Rais, Tanzania si chochote katika utalii

Rais, Tanzania si chochote katika utalii

Hivi ni kwanini ujaajiriwa Tanzania Tourist Board,hongera sana mdau umeleza vizuri wadau wa utalii wizarani chukueni huo ujumbe utafaa sana.
 
Yaani nchi yetu hii watu wake ni majanga kabisa. Sasa mtu kaanza kwa kulalamika, kaandika zaidi ya maneno 10000 kukosoa na mwisho eti Rais ampe mbinu za kuongeza mapato na kuifanya nchi kivutio kikuu cha utalii. Kweli?????!!!!!!
Hivi nguvu yote hiyo aliyotumia mpaka kutafuta takwimu za nani anaongoza ktk utalii, ameshindwa kabisa kutafuta hata wazo moja la kushauri nini kifanyike??
Siku hii nchi watanzania tutaacha kulalamika na kuanza tumia akili zetu kutoa mawazo boresho hakika tutasonga mbele.
Halalamiki bro. Nilivyomuelewa mimi anataka serikali ilinde hicho tulicho nacho tayari na iongeze mapato kwa kuongeza idadi ya watalii.
 
Rais Magufuli hatutakuelewa kama pamoja na vyote tulivyo navyo, lakini mapato ya utalii yataendelea kuwa chini kuliko ya Afrika Kusini, Misri, Morocco, Tunisia na Kenya, huku wewe mwenyewe ukisema tuna vivutio vingi vya utalii. Tuna vivutio vya utalii visivyovutia watalii.
Tanzania ina vivutio vingi lakini vingapi vinafikika kwa urahisi? Hatujaweza kuwa na infrastructure na facilities za kuweza kuattract hawa wageni wa bei kubwa tuanaowataka. Western na Southern circuit zinapokea wageni wachache sana, tour operators wanakuwa wagumu kuuza hizo destinations wanajua ugumu wa kupeleka watalii hayo maeneo.

Gharama za uhifadhi, kutunza haya maeneo yabaki kuwa vivutio vinavyovutia na kuuzika haitoki pengine, ni mapoto haya haya haya ya utalii. Fedha za kufanya doria zitakapopungua au kukosekana kabisa na mbuga kugeuka vichaka vya majangili, wawindaji haramu na wachome mkaa, hao wanyama watabaki kweli?

Mapato yatokanayo na uwindaji wa kitalii baada ya bei kupandishwa mwaka 2008 yameshuka sana na yanaendelea kushuka outfitters wengi walishindwa gharama za kumiliki vitalu na kuviacha wazi kwa sababu idadi ya hunting clients imepungua. Tumeshuhudia ujangili ukiongezeka kwa kasi kubwa kwenye reserves hasa ya ujangili wa tembo. Reserves zimegeuka kuwa malisho ya mifugo huku wahifadhi wakilalamika hawana vitendea kazi na fedha za kuendesha doria za kila siku. Kwa nini hatukujifunza?
 
Kwani Rwanda umewaona kweye hiyo list ya mtoa mada,una mahaba na Rwanda au ndo kwenu?
Sidhani kama ni swala la mahaba. Rwanda ni region ya east africa na katika biashara yoyote wa kuchunga sana ni yule mshindani wako wa karibu.
 
Huyu chalii buana,yaani badala ya kujisikitikia kama Taifa,wewe underrate,hivi kumbe na wewe umerogwa kama wengine. Toa njia mbadala what should we do as nation to tackle this situation and become the leading tourism nation in Africa
 
Way foward ipo tatizo kusoma hutaki...hiv leo VAT kwenye utalii wakati hata kumi bora hatupo Africa ..tunategemea nn halafu tuna kiburi...kumbuka utalii hauishi.....tutoze vitu vinavyo isha kama gas,madini na uwindaji kododi kubwa kwasababu hivyo vinaisha.......Analysis iliyotetwa ni nzuri sana ,ila wengi kusoma hawawez....
 
Sidhani kama ni swala la mahaba. Rwanda ni region ya east africa na katika biashara yoyote wa kuchunga sana ni yule mshindani wako wa karibu.
Watu wanaoongea sana wanaweza kukuhamisha kwenye mada,Rwanda kuna nini? Gorilla? mbna hata siye tunao kigoma au hujui?,mtoa mada kazungumzia kuboreshwa kwa mazingira ya utalii maana utalii ni starehe siyo idadi ya fisi, nyumbu au twiga,kifupi tuboreshe mazingira ili kuwe na utofauti, mtalii anapokuja hapa ajisikie au aone utofauti flan na nchi alizowahi kuzitembelea.Sasa wewe umekimbilia Rwanda ndiyo maana nikakuuliza una mahaba na Rwanda au kwenu?
 
