Rais wangu Magufuli, mimi sio mnafiki

goshaiwedi

Member
Feb 23, 2020
60
76
Naendelea, umezungumza kirefu sana, na nimekufuatilia sana, unapenda kuzungumza na wananchi wako, ila mheshimiwa msema kweli ni mpenzi wa mungu, hotuba zako nyingi zimekuwa kama mipasho, yaani unalaumu mwanzo mwisho, kwa mfano kuhusu mwanao aliyepona corona kwa kujifukiza, maudhui yako yamesimama kuwapinga wataalamu wako uliowateuwa mwenyewe kuwa wameshindwa kufahamu kuwa malimao yanatibu COVID 19 lkn wewe umejua,

Hapo maana yake umewabeza wataalamu wetu, mfano mwingine, rafiki yako aliyepimwa MUHIMBILI na kuonekana ana covid lkn alipoenda (sipakumbuki) akakutwa hana, maana yake ulikuwa unawananga maproo wa MUHIMBILI kuwa hawana uwezo ama ni wazembe, mh rais wapo watakaoisifia hotuba yako lkn tambua ndio wale wale waliokusifia ulipobaini mapapai yana covid, lakini hawajiulizi mbona tume iliyoundwa iko kimya?,

Maana yake hakukuwa na ukweli, hivyo mh rais jaribu kuhutubia kwa upole bila hasira wala kuwa mtu wa kulaumu taasisi zako, nilitegemea sehemu ya hotuba yako ingelaumu wapinzani lkn naona sehemu kubwa umekuwa unalalamikia wataalamu wako kama vile wanapatikana kwa kura, mh unawakatisha tamaa, badilika, tangu uhamie Chato huwezi hutubia wananchi bila ama kutumbua ama kuteua, kuna msemo alisema JENERAL ULIMWENGU, ukiona unaowaongoza hawaelewi kile unachoma basi tambua ama hawajui ama wewe hueleweki, kubadili balbu kila siku si dawa, pengine holder ndio mbovu, ni hayo tu mh samahani ikiwa ntakukwaza

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Kama ulimskiliza vizuri ile speech aliokua anelezea mapapi alisema labda hawapo professional, ama vifaa ni vibovu ama blabla zingine, uwe unaskiliza kuelewa sio unaskiliza kupost
 
Back
Top Bottom