Rais wa uswiss akisubiri treni

Rais wa uswiss akisubiri treni

MJIMPYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
506
Reaction score
273
Hapa Mh Rais akisubiri treni bila kuwa na mlinzi yeyote.
Raha kweli!

attachment.php
 
Attachments

  • Untitled.jpg
    Untitled.jpg
    24.9 KB · Views: 2,634
Na ni hapa " Mabilioni a.k.a vijisenti" vya mafisadi wa Bongo yamefichwa...
 
Nyongeza:

1.Anaishi kijijini kama kilomita 20 hivi kutoka Ikulu yake-Bern.
 
Inawezekana anamjua mzee wa vijisent.
 
Rais, halafu anaishi kijijini? Nani anakaa ikulu sasa!

Mkuu, Uswisi wanamfumo wa kipekee sana kiutawala. Kwa nyongeza, usishangae kupishana naye mtaani, Bern, akiwa amepanda baiskeli!
 
Huyo mama mwenye ujauzito ndiye bodyguard wake kama hamjui....
 
Jana mmesikia ya Uhuru Kenyatta, alipotembelea jimbo ambalo ni Ngome ya Raila. Mawe yametupwa High Table alipokaa Uhuru bila woga wananchi wakatoa ya moyoni kwa kichapo.
 
Mkuu, Uswisi wanamfumo wa kipekee sana kiutawala. Kwa nyongeza, usishangae kupishana naye mtaani, Benn, akiwa amepanda baiskeli!
nimeifuatilia hii habari nikafurahi sana. yani huko kuna mahusiano mazuri kati ya watawala na watawaliwa. sehemu nzuri sana ya kuishi hiyo... hapa bongo hata ukikatisha karibu na wizara tu walinzi wanakufokea, hahahahahaaa!!

Twitter Doesn't Know What To Think Of This Pic Of Switzerland's President Alone At The Train Station | Business Insider
The Swiss president's commute goes viral on twitter
https://twitter.com/Twiplomacy/status/507104481335861248
 
Uzuri wa wenzetu viongozi wanawajenga wananchi wao kuwa binadamu ili ambapo matokeo yake hawahofiani wakati sisi watawala wanatujenga tuwe kama wanyama ambapo matokeo yake ni kuhofiana.
Wenzetu wanadai ujira kwa umma kwa kazi wanazozifanya wakati hapa wanaiba mali za wananchi kwa hiyo inabidi kuwaogopa au kuwatisha wasikuulize 'pesa zetu zinafanya nini'!?
 
Daah kumbe hata wanaume wa kiswiz balaa, ona mama wa watu alivyochoka wakati huku kitoto cha kwanza kikiwa bado hata miaka miwili hakijafikisha
 
Pamoja na ukweli kwamba ni nchi ndogo,sawa tu pengine na moja ya mikoa ya Bongo.Lakini uchumi wao imara sana.Watawala wanafanya kazi kwa ajili ya waliowaweka madarakani.Maisha bora kiukweli kwa kila "Mswisi" yamewezekana....
 
Uzuri wa wenzetu viongozi wanawajenga wananchi wao kuwa binadamu ili ambapo matokeo yake hawahofiani wakati sisi watawala wanatujenga tuwe kama wanyama ambapo matokeo yake ni kuhofiana.
Wenzetu wanadai ujira kwa umma kwa kazi wanazozifanya wakati hapa wanaiba mali za wananchi kwa hiyo inabidi kuwaogopa au kuwatisha wasikuulize 'pesa zetu zinafanya nini'!?

absolutely true. huko watu 'wanapanga foleni' kulipa kodi, wanajua inawafanyia nini. angalia hapa kwetu watu wanavyokwepa kodi, k'koo wanafukuzana na TRA kila siku. watu wanaona haina haja ya kulipa kodi kwa sababu pesa haiwafanyii kazi, mafisadi wanazipiga tu (rejea mabilioni yaliyochotwa na wachache). chukulia mfano wa k'koo, watu wanalipa ushuru wa manispaa lakini eneo halifanyiwi usafi, marekebisho, nk. hapo usitegemee kutakuwa na mahusiano mazuri ya watawala-watawaliwa.
 
Daah kumbe hata wanaume wa kiswiz balaa, ona mama wa watu alivyochoka wakati huku kitoto cha kwanza kikiwa bado hata miaka miwili hakijafikisha

Kwao sio tatizo. Serikali itawajibika kwa matunzo ya watoto hao; pia mzazi (wazazi).
Nguvu kazi inaandaliwa mapema ili baadaye ije kulijenga taifa lao. Watakosaje kuwa wazalendo kama serikali inawajibika kwako moja kwa moja kwa namna hiyo...?
 
Hapa sweden kuna uchaguzi mwezi ujao na kuzungka kwangu huko mjini kwenye mji mdogo wa hapa sweden nikakutana na kiongozi mzito tu wa chama tawala akiwa amekaa kwenye cafeteria ya kawaida tu wezake wawili wakiwa kwenye masuala Yao ya campain, hakuna cha ulinzi wala nini, Ingekua hapa bongo basi kwanza hiyo gharama tu ya kuka hapo ingekua ni balaa pammoja na huduma ya hali ya juu, who cares si mali ya uma tu... na Utaona ma gari Aina ya mashangigi hapo nje
 
Back
Top Bottom