Sawa lakini kikubwa hapa ni bei zetu za bidhaa hiyo ya utalii ukilinganisha na majirani zetu ambao ndio washindani katika bidhaa hiyo ambayo ni watu.
 
Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa. Mwenzio kaonyesha kabisa kwa data kuhusu utalii, ww unajifanya mzalendo huna data hata moja zaidi ya kusema tuna vivutio vingi tofauti nyuma ya Brazil wala huna data kutoka chanzo chochote. Au wewe ndio mmojawapo ya watu mnaompotosha rais kwamba tuna vivutio vingi mpaka watalii wanagombea kuja Tanzania? Ww ndio wale mliomezeshwa data kwenye vyuo vya siasa na hamna mjualo zaidi ya uzalendo wa kulinda tumbo.
Hakuna mwenyehaki ya kuidharau Tz na watz...hatakama Una dégrées 800. Mnaleta viuchambuzi vyenu visivyo na way forward huku mkipewa kazi hamuwezi...acheni mabadiliko yaje tukikosea tutajirekebisha. Uzalendo kwanza hao watalii wasioweza lipakodi wapelekeni makwenu ndo msimamo wasasa
 
Watanzania ni watu wenye bahati mbaya sana maana mara nyingi wanaaminishwa kuwa wao ni bora katika kila kitu. Wengi wao, kwa ujinga tu, nao wameyabeba maneno hayo na kuyaweka katika vichwa vyao.

1.Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote Duniani, ambao ni uwongo, lakini wao wanaamini

2. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa tuna gas nyingi kuliko nchi yoyote, ambao ni uwongo

3. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina madini ya kila namna na ina madini mengi kuliko nchi yoyote Duniani/Afrika, ambao ni uwongo

4. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye amani kuliko nchi zote za Afrika, ambao ni uwongo

5. Wapo Watanzania wanoamini kuwa nchi yetu ina demokrasia, utawala wa sheria na uongozi mzuri kuliko nchi yoyote ya kiafrika, nao ni uwongo lakini wanaamini

6. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana ambayo kila mwanadamu angependa kuja na kuishi, nao ni uwongo lakini wengi wanaamini hivyo

7. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi na mazingira mazuri ya utalii ambayo hayapo mahali pengine popote Duniani, ambao ni uwongo mkubwa.

Takwimu za mwaka 2014 kuhusu utalii wa kimataifa (International tourist arrivals) inaonesha kuwa hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo ilikuwa miongoni mwa nchi 10 za juu katika kutembelewa na watalii. Hii inaonesha kuwa watalii hawa wa kizungu wanapendelea zaidi kwenda kwenye mabara mengine kuliko Afrika.

In 2014, there were 1.133 billion international tourist arrivals worldwide, with a growth of 4.3% as compared to 1.087 billion in 2013.[1] The top 10 international tourism destinations in 2014 were

1. France Europe 83.7 million
2. United States North America 74.8 million
3. Spain Europe 65.0 million
4. China Asia 55.6 million
5. Italy Europe 48.6 million
6. Turkey Europe 39.8 million
7. Germany Europe 33.0 million
8. United Kingdom Europe 32.6
9. Russia Europe 29.8 million
10. Mexico North America 29.1

Katika Afrika, Tanzania haipo hata katika 10 bora

In 2014, there were over 55.7 million international tourist arrivals to Africa, the top ten African destinations were
1. Morocco 10.2 million
2. Egypt 9.6 million
3. South Africa 9.5 million
4. Tunisia 6.0 million
5. Algeria — 2.7 million
6. Mozambique — 1.8 million
7. Zimbabwe 1.8 million
8. Kenya — 1.4 million
9. Uganda — 1.2 million
10. Namibia — 1.1 million

Jambo la kusikitisha ni kwamba, nchi inayoongoza kwa kutembelewa na watalii wageni katika Afrika ambayo ni Morocco, idadi ya watalii inaowapokea ni chini ya watalii wanaotembelea nchi ya mwisho ya 10 bora ya Ulaya.

