JK kwa nini haongei Kireno?Rais wa Msumbiji kwanini haongei Kiswahili?
.
JK kwa nini haongei Kireno?
Huyu rais wa Msumbiji nasikia elimu ya msingi ameipata hapa Tanzania, kwanini hatakikuongea Kiswahili?.
Anaongea lugha ya kwao tu, lakini viongozi wetu wanaongea kiingereza badala ya kiswahili.
Mgeni akija kwetu ningependa Rais wetu nae aongee kiswahili ili huyo mgeni aelewe kupitua mkalimani, sio kupiga makelele tu kuhamasisha kiswahili kwa Maneno, tunataka vitendo na kiongozi mkuu wa nchi Rais, yeye ndio awe mfano.
Nilijisikia vibaya sana juzi my prezidaa kazungumza kingereza
Sijapenda kwa kweli acha tu niwe mkweli kwa hili
Kichekesho cha nchi hii bana. unakuta kiongozi analazimisha sijui wanafunzi wajifunze kiswahili yeye anapeleka watoto wake kwenye shule ya kiingereza. Ajira zikitoka wanapewa wale wanaoujua kiingereza kwanza!!!
JK kwa nini haongei Kireno?
Jamani acheni majungu kwani Kireno ni lugha ya asili ya Msumbuji? Yeye Katumia Kireno wa kwetu Kiingereza tatizo liko wapi? Wote wametumia lugha za kikoloni. Kwa hiyo basi wote wawili wamekuwa influenced na cultural imperialism mmoja anamtukuza bawana wake mreno na mwenzake anamtukuza bwaba wake Mwingereza hapo ngoma draw. Kama Rais wa Msumbiji angeongea kimakonde ningeona kuna pointi lakini kwa sasa prezida wetu hajafanya kosa lolote. Wao wanajitutumua kwa Kireno na sisi tuna jitutumua kwa Kiingereza. Chezea sisi wewe!
Msumbiji kireno nikama lugha ya taifa, wamakonde karibu woote wa msumbiji wanajua kireno. Kwahiyo kuongea kwake kireno sio bahati mbaya, naamini huenda hata hicho kimakonde hakijui kama anavyo jua kireno kwahiyo yeye kwake ni fahari kuongea kireno.
Kusoma hapa Tanzania hakuhalalishi kujua Kiswahili. Kuna shule nyingi tu zinatumia syllabus za kigeni ikiwa ni pamoja na lugha ya kufundishia. Raisi Nyusi wa Msumbiji alisoma shule ya Msingi Frelimo iliyopo wilayani Tunduru na baada ya hapo alirudi kwao kwa masomo ya sekondari na kuendelea. Ni vyema ukajiridhisha kama hiyo Frelimo Primary School ilikuwa inatoa elimu kwa kutumia lugha gani!Jk, hajui kireno, huyo wa msumbiji anajua kiswahili vizuri, na hata elimu ya msingi ameipata hapahapa, ...