Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

mpaka ulipofikia huu uzi ninaamini Frank wanjiru ni malinzi mwenyewe, maana sizani kama angebaki kimya mpaka sasa

Kwahiyo kumbe pale mwanzoni nilipomjibu Mtu hivi mlikuwa hamniamini? Nakubaliana tena nawe kuwa kwa 100% atakuwa ndiyo Yeye mwenyewe Mkuu. Aliamua kulitumia lile jina la mbele la Kikenya ili ' kutuzuga ' Watanzania lakini akasahau kuwa alipoamkia Yeye leo sisi wenzake tulilala majuzi. Kwa ninavyomjua huyu Jamaa akiona tu uzi wa Jamal Malinzi hawezi kuwa kimya na kwa mshangao mkubwa uzi sasa unaenda page ya 13 bado hajaleta ' pua ' yake humu.

Frank Wanjiru tafadhali ukitoka hapo Selander Bridge na TAKUKURU kabla hujaenda kuoga na kutoa ' nuksi ' ya kulala ' Lupango ' njoo huku tafadhali ' tuyajenge ' na ' tuyajadili ' kwani tungependa sana tusikie kutoka upande wako ' horse's mouth ' ili utumalizie ubishi.
 
Nasubiri reaction ya FIFA juu ya hiyo move ya takukuru kuingilia vyama vya hiari!! Sijui nani mshitaki

Hapana mkuu kwenye maswala ya jinai FIFA hawezi sema lolote.

Ye mwenyewe muhanga FBI walivyowakusanya genge la blatter kwenye maswala ya graft mpaka ufalme ukaporomoka
 
Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu Celestine Mwesigwa, walikatamatwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU na leo wanatarajia kufikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kujibu mashtaka juu ya matumizi mabaya ya ofisi.

Msemaji wa Takukuru Tunu Muleli, amesema, wanawashikilia viongozi hao wa juu wa TFF, kwa mambo mbalimbali ambayo hawawezi kuyaweka wazi lakini baada ya kukamilisha wanacho kihitaji watawaeleza wananchi na wapenda mchezo wa soka.

Kwa muda mrefu kumekuwepo na tuhuma mbalimbali dhidi yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Taasisi hiyo ya kitaifa na inasemekana TAKUKURU wamekuwa kwenye uchunguzi kwa muda sasa mpaka jana walipoamua kuwatia nguvuni.

Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.

Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL ulithibitisha Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.

Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaainishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.

Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini.

Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.

Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.

Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.

Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayayi na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza.

Dola 4,023 zilitolewa Desemba 24, 2013 kwa ajili ya posho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa wafanyakazi wa TFF na Dola 30,000 zilitumika kwa semina elekezi kwa makocha iliyofanyika Lushoto (coach retreat at Lushoto), ripoti inasema.

Inaongeza: “Dola 2,829 zilitumika kutoa rambirambi na misaada, Dola 3,298 zikakopeshwa kwa Chama cha Soka Mbeya huku Dola 989 zikitolewa kwa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara zikiwa ni msaada.”

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa, Dola 90,000 zilitumika kulipia fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim P.

Source: Goal.com
 
Kwahiyo kumbe pale mwanzoni nilipomjibu Mtu hivi mlikuwa hamniamini? Nakubaliana tena nawe kuwa kwa 100% atakuwa ndiyo Yeye mwenyewe Mkuu. Aliamua kulitumia lile jina la mbele la Kikenya ili ' kutuzuga ' Watanzania lakini akasahau kuwa alipoamkia Yeye leo sisi wenzake tulilala majuzi. Kwa ninavyomjua huyu Jamaa akiona tu uzi wa Jamal Malinzi hawezi kuwa kimya na kwa mshangao mkubwa uzi sasa unaenda page ya 13 bado hajaleta ' pua ' yake humu.

Frank Wanjiru tafadhali ukitoka hapo Selander Bridge na TAKUKURU kabla hujaenda kuoga na kutoa ' nuksi ' ya kulala ' Lupango ' njoo huku tafadhali ' tuyajenge ' na ' tuyajadili ' kwani tungependa sana tusikie kutoka upande wako ' horse's mouth ' ili utumalizie ubishi.
kabsa mkuu afu aje akiri kwanini anajaribu kutuzuga sisi kwa kutuaminsha nyeusi kuwa nyeupe
 
Malinzi aligombea kupiga hela sio kukuza soka sasa ofisi nzima nshomile yani wakianza kuongea kilugha utafikiria uko muleba
 
Elimu yake please... Tusipeleke peleke watu tu hana ambao hawana elimu
Hao wenye elimu waliyopita wamewasaidia nini!Tff Inataka mtu wa mpira na mwenye uelewa hawa wavaa siri wenyei matumbo makubwa hata mpira hawajacheza wana ngangania Tff ili waibe tu!

Ova
 
Waogopeni hao wanaonunua ushindi kwavle lazma watatumia nafasi zao kurudisha kile walichotumia wakat wa kampeni
 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Jamal Malinzi amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini(TAKUKURU) akiwa katika harakati za kutembeza Mlungula.

Hatimae "Danganya Toto" ya Malinzi sasa imefikia kikomo.

Taarifa zaidi, zitakujia kupitia Uzi huu...

=====
UPDATE:
5d33c4389fb4ac0e184df79b48284a85.jpg
Jamal Malinzi

9d00e86a6e1309c125c313431a0c0257.jpg
Celestine Mwesigwa

Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Kwa matumizi mabaya ya Ofisi.



======
UPDATES:

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kwamba Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Celestine Mwesigwa usiku wa kuamkia leo tarehe 28, June, 2016 walikatamatwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini – TAKUKURU na huenda leo wakafikishwa mahakama ya mkazi Kisutu kujibu mashtaka juu ya matumizi mabaya ya ofisi.

Kwa muda mrefu kumekuwepo na tuhuma mbalimbali dhidi yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Taasisi hiyo ya kitaifa na inasemekana TAKUKURU wamekuwa kwenye uchunguzi dhidi kwa muda sasa mpaka jana walipoamua kuwatiwa nguvuni.

Hivi karibuni gazeti la Nipashe liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.

JAMALI AMEFANYA HAYA UFISADI WA KUTISHA TFF, Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.

Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.

Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.

Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).

Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.

Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.

Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.

Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza


====
Ndugu mwanaJF, rejea thread hizi nilizowahi kuleta kuhusiana na Ufisadi wa Jamal Malinzi na Timu yake.

1: UFISADI TFF: Bil 1.1 zachotwa ndani ya wiki 1, PCCB washikwa na kigugumizi kumpeleka Malinzi Kortini

2: UFISADI TFF: Malinzi mwogope Mungu, Fedha za TBL dola 425,000 umezichota kutoka akaunti hizi

Kumbe ni Mwaka Uliopita 2016????
 
Hili bwanyenye topetope limeharibu sana ligi kuu pia limeua soka kwa kupenda madaraka na wizi wa pesa za umma ili kunenepesha jitumbo lake na mashavu yake kama mimba ya panya. Likamuliwe hasa na lilipe pesa zote lilizoiba.
 
Huyu Malinzi aliingia TFF kupiga pesa na wala sio kuongoza Mpira ndio maana Mpira wa TZ umeshuka sana, Asirudi tena huyu. Kajaza kabila lake ili apige vizuri pesa na kuonea baadhi ya timu na watendaji wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom