Rais wa Msumbiji kwanini haongei Kiswahili?

Rais wa Msumbiji kwanini haongei Kiswahili?

Huyu rais wa Msumbiji nasikia elimu ya msingi ameipata hapa Tanzania, kwanini hatakikuongea Kiswahili?.

Anaongea lugha ya kwao tu, lakini viongozi wetu wanaongea kiingereza badala ya kiswahili.

Mgeni akija kwetu ningependa Rais wetu nae aongee kiswahili ili huyo mgeni aelewe kupitua mkalimani, sio kupiga makelele tu kuhamasisha kiswahili kwa Maneno, tunataka vitendo na kiongozi mkuu wa nchi Rais, yeye ndio awe mfano.

Umeongea vitu vingi kwa wakati mmoja. Kichw acha habari kinasema eti kwani haongei kiswahili? Lakini pia unaongelea lugha ya kiswahili kutotumiwa na viongozi wetu. Sasa sijui tukusaidiaje
 
Katoa hotuba fupi kuliko nilivyotarajia! Wabunge wenyewe wameachwa wanashangaa. Walitegemea hotuba ndeeefu salizozoea!
 
Kwa mtindo huu graduates wa linguistics wataishia kuwa walimu tu maana hata hizo kazi za UN ni kanjanja kupata. Laiti viongozi wangekuwa na nia ya kweli ya kuikuza lugha yetu nina hakika wakalimani wazuri tunao basi tu. Imagine angeongea kiswahili na kupata mkalimani atakayemtafsiria mheshimiwa wa Msumbiji kwa lugha ya kwao.... just thinking aloud
 
Pamoja na lugha zaidi ya 4 ninazoweza kuongea na kuandika kwa ufasaha, mimi na kiswahili ni damdam.Nikiongea kifaransa utasema nimezaliwa paris, nikija kiingereza utadhani kwetu ni UK,Kijerumani ndio usiseme.....kiarabu nacho si haba haswa cha mashariki ya kati.

My take, lugha zao tuzijue lakini tudumishe ya kwetu ambayo ni kiswahili. Kutokujua lugha sio ushamba kama wadhaniavyo watu wengi.
 
Huyu rais nishakutana nae mara kibao tu akiwa na wabongo anaongea kiswahili kama kakulia tandale nimekutana nae tangu akiwa waziri na mpaka sasa rais
 
pooocha voces tanzanianos sao confusos de mais...................gostam maning de reclamar....pooorah pah isso nao tem nada ver, a nossa língua oficial é portugues cara,tem que saber.
 
Jana kupitia ITV taarifa ya habari wakati yupo chuo cha Diplomasia nimemsikia akibonga Kiswahili safi kabisaa....
 
Aliongea kiswahili tena muda mrefu tu akiwanasihi watanzania. Mleta mada umekurupuka kuhusu rais wa msumbiji.

Kikwete ndo alikosea kuongea kiingereza wakati mgeni anakifahamu vyema kabisa kimatumbi.

Aibu kwa kikwete!!
 
kwani Tanzania lugha za mawasiliano katika maeneo ya kijamii au maofisini nizipi??
 
hivi nyinyi mnakijua mnachobishania. si muulize kama hamjui............................
:sad:
 
mkapa anajua kiingereza kuliko raisi yeyote aliyewah kutokea afrika mashariki na kati
 
pooocha voces tanzanianos sao confusos de mais...................gostam maning de reclamar....pooorah pah isso nao tem nada ver, a nossa língua oficial é portugues cara,tem que saber.

Mkuu hebu tafsiri kidogo ili wengine tuambulie.
 
Umeongea vitu vingi kwa wakati mmoja. Kichw acha habari kinasema eti kwani haongei kiswahili? Lakini pia unaongelea lugha ya kiswahili kutotumiwa na viongozi wetu. Sasa sijui tukusaidiaje

Soma comments za watu wengine humu utaelewa nilichokuwa na maanisha.
 
pooocha voces tanzanianos sao confusos de mais...................gostam maning de reclamar....pooorah pah isso nao tem nada ver, a nossa língua oficial é portugues cara,tem que saber.

Obligado muito bem.
 
Alikuwa anaongea Kireno lugha ya taifa la Msumbiji. Lugha hii imetokana na mkoloni Mreno aliyewatawala. Huko Msumbiji hakuna asiyejua na kuongea kwa ufasaha Kireno.
 
Back
Top Bottom