In 2014, there were over 582 million international tourist arrivals to Europe, an increase of 3.0% over 2013. In 2014, the top ten destinations were

1. France 83.7 million
2. Spain 65.0 million
3. Italy 48.6 million
4. Turkey 39.8 million
5. Germany 33.0 million
6. United Kingdom 32.6 million
7. Russia 29.8 million 28.4
8. Austria 25.2 million
9. Greece 22.0 million
10. Poland 16.0 million

Ukija kwenye mapato ya utalii, Tanzania na Afrika si lolote na si chochote. Idadi kubwa ya watalii inawianika kwa kiwango kikubwa na mapato ya utalii. Hayo maneno ya kusema kuwa unaweza kuwa na watalii wachache halafu mapato yakawa makubwa ni ndoto za alinacha zinazootwa na maprofesa wa Tanzania pekee.

International tourism receipts grew to US$1,245 billion in 2014, corresponding to an increase in real terms of 3.7% from 2013.[11] The World Tourism Organization reports the following countries as the top ten tourism earners for the year 2014, with the United States by far the top earner.
1
23px-Flag_of_the_United_States.svg.png
United States North America $177.2 billion
2
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Europe $65.2 billion
3
23px-Flag_of_the_People%27s_Republic_of_China.svg.png
China Asia $56.9 billion
4
23px-Flag_of_France.svg.png
France Europe $55.4 billion
5
23px-Flag_of_Macau.svg.png
Macau Asia $50.8 billion
6
23px-Flag_of_Italy.svg.png
Italy Europe $45.5 billion
7
23px-Flag_of_the_United_Kingdom.svg.png
United Kingdom Europe $45.3 billion
8
23px-Flag_of_Germany.svg.png
Germany Europe $43.3 billion
9
23px-Flag_of_Thailand.svg.png
Thailand Asia $38.4 billion
10
23px-Flag_of_Hong_Kong.svg.png
Hong Kong Asia $38.4 billion

Kwa mapato ya utalii wa kimataifa katika Afrika, nchi inayoongoza ni Afrika Kusini ($9.4 billion) ikifuatiwa na Misri ($7.2 billion), Morrocco ($7.1 billion) na Tunisia ($2.3 bilion). Kwa ujumla yule anayeongoza kwa mapato ya utalii katika Afrika hayupo katika 10 bora za Dunia, na ni chini ya mapato ya nchi ya mwisho ya 10 bora katika mabara mengine.

Mapato ya utalii ya Tanzania kwa mwaka 2014 yalikuwa $1.95 billion, chini kuliko mapato ya Singapore ($19.20 billion), Turkey ($37.37 billion), Qatar (10.58 billion) au Misri ($7.21 billion). Singapore, Turkey, Qatar na Misri hawana twiga wala tembo lakini wanatuzidi kwa idadi ya watalii na kimapato mara dufu.

Profesa Maghembe, Rais wetu na Watanzania, wanatakiwa kufahamu kuwa vivutio vya utalii ni zaidi ya idadi ya tembo, fisi, twiga, pundamilia na ngiri tulio nao. Utalii mkubwa ni akili, yaani unaweza kufanya nini kwa kutegemea mazingira yako ili watu wa mataifa mengine waje kushuhudia na kustarehe katika mazingira yako.

Watanzania, kwa ujinga wetu, tunaamini kuwa kwa sababu tu tuna nyumbu wengi, twiga na tembo basi watu wengi, Dunia nzima wanahangaika ili waje watazame sura ya twiga. Watalii hawana haja na sura ya pundamilia wala mbwa mwitu bali wanataka kuona mazingira ya kuvutia yaliyo tofauti na mahali pengine, na sisi tunaweza kuwatumia wanyama hao kuweza kuyafanya mazingira yetu kuwa ya kuvutia zaidi kuliko Misri ambako mapiramidi na chuo kikuu cha kwanza cha Alexandria, vimetosha kuizidi Tanzania kimapato.

