Rais Trump: Tiktok haitaongezewa muda Marekani

Faith Luvanga

Member
Aug 21, 2018
14
15
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa tarehe ya mwisho iliyopagwa kwajili ya kampuni ByateDace ya China kuuza programu nukushi ya Tiktok nchini humo haitaongezwa.​

Trump ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla hajaondoka kwenda Michigan kuendelea na kampeni yake na kuongeza kuwa programu hiyo itafungwa au kuuzwa ikiwa China haitaiuza hadi kufikia tarehe ya mwisho iliyopangwa.​

Kampuni hiyo imekua ikiangalia mnunuzi wa programu hiyo ili iweze kuuza mpaka kufikia katikati ya mwezi Septemba 2020 ili kutimiza agizo la rais Trump.​

Tiktok ni programu nukushi ya video inayoruhusu watu kupakia video fupi, iliyojizolea umaarufu zaidi Marekani hususan kwa vijana. Lakini Serikali ya Marekani inadai kuwa taarifa za watu wanaotumia programu hiyo zinahifadhiwa nchini China. Tiktok imesema haiwezi kukubaliana na ombi lolote la Serikali ya China kuhusu kutoa taarifa za watumiaji wake.​

Seneta wa Chama cha Republic, Josh Hawley, ambaye ni mshirika wa karibu wa Trump, ameiambia Reuters kuwa yeye pia haungi mkono suala la kampuni hiyo kuongezewa muda, na kuongeza kuwa hakuunga mkono matokeo ambayo hayakuhusisha uchunguzi kamili.​

Mapema mwezi Septemba Reuters iliripoti kuwa wanunuzi wa Tiktok walikua wakijadili njia kadhaa za kuchukua umiliki wa ByteDance, ambazo zilijumisha kuratibu shughuli zote zinazo fanyika nchini Marekani.​
 
Hapo masikini ukiwa nacho tajiri anakunyang'anya hata kwa kulipa


Ikishauziwa wa marekani itafikia hatua ya WhatsApp na instergram
 
Back
Top Bottom