- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na hii video ikisambaa katika mitandao ya kijamii na kuelezwa kuw Rais Wa Marekani Donald Trump amezidiwa na amekimbizwa hospital
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinachoonesha msafari wa magari ukiwa na ving'ora na kusababisha magari mengine kusimamam na kuelezwa kuwa ni msafara wa Rais Donald Trump akiwahishwa hospital.
Chanzo kimoja kiliandika.
"Taarifa zisizothibitishwa zinaeleza Rais Trump amekimbizwa hospital, barabara zafungwa"
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa taarifa hizo si za kweli.
Ufuatiliaji kwa kutumia maneno muhimu umejirirdhisha kuwa hakuna chanzo chcohote cha kuaminika ndani na nje ya Marekani kilichochapisha hiyo kueleza kuwa Rais Trump amekimbizwa hospital.
Aidha video iliyoambatanishwa na Taarifa hizo si ya mwaka 2026, video hiyo ilichapishwa mwaka 2024 wakati Rais Donald trump aliposhambuliwa kwa risasi alipokuwa akifanya kampeni za kugombea Urais.
Vyanzo mbalimbali viliripoti taarifa iliyoambatana na video hiyo mwaka 2024 na kuelezwa kuwa Mgombea huyo wa Urais ametolewa Hospital na kusindikizwa na msafar mkubwa wa polisi.
Hata hivyo hakuna Taarifa yyote kutoka Ikulu ya Marekani ama Donald Trump mwenyewe kuthbitisha kuwa hali ya kiongozi huyo ni mbaya na hivyo amekimbizwa hospitalini.
Vile vile Ras Trump ameonekana akiendelea kuchapisha taarifa mbalimbali kupitia ukurasa wake wa Truth kuelezea mambo mbalimbali ikiwemo vita inayoendelea baina ya na Iran na wao.
Ukurasa wa Commentary wa machapisho ya Rais Trump kupitia ukurasa wa X umeandika kuwa Taarifa hizo si za kweli na zipuuzwe.
"President Trump is not ill and not at Walter Reed Hospital.Ignore all of the fake news"