Ushauri wangu kwa Rais, fukuza kazi prof. Maghembe maana amekupotosha kwa kueleza kuwa hakuna uhusiano wa mapato katika utalii na idadi ya watalii. Waziri unayetakiwa kuwa naye ni yule ambaye ataihakikishia Tanzania inapata ongezeko kubwa la watalii na siyo upungufu wa watalii. Bila ya kujali kama ongezeko la idadi ya utalii na mapato ya utalii vitategemea kupungua kwa kodi au kuondoa baadhi ya kodi, au kuongeza mbinu za kujitangaza au kuboresha miundombinu na huduma za kitalii, ukweli ni kwamba tunahitaji ongezeko la idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii ambavyo vinaenda sambamba hata kama siyo kwa uwiano 1:1

Rais Magufuli hatutakuelewa kama pamoja na vyote tulivyo navyo, lakini mapato ya utalii yataendelea kuwa chini kuliko ya Afrika Kusini, Misri, Morocco, Tunisia na Kenya, huku wewe mwenyewe ukisema tuna vivutio vingi vya utalii. Tuna vivutio vya utalii visivyovutia watalii.

Mheshimiwa Rais, hotuba zako za mara kwa mara za kuelezwa nchi hii imeibiwa sana tumekwishazisikia kiasi cha kutosha, sasa tunahitaji kusikia kutoka kwako juu ya mbinu za kuongeza mapato ya utalii (siyo kodi za utalii bali mapato), mbinu za kuongeza mauzo ya mazao yetu nje ya nchi, mkakati wa kujenga uchumi wa viwanda, na namna rasilimali nyingine kama gas na madini zinavyoweza kubadilishwa kuwa mapato ya wananchi na Taifa. Mheshimiwa Rais tunataka mbinu na mikakati ya kuongeza mapato ya Watanzania.

Sisi wengine daima tutazidi kueleza pale tunapoona mbinu siyo sahihi. Tunaamini una dhamira njema lakini tuna mashaka makubwa katika mbinu.

Binadamu tuna miaka michache Duniani, hatuna muda wa kufanya majaribio bali tunatakiwa kuenenda kwa namna na mbinu zilizosahihi katika kuibadilisha nchi hii iliyo maskini kupindukia lakini iliyo na fursa nyingi zilizofunikwa. Fursa ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kitalii ni kubwa sana lakini hatuna watu wa kuweza kufungua fursa hizo ili jamii iweze kuziona kwa sababu waliopewa mamlaka ya kuzifunua kwa umma wanafanya kila mbinu ya kuzifunika ili wananchi wasizione na wala wasizifaidi.
Asante Mkuu....mungu akubariki sana,sijui wewe ndiye yule mkinga wa mada za channel ten pamoja na kilala?
Safi sana,
 
Bahati mbaya mkulu amezungukwa na wapiga waragi,wanajisifia wingi wa fisi na bundi kama vile Kenya hawapo,Bahati nzuri wanyama hawa huhama kila msimu,washauri wa utalii wa Kenya watawashauri watalii wawasubiri wanyama wakiwa Kenya....pole Tanzania ni Mara nyingine tena umepata bahati mbaya kuliko iliyopita
 
Labda lengo ni kuiua kiuchumi mikoa iliyochagua chadema kwa kuwa huko biashara ya utalii iko juu sana
 
Hongera sana mkuu, Heshima mbele. umetafakari, umechambua, umetafiti, umeandika. Nikiangalia ID yako naona umejiunga JF siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Hii inanipa matumaini kwamba hata baada ya Mzee Mwanakijiji kuchanganyikiwa, kuna kizazi kipya cha wachambuzi wenye hoja nzito, zilizofanyiwa utafiti. (RIP Mzee Mwanakijiji) Ee, maana kama mtu anataka kukupinga, akatafute hizo data na kuja na zingine tofauti na hizo.

Ila mimi nilipomsikiliza Rais wetu mpendwa sana akiongelea kodi zilizoongezwa katika utalii, alipokuwa anahutubia Polisi, naona kwamba actually yeye ndiye aliyekataa kuondoa kodi hiyo. ile tone yake, namna anavyoongea, si kwamba ameshauriwa vibaya, ila yeye ndiye kawashauri washauri wake, ushauri ambao kwa maneno mengine ni amri. haina tofauti na siku ile aliposema "nawaomba wanasiasa wenzangu waache siasa za ushindani wasubiri mwaka 2020", halafu siku chache baadaye akawaagiza polisi kwa lugha kali sana, wamshughulikie yeyote atakayekaidi "agizo". kwa hiyo hakuna tofauti kati ya "ombi" na "amri". kadhalika ukiangalia mapendekezo mengi sana ya serikali kwenye bajeti, yalipita vilevile bila mabadiliko makubwa, na sababu ni kwamba kuna mtu aliyetia ngumu. kwa hiyo ushauri wako kwa mheshimiwa Rais kwamba amtimue Magembe, nadhani hapa hauhitaji kwa sababu kama Magembe yuko tayari kuimba nyimbo na kucheza ngoma inayopigwa Ikulu, basi wala hana tatizo.
It is very true by almost 100 %

Nchi yetu hivi sasa inaendeshwa kwa staili ya ONE MAN SHOW.........

