Rais wetu JK, this is too much !

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Nimejisikia huzuni sana baada ya kuikuta picha ya Rais Kikwete ktk gazeti la Mwananchi uk.3. Ktk picha hiyo, Rais Kikwete akiwa na Ofisa wa NBC, anaonyesha kadi yake mpya ya NBC Debit Master Card.

Sioni sababu ya Rais kutumiwa kibiashara na NBC. Hivi kesho NBC wakianza kuitumia picha hiyo kwenye promo zao itakuwaje? Nasema hivyo kwa sababu niliingia Guest fulani huko Geita nikakuta picha imebandikwa receiption Rais Mkapa akiwa na mwenye hiyo guest na familia yake. Tunadhibitije picha ikitumik isivyo?
 
Cha ajabu kipi? Mbona Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ana promote kilimanjaro(mlima bana!) uwepo kati ya maajabu saba asilia ya dunia.Nakumbuka pia aliyekuwa Rais wa zambia Kenneth Kuanda amewahi promote utumiaji wa neti.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akionyesha kadi yake mpya ya
NBC Debit Master Card mara baada ya kukabidhiwa na maofisa wa Benki ya
NBC Ikulu, Dar es Salaam hivi karibuni. Kadi ya NBC Debit Master Card
ilizinduliwa na benki hiyo Oktoba 18 mwaka huu. Kutoka kushoto ni,
Meneja wa Tawi la Corporate Bi. Jacqueline Sindano Mkuu wa Shughuli za
Kibenki wa NBC, William Kallaghe na Mwakilishi wa Mauzo, Emmanuel
Mseti.

Ris Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akijaza fomu ili kupata kadi
mpya ya Debit Master Card ya Benki ya NBC Ikulu, Dar es Salaam hivi
karibuni. Kadi ya NBC Debit Master Card ilizinduliwa na benki hiyo
Oktoba 18 mwaka huu. Wanaomsaidia Rais kutoka kushoto ni, Meneja Tawi
la Corporate Bi. Jacqueline Sindano, Mkuu wa Shughuli za Kibenki,
William Kallaghe na Mwakilishi wa Mauzo, Emmanuel Mseti.

Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mkuu wa Shughuli za Kibenki wa
NBC, William Kallaghe na baadhi ya maofisa wa benki hiyo waliokwenda
Ikulu, Dar es Salaam hivi karibuni ambako walimkabidhi kadi mpya ya
NBC Debit Master Card. Kushoto ni Mwakilishi wa Mauzo, Emmanuel Mseti
na Meneja wa Tawi la Corporate, Jacqueline Sindano
 
Anahamasisha wananchi watumie card . Wakati wa kutembea na kitita cha noti kimepitwa na wakati.
 
huyu mkulu wa bongoi tumeshamzoea, huyu ni sharobaro men! Anatumia debit master card men! U know what i'm saying men? ana swagga men!,muuza sura men! Kapiga picha na 50 cent men! Yuko bllingling men! Oooooooh mamaaaa! Bado unashangaa? Oooh ny Gad!
 
Yale ya kwenye orijino komedi ndo hayo,picha ya rais dili,hiyo guest huwezi nkukuta wanabanwa kulipa kodi,na hata kama kuna vya chini ya zulia hakuna wa kunusa,wanajua mwenye mali anajuana na mkapa,the same to jk

Nimejisikia huzuni sana baada ya kuikuta picha ya Rais Kikwete ktk gazeti la Mwananchi uk.3. Ktk picha hiyo, Rais Kikwete akiwa na Ofisa wa NBC, anaonyesha kadi yake mpya ya NBC Debit Master Card.

Sioni sababu ya Rais kutumiwa kibiashara na NBC. Hivi kesho NBC wakianza kuitumia picha hiyo kwenye promo zao itakuwaje? Nasema hivyo kwa sababu niliingia Guest fulani huko Geita nikakuta picha imebandikwa receiption Rais Mkapa akiwa na mwenye hiyo guest na familia yake. Tunadhibitije picha ikitumik isivyo?
 
Nimejisikia huzuni sana baada ya kuikuta picha ya Rais Kikwete ktk gazeti la Mwananchi uk.3. Ktk picha hiyo, Rais Kikwete akiwa na Ofisa wa NBC, anaonyesha kadi yake mpya ya NBC Debit Master Card.

Sioni sababu ya Rais kutumiwa kibiashara na NBC. Hivi kesho NBC wakianza kuitumia picha hiyo kwenye promo zao itakuwaje? Nasema hivyo kwa sababu niliingia Guest fulani huko Geita nikakuta picha imebandikwa receiption Rais Mkapa akiwa na mwenye hiyo guest na familia yake. Tunadhibitije picha ikitumik isivyo?

Hiyo Gest inaitwaje?
 
Katika hadhi ya Urais, mtu anahitajika kuwa na kadi ya namna hiyo? Anaitmua wapi na wakti gani? Mimi nadhani kila kitu kinafanywa na wasaidizi wake.
 
of coz is a logical here unachoongea ni kweli lakin pia hakina maana
 
Acha ujinga Rais anahaki yakuunga mkono kila kitu cha maendeleo. Kama Rais NBC TUNAMJALI NAKUMPENDA. Acha wivu.
 
huyu mkulu wa bongoi tumeshamzoea, huyu ni sharobaro men! Anatumia debit master card men! U know what i'm saying men? ana swagga men!,muuza sura men! Kapiga picha na 50 cent men! Yuko bllingling men! Oooooooh mamaaaa! Bado unashangaa? Oooh ny Gad!
wewe utakuwa ni msanii wa bongo flava
 
Anahamasisha wananchi watumie card . Wakati wa kutembea na kitita cha noti kimepitwa na wakati.

Mkuu, yawezekana unachosema kina ukweli na mantiki kidogo, lakini je, hakuna wengine wa kufanya kazi hiyo? Benki zingine zitakapozindua huduma kama hiyo nazo ziende ikulu? Atakataa kuzipokea? Lakini wakati mwingine wasaidizi wake ndio hasa wa kulaumiwa kwa ushauri mbaya.
Kwa sababu, wanaotaka kumwona Mhe. Rais hawaendi kwake moja kwa moja. Lazima wawaone wasaidizi wake na kueleza sababu ya kutaka kumwona. Nadhani wao ndio wanaomshauri vibaya na kuonekana akifanya vitu kama hivyo.
 
Cha ajabu kipi? Mbona Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ana promote kilimanjaro(mlima bana!) uwepo kati ya maajabu saba asilia ya dunia.Nakumbuka pia aliyekuwa Rais wa zambia Kenneth Kuanda amewahi promote utumiaji wa neti.

acha ushambaa wewe mtofautishe kikwete na mwinyi afu kisha tofautisha mlima kilimanjaro na NBC..fikiria kabla ya kukomenti kama uwezo wa kufikiria huna nenda fesibuku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom