Rais wa wanyonge, wanyonge wapi?

Halafu viongozi wetu hata awamu iliyopita wanapenda kutumia maneno ya kusema wananchi 'Masikini, wanyonge, dhaifu, au sisi ni taifa masikini sijui na nini lakini wanashindwa kujua hata kama kuna ukweli lakini wanatuumbia tu hizo hali na sisi tunajiona wanyonge na dhaifu

Kuna maneno mengi tu ya kupeana moyo, ushujaa, kutokukata tamaa na kuonyesha kama kesho yetu ipo nzuri zaidi kama Taifa kila mtu akitimiza wajibu wake

Namtambua mtoa mada hakulenga huku ila nimeona tu hii nayo changamoto ktk hotuba za viongozi wetu kutangaza umasikini na udhaifu wa wananchi hata kama upo sio sawa na badala yake waanze kutujenga ktk kuwa chanya na kesho yetu 'will be better than today'
 
Asante mkuu kwa kuwakilisha,hata Mimi ningependa kujua sifa zinazotumiwa na rais kuwàjua hao watanzania wanyonge ili nàmi nijipime kama nipo kwenye hilo kundi la wanyonge ama laa
 
Okwo ,leo hutaki kuitwa mnyonge? Hujawai kunyongwa ww? Au neno mnyonge ngumu? Kwa kingereza mnyonge means what labda tuanzie apo kuelewa.
 
Watanzania wavumilivu/wajinga/waoga..Ona enya watu wanajua haki zao.Huwezi waita wanyonge wakuache salama
 
Kama wewe ni maskini unategemea uitweje ili usionewe? Uitwe tajiri? Hata Tanzania inaitwa maskini na nchi tajiri akiwemo huyo magufuri,
Sijui kama maskini ni tusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile billion 90 Alisha lipa. Au bombandier ndo ishapigwa mnada
 
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anawapigania wanyonge ili iweje wakati waliofanikiwa anasema hawataki. Nadhani anawapenda wanyonge kama mapenzi yake sio anataka wafanikiwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo mnyonge ikizoeleka Kinachofuata ni mnyongeni
 
utaitwaje mnyonge wewe wakati mlibadilishia gia angani kwa nguvu ya 'rasilimali' ya kukwepe umasikini kibinafsi!!! wewe si mnyonge!!
 
Mheshimiwa Rais wa JMT mara nyingi umesema wewe ni Rais wa wanyonge sasa sijui wanyonge ni wapi?
1.Ni hawa Mamantilie wanaouza chakula walio fukuzwa Stand Kuu ya mabasi ya Mkoa wa Pwani Kibaha mjini wanaotangatanga hawana uhakika hata wa mlo mmoja ??????
2.Ni hawa Babantilie wanao uza chakula USIKU walio fukuzwa Stand Kuu ya mabasi ya Mkoa wa Pwani Kibaha mjini wanaotangatanga hawana uhakika hata wa kutunza mke kwa siku moja na wengi wao sasa wametengana na familia zao zimeludi vijijini hawana uhakika tena wakuwa na ukaribu na familia zao??????
3.Ni hawa wahanga wa Bomoabomoa wa Kimara wanao lala inje huku hawajui kesho yao ?
4.Ni hawa wakulima ulio watangazia Neema ya Viwanda na sasa Mazao hayana pa kwenda juzi nilikuwa Lindi Luangwa nimenunua mbaazi Kilo 100 kwa Shilling 8,000 kilo moja ni sawa na shiling 80????


WALALA HOI WA INCHI HII NI WAPI ???

HALI NI MBAYA SANA TUNAKOELEKEA KAMA TAIFA HUKO MBELE HALI SI SHWALI NATUMAI MUDA MCHACHE VIJANA KWA WAZEE WATAANZA KUZAMIA TUJITAFAKARI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…