Katika hali halisi ndiyo maana wasaidizi wake hata pale wanapoona Bosi wao yupo 100% wrong, lakini katika serikali hii hakuna mwenye courage ya kumwambia Mfalme kuwa uko 'uchi'

Mtu pekee niliyemshuhudia akisimamia ukweli na kuamua kutokuwa mnafiki ni Gavana wa BoT, Profesa Ndulu aliyesema wazi kuwa mabenki yako sahihi by 100% kuwaarifu wateja wao kuwa mzigo wa VAT wakati wa kutumia services za benki ni wao customers na wala siyo wa mabenki....

Wakati Dr Mpango akiamua kusisitiza kuwa eti mzigo wa VAT ni wa mabenki!

Hivi ina maana Dr Mpango pamoja na kuwa mchumi aliyebobea ameamua tu kusimamia kitu ambacho siyo cha kweli kwa staili ile ile ya kumpiga 'fix' Mfalme kuwa amevaa nguo nzuri sana na anapendeza ile mbaya wakati anatembea barabarani akiwa uchi?
 
Watanzania ni watu wenye bahati mbaya sana maana mara nyingi wanaaminishwa kuwa wao ni bora katika kila kitu. Wengi wao, kwa ujinga tu, nao wameyabeba maneno hayo na kuyaweka katika vichwa vyao.

1.Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote Duniani, ambao ni uwongo, lakini wao wanaamini

2. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa tuna gas nyingi kuliko nchi yoyote, ambao ni uwongo

3. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina madini ya kila namna na ina madini mengi kuliko nchi yoyote Duniani/Afrika, ambao ni uwongo

4. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye amani kuliko nchi zote za Afrika, ambao ni uwongo

5. Wapo Watanzania wanoamini kuwa nchi yetu ina demokrasia, utawala wa sheria na uongozi mzuri kuliko nchi yoyote ya kiafrika, nao ni uwongo lakini wanaamini

6. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana ambayo kila mwanadamu angependa kuja na kuishi, nao ni uwongo lakini wengi wanaamini hivyo

7. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi na mazingira mazuri ya utalii ambayo hayapo mahali pengine popote Duniani, ambao ni uwongo mkubwa.

Takwimu za mwaka 2014 kuhusu utalii wa kimataifa (International tourist arrivals) inaonesha kuwa hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo ilikuwa miongoni mwa nchi 10 za juu katika kutembelewa na watalii. Hii inaonesha kuwa watalii hawa wa kizungu wanapendelea zaidi kwenda kwenye mabara mengine kuliko Afrika.

In 2014, there were 1.133 billion international tourist arrivals worldwide, with a growth of 4.3% as compared to 1.087 billion in 2013.[1] The top 10 international tourism destinations in 2014 were

1. France Europe 83.7 million
2. United States North America 74.8 million
3. Spain Europe 65.0 million
4. China Asia 55.6 million
5. Italy Europe 48.6 million
6. Turkey Europe 39.8 million
7. Germany Europe 33.0 million
8. United Kingdom Europe 32.6
9. Russia Europe 29.8 million
10. Mexico North America 29.1

Katika Afrika, Tanzania haipo hata katika 10 bora

In 2014, there were over 55.7 million international tourist arrivals to Africa, the top ten African destinations were
1. Morocco 10.2 million
2. Egypt 9.6 million
3. South Africa 9.5 million
4. Tunisia 6.0 million
5. Algeria — 2.7 million
6. Mozambique — 1.8 million
7. Zimbabwe 1.8 million
8. Kenya — 1.4 million
9. Uganda — 1.2 million
10. Namibia — 1.1 million

Jambo la kusikitisha ni kwamba, nchi inayoongoza kwa kutembelewa na watalii wageni katika Afrika ambayo ni Morocco, idadi ya watalii inaowapokea ni chini ya watalii wanaotembelea nchi ya mwisho ya 10 bora ya Ulaya.

