Rais umenisononesha kwenye BBC News

Thubutuuu, Wadanganyika bado wanamuomba Mungu ashuke awasaidie matatizo yao #$$^$% zetu!
 
Hivi nyie bado mnapoteza muda kufatilia kauri za Jk? Huyu mdingi kishatia pamba masikioni kiasi kwamba haoni wala hasikii. Sasa hivi anachokifanya akishaona mambo yanazidi kuharibika yeye huyooooooo anaenda zake kutalii huko ng'ambo.
akitokea mtu wa kabila la ****** yani sitakubali apewe hata ujumbe wa nyumba kumi.
 
pole bado unaaminihuyo ni rais ??labda wa bagamoyo si ulimsikilia hata mtoto wa ifm anajibu yale maswali
 
Jamaa ni mzee wa majibu mepesi kwa maswali magumu! Amejaa mbwembwe tu mdomoni, aliniudhi sana.
 
Kwa kweli huu ukosefu wa umeme ni tatizo kubwa sana na linamuathiri kila Mtanzania kasoro labda viongozi wa serikali hii. Last week nilikuwa naanzisha project ya kujenga kanyumba changu nikaenda kununua matofali nikaambiwa ni za kuorder na kusubiria sabababu mitambo ya kutengeneza matofali inatumia umeme na umeme hamna na hivyo hata bei ya tofali imepanda sababu yako machache. wa kulaumiwa ni viongozi wa serikali sababu toka walipoanza kutuingiza kwenye mikataba mibovu wakianza na ITPL mpaka Richmond tatizo linaongezeka.

Huwezi kusema tatizo ni ukame wakati toka mwaka 1992 serikali ilipoingia mkataba na IPTL tatizo hilo lilikuwa linajulikana. Na swala hapa sio ukame sababu tuna mito kibao na kwa hasara tunayoendelea kuipata kutoka IPTL na mikataba mingine ya kifisadi tungeweza kuanzisha chanzo kingine cha umeme wa maji kwenye vyanzo vingine vya uhakika zaidi kama huko Stiglers gorge, Malagarasi nk. Wakati fulani Daniel Yona akiwa waziri wa nishati na madini alisema eti mkataba wa IPTL ni sawa na wewe uwe na harusi, ualike kampuni ya kukupikia uwaambie waandae chakula cha watu 200 alafu wakaja watu 20, kwahiyo hauna ujanja zaidi ya kulipa gharama ya watu 200 ata kama wamekula watu 20. Nikasema kwa hali ya kawaida kwenye harusi zetu watu huzidi labda kama Yona alimaanisha harusi za ulaya au za mafisadi wanaoishi kama wako ulaya kwenye hili giza la umeme. unaweza kuona ni jinsi gani hatuko makini katika kushughulikia umeme mpaka tunaingia mikataba ambayo tunakuwa tunapata hasara kila kukicha.

Mkurugenzi wa TANESCO aliyepita Dr. Idrissa alisema nchi itaingia gizani kama mitambo ya kuzalisha umeme haitapatikana haraka hiyo ilikuwa mwaka 2008 kama sijakosea. Wanasiasa akiwemo raisi Kikwete wakasema watahakikisha hali hiyo haitatokea, leo imetokea. Ingekuwa nchi zingine kama Japan asinge subiri kuambiwa ajiuzulu, yeye angekuwa ashajiuzulu. Nawashangaa sana wanaomtaka Ngeleja ajiuzulu wakati tatizo kama alivyosema mwenyewe baada ya bajeti yake kugonga ukuta kwamba hili ni swala la serikali nzima. Kikwete anatoa 1.7 trillion kwa ajili ya 'wafanyabiashara' wachache eti wasiathirike na anguko la uchumi!! Tunaoathirika na ukosefu wa umeme anatuambia tatizo ni ukame!! Kwanini tusiamini kwamba hizo 1.7 trillion zimeliwa na Mafisadi anaowakumbatia??? Anahitaji mbinu gani za kitaalamu zaidi ya Mkurugenzi wa TANESCO aliyekuwa anawakilisha wataalamu wa fani husika??!!!

Napendekeza
tuanze kuanzisha Hydro-elecric power plant zingine sababu kwa kweli ndo umeme raisi tutakaoweza kuumudu. Huu ndo uwe mpango wa mda mrefu ukijumuishwa na makaa ya mawe. Sisi (TANESCO) tusiingie mkataba na kampuni yoyote ili kuzalisha umeme sababu tatizo litaendelea kuongezeka. taratibu tuanze kuifuta iliyopo. Kwa sasa kanuni za manunuzi zivunjwe ili TANESCO wakiwezeshwa na serikali wanunue mitambo hata kama ni ya mtumba (mbona tunavaa mitumba na tunang'aa) haraka ili izalishe umeme kututoa gizani na kunusuru maisha yetu kiuchumi na kijamii. Umeme iwe huduma muhimu ya serikali kwa watu wake na maendeleo yao na sio suala la watu kufanya biashara sababu hatuna wafanyabiashara wa ngazi ya kuzalisha umeme ambao hawatakuwa mafisadi au mawakala wa mafisadi na watatuongezea tu matatizo juu ya tatizo tulilonalo.

