Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Moja ya kitu ambacho kulikuwa cha kushangaza ni pale katika awamu iliyopita viongozi kutoa sifa kwa Rais ambazo zilipitiliza. Hii imekuwa tabia ya muda mrefu sana Rais kusifiwa kupitiliza na watendaji wake.
Bahati mbaya kabisa maraisi huridhia na kukubaliana na hizo sifa, lakini ukweli ni kuwa wanaosifia hawamaanishi. Watu wanasifia kwa lengo la kuwa karibu na Rais na kulinda nafasi zao.
Wameanza tena kwa speed kubwa awamu hii ya mama Samia, wanasifia kuliko kawaida. Walianza kuweka mabango makubwa barabarani ya kumsifia Rais Samia.
Leo kwenye kilele Cha wiki ya UWT wameamua kushona suti na kuandika jina la Samia. Haya yanafanywa na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wengine. Sina shaka na hizo sifa, ila nina swali tu Je, Mama Samia amekubaliana nazo?