In 2014, there were over 582 million international tourist arrivals to Europe, an increase of 3.0% over 2013. In 2014, the top ten destinations were

1. France 83.7 million
2. Spain 65.0 million
3. Italy 48.6 million
4. Turkey 39.8 million
5. Germany 33.0 million
6. United Kingdom 32.6 million
7. Russia 29.8 million 28.4
8. Austria 25.2 million
9. Greece 22.0 million
10. Poland 16.0 million

Ukija kwenye mapato ya utalii, Tanzania na Afrika si lolote na si chochote. Idadi kubwa ya watalii inawianika kwa kiwango kikubwa na mapato ya utalii. Hayo maneno ya kusema kuwa unaweza kuwa na watalii wachache halafu mapato yakawa makubwa ni ndoto za alinacha zinazootwa na maprofesa wa Tanzania pekee.

International tourism receipts grew to US$1,245 billion in 2014, corresponding to an increase in real terms of 3.7% from 2013.[11] The World Tourism Organization reports the following countries as the top ten tourism earners for the year 2014, with the United States by far the top earner.
1
23px-Flag_of_the_United_States.svg.png
United States North America $177.2 billion
2
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Europe $65.2 billion
3
23px-Flag_of_the_People%27s_Republic_of_China.svg.png
China Asia $56.9 billion
4
23px-Flag_of_France.svg.png
France Europe $55.4 billion
5
23px-Flag_of_Macau.svg.png
Macau Asia $50.8 billion
6
23px-Flag_of_Italy.svg.png
Italy Europe $45.5 billion
7
23px-Flag_of_the_United_Kingdom.svg.png
United Kingdom Europe $45.3 billion
8
23px-Flag_of_Germany.svg.png
Germany Europe $43.3 billion
9
23px-Flag_of_Thailand.svg.png
Thailand Asia $38.4 billion
10
23px-Flag_of_Hong_Kong.svg.png
Hong Kong Asia $38.4 billion

Kwa mapato ya utalii wa kimataifa katika Afrika, nchi inayoongoza ni Afrika Kusini ($9.4 billion) ikifuatiwa na Misri ($7.2 billion), Morrocco ($7.1 billion) na Tunisia ($2.3 bilion). Kwa ujumla yule anayeongoza kwa mapato ya utalii katika Afrika hayupo katika 10 bora za Dunia, na ni chini ya mapato ya nchi ya mwisho ya 10 bora katika mabara mengine.

Mapato ya utalii ya Tanzania kwa mwaka 2014 yalikuwa $1.95 billion, chini kuliko mapato ya Singapore ($19.20 billion), Turkey ($37.37 billion), Qatar (10.58 billion) au Misri ($7.21 billion). Singapore, Turkey, Qatar na Misri hawana twiga wala tembo lakini wanatuzidi kwa idadi ya watalii na kimapato mara dufu.

Profesa Maghembe, Rais wetu na Watanzania, wanatakiwa kufahamu kuwa vivutio vya utalii ni zaidi ya idadi ya tembo, fisi, twiga, pundamilia na ngiri tulio nao. Utalii mkubwa ni akili, yaani unaweza kufanya nini kwa kutegemea mazingira yako ili watu wa mataifa mengine waje kushuhudia na kustarehe katika mazingira yako.

Watanzania, kwa ujinga wetu, tunaamini kuwa kwa sababu tu tuna nyumbu wengi, twiga na tembo basi watu wengi, Dunia nzima wanahangaika ili waje watazame sura ya twiga. Watalii hawana haja na sura ya pundamilia wala mbwa mwitu bali wanataka kuona mazingira ya kuvutia yaliyo tofauti na mahali pengine, na sisi tunaweza kuwatumia wanyama hao kuweza kuyafanya mazingira yetu kuwa ya kuvutia zaidi kuliko Misri ambako mapiramidi na chuo kikuu cha kwanza cha Alexandria, vimetosha kuizidi Tanzania kimapato.

Ushauri wangu kwa Rais, fukuza kazi prof. Maghembe maana amekupotosha kwa kueleza kuwa hakuna uhusiano wa mapato katika utalii na idadi ya watalii. Waziri unayetakiwa kuwa naye ni yule ambaye ataihakikishia Tanzania inapata ongezeko kubwa la watalii na siyo upungufu wa watalii. Bila ya kujali kama ongezeko la idadi ya utalii na mapato ya utalii vitategemea kupungua kwa kodi au kuondoa baadhi ya kodi, au kuongeza mbinu za kujitangaza au kuboresha miundombinu na huduma za kitalii, ukweli ni kwamba tunahitaji ongezeko la idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii ambavyo vinaenda sambamba hata kama siyo kwa uwiano 1:1

Rais Magufuli hatutakuelewa kama pamoja na vyote tulivyo navyo, lakini mapato ya utalii yataendelea kuwa chini kuliko ya Afrika Kusini, Misri, Morocco, Tunisia na Kenya, huku wewe mwenyewe ukisema tuna vivutio vingi vya utalii. Tuna vivutio vya utalii visivyovutia watalii.

Mheshimiwa Rais, hotuba zako za mara kwa mara za kuelezwa nchi hii imeibiwa sana tumekwishazisikia kiasi cha kutosha, sasa tunahitaji kusikia kutoka kwako juu ya mbinu za kuongeza mapato ya utalii (siyo kodi za utalii bali mapato), mbinu za kuongeza mauzo ya mazao yetu nje ya nchi, mkakati wa kujenga uchumi wa viwanda, na namna rasilimali nyingine kama gas na madini zinavyoweza kubadilishwa kuwa mapato ya wananchi na Taifa. Mheshimiwa Rais tunataka mbinu na mikakati ya kuongeza mapato ya Watanzania.

Sisi wengine daima tutazidi kueleza pale tunapoona mbinu siyo sahihi. Tunaamini una dhamira njema lakini tuna mashaka makubwa katika mbinu.

Binadamu tuna miaka michache Duniani, hatuna muda wa kufanya majaribio bali tunatakiwa kuenenda kwa namna na mbinu zilizosahihi katika kuibadilisha nchi hii iliyo maskini kupindukia lakini iliyo na fursa nyingi zilizofunikwa. Fursa ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kitalii ni kubwa sana lakini hatuna watu wa kuweza kufungua fursa hizo ili jamii iweze kuziona kwa sababu waliopewa mamlaka ya kuzifunua kwa umma wanafanya kila mbinu ya kuzifunika ili wananchi wasizione na wala wasizifaidi.
Kwa sasa bandari, watalii ni kitendawili tu.watalii wote wamehamia kenya na wafanyabiashara wote wa bandari ya dsm wamehamia mombasa na bandari zingine zinazo wajali wateja.sisi tunabaki na hadithi njoo uongo njoo
 
Labda lengo ni kuiua kiuchumi mikoa iliyochagua chadema kwa kuwa huko biashara ya utalii iko juu sana
Labda lengo ni kuiua kiuchumi mikoa iliyochagua chadema kwa kuwa huko biashara ya utalii iko juu sana
Wala hoja siyo hiyo hata kidogo kwa kuwa sekta ya utalii ndiyo inayoongoza kwa kuingiza pesa nyingi za kigeni, kuzipita sekta zote kama vile Madini na kilimo.

Kwa maana hiyo haiingii akilini hata chembe kwa mtu mwenye dhamana ya wizara ya utalii anasimama hadharani kuwa nchi hii haihitaji watalii masikini wavaa mabegi migongoni, wakati hao hao watalii anaowaponda ndiyo wanaomnunulia hayo magari yake ya V8 anayotamba nayo barabarani hadi anapata kiburi cha kuwatukana hao hao watalii malofa ambao hiyo 'haba na haba hujaza kibaba' ndiyo inayowawezesha wao Mawaziri waishi kama Malaika na sasa wanataka kuwafukuza hao watalii wasije nchini ili Taifa likose pesa za kigeni ili watawala wetu watimize azma yao ya kutufanya sisi watanzania tuishi kama mashetani........
 
Ukifuatilia kwa umakini, utaona nimetoa mapendekezo. Pendekezo kubwa ni kwa wahusika wa sekta kutambua kuwa utalii ni biashara, hivyo zinahitajika mbinu za kuboresha mazingira ya biashara hii ili yavutie watalii. Mazingira yetu yaonekane ni tofauti na ya sehemu nyingine kwa ubora kwa kutumia kile ambacho wengine hawana. Na hapo ndipo akili na werevu unapohitajika ili kujua ni nini na kwa namna gani tunaweza kufanya. Tusiamini kwa vile tu tuna pundamilia au twiga, eti kwa sababu tu hawapo sehemu nyingine, basi kila mtu atakuja kwetu au anataka kuja Tanzania. Utalii ni starehe, ni lazima uandamane na starehe. Ni namna gani utalii wetu unaweza kuwa unique na kuandamana na starehe? Haya ni mambo ambayo watendaji wa sekta hii wanatakiwa kuyafanyia kazi. Sisi kama wadau tuliopo nje, ushauri tunaotoa ni wa jumla, na wao wanatakiwa kuingia ndani zaidi kuyafanyia kazi mawazo yetu ili yaweze kuonekana katika uhalisia.