Kwa kweli hili ni tatizo kubwa sana. Tunahitaji umeme sio mipango na kutaja tumeongeza megawati kadhaa. Acheni Ujuha nyie wenye madaraka ya kuongoza nchi hii.

Naomba kuwasilisha haswa haswa kwa Raisi Kikwete na wenzake waliopo Seriakalini. MUNGU atulinde na atuongoze tutatue tatizo hili, Amen.
 
hata mie nimelisikia lijamaa linazid kutulipua. he is the worst we've ever had in the southern hemisphere! tupeane pole kwakuwa bado lipo lipo sana! au tufanye ki tunisia tunisia....kimalawi malawi...
 
Mabango ya kanisa la fgbf church Dar, yarudishwe. Na zile nyaya zilizo pitishwa karibu na kanisa zisogezwe kama alivyo shauri mtumishi wa Mungu Kakobe. La hawakufanya hivo giza bado liko palepale. Kumbuka wakat wa uchaguzi Kakobe alisema 1Samweli 8:18. Msilie machungu ya umeme
 
Sishangai kwa majibu hayo Mkwe.re kulamba gentleman pass UD ya GPA ya 2.1
 
Beaking News ITV na Radio One leo mchana, Jairo amesimamishwa kazi, CAG atafanya uchunguzi wa kifedha Wizarani hapo kuthibitisha kama mashtaka dhidi ya Jairo apelekwe kwa pirato.

kumbuka Jairo ni mmoja ya swahiba wa JK na alikuwa msaidizi wake binafsi kabla ya kumpa ukatibu mkuu. ukaribu wao ndiyo ulimfanya Jairo kuwa powerful wizarani na kufuja hela kabla hata kashifa hii.
halafu ukisha ona mara rais akija atatoa maamuzi yake, mara katibu mkuu kiongozi kaamuru uchunguzi ufanyike hiyo yote ni dana dana, mwiso wa siku Jairo huyoooo anapeta tu, huku sisi tubaki aaaah
 
Mkuu Nyange,
Siku yoyote ukikutana na mtu yoyote yule akakuambia tatizo la umeme limetokana na ukame,muulize hivi:-
"Kwa mara ya kwanza The Great Ruaha ulikauka 1954,ukaanza kukauka 1991 mpaka leo unakauka kilomita 75 toka ihuguru mpaka mtera kila majira ya kiangazi,na tatizo siyo mvua kukosekana,kwani 1997 kulikuwa na mm800 kutokana na EL NINO na bwawa la mtera lilikosa maji kiangazi vilevile na lilijaza maximum ya sentimeta 30 tu" kwanini?
Huyu mtangazaji wa BBC swahili angekuwa more prepared,JK angebanwa vizuri sana,ila ndio hivyo tena!....wamekutana!
 
Kimsingi, kwa wachunguzi wa kauli kwa umakini, rais ame abdicate majukumu yake.

Ukiwa na jukumu la kuwaongoza watu, hata katika matatizo ambayo hayajulikani utatuzi wake - kutafuta dawa ya kansa na UKIMWI kwa mfano, sembuse haya ya umaskini tu kama kukosa umeme-, kiongozi unatakiwa kutafuta ufumbuzi, sio kutoa kisingizio cha "mungu". Na ukishindwa ujiuzulu ili wengine wakusaidie.

Hizi kauli za kumsingizia mungu ni uzushi tu. Sasas sie Watanzania wengine ambao hatuamini katika mungu rais Kikwete atatupa kauli gani?

Halafu Kikwete kumsingizia mungu si mara ya kwanza. Maafa ya kufa kwa wachimba madini huko Mererani, ambayo kimsingi ni swala la udhibiti mbovu wa usalama katika mchakato wa uchimbaji, rais Kikwete aliuita "mapenzi ya mungu".

Kama nchi inaenda kwa neema ya mungu maana ya kuwa na viongozi ni nini sasa? Si wajiuzulu wote tujue moja kwamba nchi inaendeshwa na mungu ?

Mie siamini mungu, naamini katika sayansi.Na mtu yeyote anayemtaja mungu kama chanzo cha matatizo namuona mzushi tu. Kikwete anaweza kuniambia nini kunielewesha kwamba yeye si mzembe?
 
Wenyewe wanaita power crises!! Hivi viongozi wetu wanaakili kweli?!!!. Wakati financial crisis ndio ilitakiwa ituumize vichwa si umeme, kuna haja ya kutegemea umeme wa maji tu?!
 
Mkuu Nyange,
Siku yoyote ukikutana na mtu yoyote yule akakuambia tatizo la umeme limetokana na ukame,muulize hivi:-
"Kwa mara ya kwanza The Great Ruaha ulikauka 1954,ukaanza kukauka 1991 mpaka leo unakauka kilomita 75 toka ihuguru mpaka mtera kila majira ya kiangazi,na tatizo siyo mvua kukosekana,kwani 1997 kulikuwa na mm800 kutokana na EL NINO na bwawa la mtera lilikosa maji kiangazi vilevile na lilijaza maximum ya sentimeta 30 tu" kwanini?
Huyu mtangazaji wa BBC swahili angekuwa more prepared,JK angebanwa vizuri sana,ila ndio hivyo tena!....wamekutana!
Kobello, wewe si umesema ni magamba daima hadi kifo?
 
