariki ya Kati.
Baada ya mkoloni kuondoka ni jamii chache za kiafrika zilifanikiwa kutunza yale ya kale na zimekuwa na kitu cha kuionesha dunia ambacho dunia haina. Hivyo dunia ya leo imekuwa tayari kusikiliza na kujifunza kwasababu ni kitu kipya ambacho kimebeba taswira yote ya jamii fulani ambayo ilitengwa hapo mwanzo wakati dunia inaendeshwa na mtu mweupe. Leo hata umsikilize mtu kama Burna Boy au Sarkodie ambao mmoja huimba Afro-Pop na mwingine huimba Hip-Hop lazima utayasikia mahadhi ya muziki wa Afrika Magharibi.
Sisi tulikuwa ni Bakurutu na Taarab ambayo binafsi naamini ilibebe taswira nzima ya utamaduni wetu na ingeendelea kubeba mpaka leo hii kwasababu muziki hukua (Evolves), lakini sijui nini kilitokea hapa katikati muziki ule ukafa. Ukifuatilia wasanii wengi wa Tanzania waliofahamika huko duniani hata kabla ya Diamond Platnumz walikuwa ni wazee wetu wa Bakurutu. Taarab nayo japo wengi tuliikebhei ilikuwa na aina ya uimbaji ambao ulikuwa unaendana na Soprano (Msanii wetu Zuchu ana aina hii ya uimbaji na kama angepata waalimu wazuri angefanya makubwa sana sanaaa)
Leo hii tuko Amapiano, tuko Sebene, tuko Nigeria na hatuna muziki wetu kabisa ambao unatutambulisha. Mimi binafsi napenda kila aina muziki mradi tu uone aina ya utaalamu (Sophistication) na ubunifu (creativity) hivyo sipingi uimbaji wa Amapiano, Sebene au Western AfricaAfro-Pop. Lakini ukweli ni kwamba Tanzania ina wasanii wachache sana ambao wanaweza kutoa nyimbo leo ambayo itakuwa kusikilizwa na vizazi vijavyo na kuwafundisha kitu, au hata kutengeneza muziki ambao unaweza kusikilizwa na jamii nyingine duniani na kujifunza kitu.
Leo hii nikiwasikiliza wakina Asa, Burna Boy, Cobhams Asuquo, Omah Lay, Timi Dakollo, Becca Africa, Sarkodie, nabaki nasema Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Baghosha. Inabidi tukaze buti na kufanya jitihada za ziada kukuza muziki wetu, tusiishie kulalamika kwamba ni lini wasanii wetu watatambulika vizuri dunia na kuchukua tuzo kubwa na za heshima kama Grammy.