Rais wa zamani wa DRC atua Goma

Rais wa zamani wa DRC atua Goma

Je ni sahihi kutumia Siasa Kwa Maslahi Binafsi na kuacha nyuma maslahi ya Nchi na Wananchi wote kiujumla?

Je anachokifanya Kabila kuungana na Waasi (ambao kimsingi waliokuwa maadui zake kipindi akiwa Rais) Kuna Manufaa Kwa Congo na Ukanda wa Africa Mashariki na Kati kiujumla?
Kwanza kabisa, niambie nchi ya Kiafrica, ukiondoa Burkina Faso, leo hii ina uongozi wa kizalendo? Haipo. Zote kimasrahi zaidi. Kiongozi anaeangalia maslahi ya wananchi ni nani? Wachache mno, na bado ya wao kuondoa vyao.

Kabila bado binadamu, na mpaka sasa, nchiini kwake ni kama raia wa kawaida. Vyeo vyote alishavuliwa.

Kabila, ni miongoni mwa matajiri. Kwa experience yake ya jeshi, uongozi na siasa, bado ni msaada mkubwa kwa sababu ya ushawishi wake kitaifa na kimataifa.

Manufaa anayo kwa namna moja ama nyingine, kwa sababu waliowahi kuwa maadui zake, leo hii ndo msaada pekee alio nao wa karibu kuweza kubaki na uraia wake. Na wakiungana, serikali iliyomvua heshima ikaondoka, nani wa kumgusa tena? Ungeuliza tu labda amejiandaaje kuweza kusafisha jina lake kwa matukio ya awali.

Mwisho kabisa, kiti kile cha urais, watu wengi hukifananisha. Rais kama rais hana mamlaka ya kuliendesha taifa kama anavotaka yeye. Nyuma yake kuna kamati yenye nguvu zaidi. Na ndo maana utagundua serikali ya DRC ina makundi mawili, makubwa yenye nguvu.

Taarifa nazoweza kukuhakikishia, ila kwa kukuomba na wewe usubilie ujionee, ni kwamba Moise Katumbi, nae yupo upande wa Kabila na AFC/M23. Bro, hawa watu wana uwezo zaidi ya unavyofikilia.

Inasemekana, mwezi ujao jeshi la AFC/M23 likaanza kupokea mshahara kama majeshi yote. Unategemea kinachoenda kutokea ni nini?
 
Joseph Kabila aliyekuwa Rais wa DRC amezungumza kwa video na akamuita Rais wa sasa wa DRC Dictator. Kabila amezungumza baada ya Bunge la DRC kumuondolea kinga ya kutokushitakiwa. Mamlaka za DRC zinataka kumshitaki kabila kwa makosa ya Uhaini na uhalifu wa kivita akihusishwa na M23.

Serikali ya sasa ina wafuasi wengi wa Kabila, na huku zaidi ya wanajeshi wakuu 20 wapo nyuma ya nondo, kufuatia kinachoitwa usaliti uliopelekea Kivu zote kuangukia mikononi mwa AFC/M23(waasi).
Mimi jamaa huyu nilisha mshitukia siku nyingi, hasa baada ya baba yake wa kufikia kufa kifo cha kutatanisha - Kabila Sr, hakuwa Baba yake wa damu yeye na dada yake walilelewa naye for some reasons that beats me!! Mwisho WA siku ndiyo hivyo TENA!!
 
Back
Top Bottom