Umetoa suluhisho thabiti sana. Kinacholeta shida mara nyingi ni misconceptions. Yaani mtu anaamini amelielewa tatizo kumbe hajalielewa halafu anakimbilia kutoa majibu. Ukijenga tabia ya kufikiria majawabu peke yake ukaacha kufikiri kuhusu tatizo, mara nyingi utatoa majawabu ambayo si sahihi. Mamdani anasema 90% ya majibu yanapatikana katika ku-define problem. Ukipatia definition ya tatizo, ni kama vile una 90% ya jibu ya hilo tatizo. Vyuo vyetu vinafundisha kutafuta majawabu, badala ya kufundisha ku-define problems. Rais wetu na washauri wake wanashindwa kuielewa "multiplier effect" ya utalii. Tatizo ni misconceptions na mihemuko ya kutaka kuongeza makusanyo ya kodi bila kufikiria athari.
 
Mimi binafsi nilikuwa nakuna kichwa, hivi hiyo nyongeza ya bajeti ya shilingi trilioni 7 kutoka shilingi trilioni 22 ya mwaka jana wakati wa Kikwete hadi trilioni 29 ya awamu hii ya Magufuli nyongeza hizo wanatumia miujiza gani kuzipata?

Sasa ndiyo nimepata jawabu kumbe ndiyo hizo pesa za VAT walizopania kuzipata toka kwa wananchi malofa kwenye miamala yao ya simu na wakati wote wanapotumia huduma za benki huku wakiamua kuziba 'pamba' masikioni kugoma kabisa kumsikiliza mtu yeyote atakayewaeleza impact kubwa kiuchumi itakalolipata Taifa kama watalazimisha huo mpango wao.

Tayari madhara tumeanza kuyaona kwa kuwa watalii hao malofa ndiyo walikuwa wakifikia Hotel za kawaida ambazo sasa kwa kuwakosa watalii hao baadhi ya Hoteli hizo tayari zimeshafunga shughuli zake na kuzigeuza Hosteli, kama ile Hoteli iliyopo Ubungo ambayo inamilkiwa na Mheshimiwa Mbunge wa Chama Cha CCM.

Hilo suala litaleta madhara makubwa sana nchini kama hatua za dharula hazitachukuliwa kwa kuwa kuna ajira za vijana maelfu kwa maelfu wanaofanya kazi za hoteli ambazo zitapotea na hao vijana watarudi mitaani na kuishi kama mashetani.......
 
Ungekuja na solutions siyo lawama mwanzo mwisho
Du kwa hiyo hujaona suluhisho alilotoa? Au hujaelewa alichoandika? Yaani wewe umekariri tu kusema hajatoa suluhisho? Mbona kaweka kila kitu wazi kwa weledi mkubwa? aAu hasira za kukosolewa malaika wako zimekupofusha akili!
 
Hakuna mwenyehaki ya kuidharau Tz na watz...hatakama Una dégrées 800. Mnaleta viuchambuzi vyenu visivyo na way forward huku mkipewa kazi hamuwezi...acheni mabadiliko yaje tukikosea tutajirekebisha. Uzalendo kwanza hao watalii wasioweza lipakodi wapelekeni makwenu ndo msimamo wasasa

Hakuna mwenye tatizo la kulipa kodi maana sisi hatukuzoea vya bure kama nyie mnaolipiwa kila kitu na serekali. Sisi ni wanaume wa shoka tumezoea kujitegemea bila kujali fadhila kama nyie mnaolipiwa mpaka malazi na familia zenu. Shida iliyopo ni timing ya hiyo kodi, ungekuwa unajua biashara hii wangalau tungeweza kuongea lugha moja. Sasa hapa tunaongea na wewe mzalendo wa kulinda kujaza tumbo lako inakuwa ngumu kuelewana.
 
Back
Top Bottom