Rais wa FIFA amuuliza Hersi "Hivi nyie ndiyo mliwaibia pesa wale Wanigeria"?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,136
7,905
Leo Rais wa FIFA aliyekuja kuiona timu yake ya Simba ikipambana na Al Ahly alikwenda katika kituo cha mafunzo cha TFF na Rais wa Yanga, Hersi Said akaona huyu bila kumfuata huko huko aliko naweza nisije kumuona tena maishani mwangu. Basi akazamia hivyo viwanja vya TFF, Infantino akienda huku, Hersi yumo, akienda kule, yumo, kama vile ye ndiyo katibu wa TFF.

FIFA.jpeg


Infantino akaona huyu jamaa ni vipi tena mbona ameniganda hivi? Akamuuliza, hivi nyie si ndo mliwapulizia sumu wale wanigeria mkawaibia kitita chao, dahh Hersi nguvu ikamuishia, akaanza kujitetea "ooh unajua wanigeria walikuwa wanataka kutuchafua sisi ni wananchi..." Wasaidizi wa Infantino walionekana kuzozana wakiulizana, "hivi bosi yuko salama kweli? Huyu ni nani, mbona jana hatukumuona?" Wakati Hersi akiendelea kujitetea kama kafumaniwa, Infantino akampigia secretary wake, alivyokata SIMU akamuuliza na yule Kocha aliyewaita manyani vipi mlimalizana naye? Hersi nguvu zikamuishia kabisa ila akakumbuka kuna bakuli lilipitishwa fedha zilipotimia wakamlipa mtesi wao.

Hersi akamkaribisha kwenye mechi ya Yanga na Azam, Infantino akasema "yaani nimetoka kuangalia mpira wa kiwango cha African Football League nije kuwaangalia kina Kibabage na Mzize? Acha masikhara sheikh. Kwanza kesho nawahi Cairo kuwasapoti chama langu Simba. Simba guvu moya"

Ushauri wangu kwa Hersi na Yanga, jaribuni kudeal na CAF, hao ndiyo mchezo mzima na njia nzuri ya kuifikia FIFA. Huyo Infantino hawezi kuwa na msaada kwenu kama hamjajenga connection CAF.
 
Hersi alijaribu kumpeleka Infantino Kimbiji lakini waaaapiii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom