Burna Boy ni uso mpya wa muziki wa Afrika ? Bongo Fleva igeni mfano

Gibborim

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
388
877
Huyu jamaa nimekuwa nikimfuatilia kwa muda kidogo nione mwelekeo wake kimuziki. Kila siku anazidi kuimarika na kuwa fundi. Kiufupi Burna Boy anafanya kitu ambacho wasanii wachache wa Afrika wameweza kukifanya, kuchanganya mahadhi ya muziki wa kale wa Afrika na muziki wa kizazi kipya wa Afrika.

Miaka ya 60, 70, 80 hadi 90 mwanzoni muziki wa barani Afrika ulitawaliwa na wasanii ambao waliuvaa vizuri uhusika wa Afrika katika sanaa yao ya muziki na walitengeneza muziki uliokuwa wa aina yake ambao ni mtaalamu tu angeweza kuutengeneza. Muziki huu ulifika sehemu nyingi za dunia na kujijengea umaarufu wa aina yake.

Wasanii kama Fela Kuti, Angelique Kidjo, Remy Ongala, Miriam Makeba, Black Mambazo (Lady Smith), Salif Keita, Youssou N'Dour, Khadija Nin na wengine walitengeneza muziki wa aina yake ambao ulikuwa ni wa kipekee kuanzia kwenye sauti (Vocals), vifaa (instruments), uchezaji, mavazi na mpangilio wa bendi zao ulikuwa umejaa ubunifu ambao ulibebe Afrika na kufanya muziki huo ufike mbali.

Hapa katikati kuanzia 90 katikati muziki wa Afrika ulianza kupoteza mwelekeo wake baada ya wasanii, lebo na vyombo vya habari kuanza kuingiza baadhi ya mambo ya nje kwenye sanaa ya Afrika. Yakawa ni mambo ya midundo tu bila kuwa na kitu chochote cha ziada. Muziki unabamba leo tu lakini kesho unachuja.

Wasanii wa kizazi kipya Afrika walioweza kudumisha muziki wa Afrika angalau ni wale ndugu zetu wa Kongo lakini nao siku hizi wanaanza kuzingua. Wanakuwa na maneno mengi tu bila kitu cha maana.

Burna Boy amekuja na akili ya tofauti kidogo, ambapo ameweza kutumia mahadhi ya kipekee ya muziki wa kale wa Afrika huku akiwa msanii wa kizazi kipya. Walimu wake wakubwa ni kama Femi Kuti na Angelique Kidjo. Sasa anapopasua anga watu walioanza kusikiliza muziki hivi karibuni hawaelewi kwanini Burna Boy anafanikiwa sana. Wanasema anabebwa, lakini watu ambao wanafahamu muziki wakimsikiliza Burna Boy wanaona utofauti.

Katika historia ya muziki wa dunia, wasanii wa Afrika waliowahi kuchukua tuzo kubwa za muziki au kufanya matamasha makubwa duniani ni wale ambao wameleta kitu kipya kwenye tasnia ya muziki. Lakini siyo kuimba RnB, HipHop, Soul, Jazz, Raggae au Blues. Wenzetu wa nje hii miziki wanaisikia kila siku hivyo sisi hatuwezi kupeleka kitu kipya kwao.

Tukisingizia kwamba kila zama na nabii wake nadhani tutakuwa hatuyaangalii mambo katika taswira pana. Maana huko Ulaya kuna miziki ya zamani The Classics kama ya wakina Mozart lakini leo bado inabamba tu. Au Opera Music mpaka leo bado ni hatari sana, mziki wa msanii kama Luciano Pavarotti huwa hauchuji.

Wamarekani weusi walifanikiwa sana kwasababu walileta kitu kipya kwenye tasnia ya muziki ambacho mchango wake utadumu vizazi hadi vizazi. Walileta Jazz, Soul, HipHop, Blues, Raggae na RnB ambazo ndiyo utambulisho wao mpaka leo hii.

Burna Boy ndiko anaelekea huku kama ataendelea hivi. Nadhani wasanii wetu wa Bongo Fleva wana kitu kikubwacha kujifunza kutoka kwa Burna Boy...
 
Wakina king monada ndo wanaimba miziki yenye ladha ya kiafrika na wanadunda.....kiufupi hakuna nchi inayoifikia south Africa kwa aina ya muziki unayoiongelea.
 
Khadija Nin natamani radha ya mziki wake urudi, Napenda nyimbo zake kama ;
- Sina Mali,Sina Deni
- Wale watu
- Samborela
- Mama
Natamani tena kusikia mziki kama huu, wenye vionjo vya kiafrika na magharibi
 
Khadija Nin natamani radha ya mziki wake urudi, Napenda nyimbo zake kama ;
- Sina Mali,Sina Deni
- Wale watu
- Samborela
- Mama
Natamani tena kusikia mziki kama huu, wenye vionjo vya kiafrika na magharibi
Miziki kama ile ni wasanii wachache sana wa kizazi hiki wanaweza kuitengeneza.
 
Khadija Nin natamani radha ya mziki wake urudi, Napenda nyimbo zake kama ;
- Sina Mali,Sina Deni
- Wale watu
- Samborela
- Mama
Natamani tena kusikia mziki kama huu, wenye vionjo vya kiafrika na magharibi






Hawa wameweza.
 
Back
Top Bottom