johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,947
- 141,925
Rais wa Zambia aliyechaguliwa hivi karibuni na kuapishwa juzikati kwa mbwembwe na vigelegele amedai ameikuta Hazina ya nchi nyeupe yaani haina fedha.
===
Rais mpya wa Zambia ameambia BBC kwamba amerithi hazina "tupu", wakati " kiasi cha kutisha" cha pesa kikiibwa.
"Watu bado wanajaribu kuhamisha fedha hata dakika hizi za mwisho hatua ambayo hairuhusiwi kwani pesa hizo sio zao," Rais Hakainde Hichilema alisema.
Alimshinda mpinzani wake Edgar Lungu katika uchaguzi wa urais mwezi uliopita.
Bwana Hichilema hakutaja maafisa wowote. Bwana Lungu hapo awali alikanusha makosa yote.
BBC imetka tamko kutoka kwa chama chake. Bwana Lungu aliliongoza taifa hilo lenye utajiri wa shaba tangu 2015. Alisifiwa sana kwa mabadiliko mazuri ya madaraka kwenda kwa Bwana Hichilema, ambaye alishinda urais baada ya majaribio matano bila kufaulu
Deni kamili ‘halijafichuliwa’
Bwana Hichilema alishinda uchaguzi huo kwa ahadi ya kukabiliana na ufisadi, na kumaliza mgogoro wa kiuchumi ambao umesababisha deni la Zambia kuongzeka .
Katika mahojiano na BBC, rais mpya alielezea hazina hiyo kuwa "tupu kabisa".
Aliongeza kuwa "shimo ni kubwa zaidi kuliko tulivyotarajia" na hali ya deni ilikuwa "haijafichuliwa kabisa" na serikali ya zamani.
"Kuna uharibifu mwingi, kwa bahati mbaya," Bwana Hichilema alisema.
Aliongeza kuwa serikali yake "haitovumilia kabisa" ufisadi, na itachunguza alichokiita harakati zinazokiuka sheria za kuhamisha fedha .
"Sitaki kusema mengi ... tunachokichukua ni cha kutisha," rais alisema.
"Utahisi hakuna mtu anayeweza kufanya kitu kama hicho lakini inafanyika. Watu wamefanya hivyo. Bado wanajaribu kufanya hata sasa."
Bwana Hichilema ameteua mchumi na mshauri wa zamani wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Situmbeko Musokotwane kama waziri wa fedha.
"Iiwapo hatutafanya chochote kwa bajeti, basi bajeti itakuwa hasa kwa ajili ya kulipa mishahara na pia kulipia madeni," Bw Musokotwane alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema mara tu baada ya kuteuliwa.
Zambia inadaiwa wastani wa $ 12bn (£ 8.6bn), ripoti za awali zilisema.
Inatumia angalau 30% ya mapato yake kwa malipo ya riba, kulingana na kampuni ya viwango vya mkopo S&P Global.
Mwaka jana, Zambia ilikosa ulipaji wa riba, na kuifanya kuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kukosa kulipa mkopo wakati wa janga la Corona .
Pia inakabiliwa na ugumu wa kulipa mikopo mingine
Chanzo: BBC