Raisi Samia hizi sifa umekubaliana nazo?

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Moja ya kitu ambacho kulikuwa cha kushangaza ni pale katika awamu iliyopita viongozi kutoa sifa kwa Rais ambazo zilipitiliza. Hii imekuwa tabia ya muda mrefu sana Rais kusifiwa kupitiliza na watendaji wake.

Bahati mbaya kabisa maraisi huridhia na kukubaliana na hizo sifa, lakini ukweli ni kuwa wanaosifia hawamaanishi. Watu wanasifia kwa lengo la kuwa karibu na Rais na kulinda nafasi zao.

Wameanza tena kwa speed kubwa awamu hii ya mama Samia, wanasifia kuliko kawaida. Walianza kuweka mabango makubwa barabarani ya kumsifia Rais Samia.

Leo kwenye kilele Cha wiki ya UWT wameamua kushona suti na kuandika jina la Samia. Haya yanafanywa na Wakuu wa Mikoa na Wakuu wengine. Sina shaka na hizo sifa, ila nina swali tu Je, Mama Samia amekubaliana nazo?

Screenshot_20211023-100909_1.jpg


20211023_101359.jpg
 
Hizi sifa inawezekan hazimkuti/kumfikia Mh.
Acha uongo, Leo kwenye hiko kilele Cha UWT mgeni rasmi ni yeye mama Samia. Ina maana hao wakuu wa mikoa waliovaa hizo suti hawaoni?
 
Musiba aliwahi KUMSIFIA MWENDAZAKE kuwa "Mambo anayoyafanya hata YESU HAKUWAHI KUYAFANYA"Msifiwa licha ya kuwa ni Mkristo alikaa kimya
Maendeleo nchi hii tusahau. Kama technocrats wetu asubuhi mpaka jioni wanawaza maneno mazuri ya kusifia na kumfurahisha kiongozi, sijui ni muda gani wanatumia kufanya kazi za kibunifu za kuwasaidia wananchi
 
Maendeleo nchi hii tusahau. Kama technocrats wetu asubuhi mpaka jioni wanawaza maneno mazuri ya kusifia na kumfurahisha kiongozi, sijui ni muda gani wanatumia kufanya kazi za kibunifu za kuwasaidia wananchi
Hapo ndio uone kuwa hawa watu Kama wanaweza kumshauri raisi
 
Wameanza tena kwa speed kubwa awamu hii ya mama Samia, wanasifia kuliko kawaida. Walianza kuweka mabango makubwa barabarani ya kumsifia mama Samia.

Leo kwenye kilele Cha wiki ya UWT wameamua kushona suti na kuandika jina la Samia.

FURSA FURSANA
 
miongoni mwa watu hatari katika maisha yetu ni wanaotusifia sana bila kutukosoa, funzo tumelipata kwa mwenda zake, hao hao walomsifia sana leo karibu 3/4 wamemgeuka
 
Back
Top Bottom