Ukisikiliza unaweza kutoa machozi. Rais anasema tatizo ni mvua naukame, hapo kwanza anakwepa majukumu yake ya kuliandaa taifa na majanga.
Yaani hana solution isipokuwa kudra tu. Ni Kikwete alikuwa waziri wa nishati na tatizo kama hili lilitokea, ingekuwa ni nafasi nzuri kwake kujua ufumbuzi kuliko mtu mwingine. Inaonyesha hakuwahi kujifunza lolote kabla ya kuelekea magogoni.

Anasema, serikali yake tu imeongeza megawati 300 ukilinganisha na zilizokuwepo tangu tupate uhuru. Haiujuilikani amwekeza wapi kwa hizo 300 kuingia katika grid ya taifa. Alichosema nikukandia yaliyofanywa na watangulizi wake hasa Nyerere. Kikwete hajatuambia amejenga mabwawa mangapi yaliyoongeza mw 300, kama ni jenerata je hiyo ni sustainable project?

Amejisifia kuwa mradi wa kihansi ulifanyika akiwa waziri wa nishati, hakueleza kuwa IPTL yenye rushwa chafu na iliyojenga rushwa katika sekta ya nishati ililetwa na yeye akiwa waziri. Hukujisifia kuwa Richmond iliyokuja wakati akiwa Rais ilizalisha kiasi gani. Rais amesahau kuwa ni yeye alisema katika kamati kuu kuwa Dowans ilipwe kabla ya kubadilisha kauli baada ya wabunge wake kumjia juu. Alichofanya ni kuchukua credit za kazi za wenzake na kutotaja makosa lukuki aliyoyafanya katika sekata ya nishati akiwa waziri na Rais yanayoliumiza taifa leo. Mengi yake yakiwa utendaji na kusaini mikataba mibovu na mengine ni kulinda wahujumu wa nishati kwa tume, haditihi na ngano, leo anamsingizia mungu.Kenya wana ukame mkali mbona tataizo si kubwa kuliko hapa kwetu.

Kama alivyosema Kobello hapo juu, kama mtangazaji angekuwa makini basi tungekuwa na cha kucheka zaidi. Kama Rais anasema tatizo ni mungu kutoleta mvua na si mabwawa yanayopungua ujazo basi kuna tatizo kubwa.
 
Ulioleta hii mada unam quote Rais out of context, mbona huongei na laivyosema kuwa kwa awamu zote zilizopita umeme uliwekezwa ni 600MW tu na nyingi zinategemea vyanzo vya maji. Na katika kipindi chake kifupi 145MW tayari (si za kutegemea maji) na mitambo mingine ipo njiani ambayp imeagizwa kuanzia June mwaka jana, mipya kabisa. Na uwekezaji mwingine kwenye makaa ya mawe na njia zingine mbadala, mbona yote hayo huyasemi? Au ulitaka mitambo ikiagizwa leo kesho ifanye kazi? Unanshangaza! Kakosea nini hapo na ndivyo vyanzo vya umeme alivyovikuta na mvua zimegoma kujaza mabwawa, hayo ndio baadhi ya matatizo aliyokuta kawachiwa na awamu zilizopita nae anafanya kila njia kuhakikisha anayatatua na mfano mzuri kuwa mitambo imeagizwa na mikataba imesainiwa na jitihada zinafanywa sio kama hazifanywi ulitaka nini zaidi ya hicho?
 
Hii ndo dawa si anapenda kutembeatembea halafu kujieleza hawezi. kajitakia mwenyewe hata haangalii mfano wa marahisi wanaotuzukuka yeye anafikiri ni bora kuliko wao
 
Ulioleta hii mada unam quote Rais out of context, mbona huongei na laivyosema kuwa kwa awamu zote zilizopita umeme uliwekezwa ni 600MW tu na nyingi zinategemea vyanzo vya maji. Na katika kipindi chake kifupi 145MW tayari (si za kutegemea maji) na mitambo mingine ipo njiani ambayp imeagizwa kuanzia June mwaka jana, mipya kabisa. Na uwekezaji mwingine kwenye makaa ya mawe na njia zingine mbadala, mbona yote hayo huyasemi? Au ulitaka mitambo ikiagizwa leo kesho ifanye kazi? Unanshangaza! Kakosea nini hapo na ndivyo vyanzo vya umeme alivyovikuta na mvua zimegoma kujaza mabwawa, hayo ndio baadhi ya matatizo aliyokuta kawachiwa na awamu zilizopita nae anafanya kila njia kuhakikisha anayatatua na mfano mzuri kuwa mitambo imeagizwa na mikataba imesainiwa na jitihada zinafanywa sio kama hazifanywi ulitaka nini zaidi ya hicho?


Hahaa zaidi ya hiyo sasa ni safari tu za nje. KILIMO KWANZA bila viwanda inawezekana?
 
Back
Top Bottom