Rais, Tanzania si chochote katika utalii

Rais, Tanzania si chochote katika utalii

Watanzania ni watu wenye bahati mbaya sana maana mara nyingi wanaaminishwa kuwa wao ni bora katika kila kitu. Wengi wao, kwa ujinga tu, nao wameyabeba maneno hayo na kuyaweka katika vichwa vyao.

1.Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote Duniani, ambao ni uwongo, lakini wao wanaamini

2. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa tuna gas nyingi kuliko nchi yoyote, ambao ni uwongo

3. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina madini ya kila namna na ina madini mengi kuliko nchi yoyote Duniani/Afrika, ambao ni uwongo

4. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye amani kuliko nchi zote za Afrika, ambao ni uwongo

5. Wapo Watanzania wanoamini kuwa nchi yetu ina demokrasia, utawala wa sheria na uongozi mzuri kuliko nchi yoyote ya kiafrika, nao ni uwongo lakini wanaamini

6. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana ambayo kila mwanadamu angependa kuja na kuishi, nao ni uwongo lakini wengi wanaamini hivyo

7. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi na mazingira mazuri ya utalii ambayo hayapo mahali pengine popote Duniani, ambao ni uwongo mkubwa.

Takwimu za mwaka 2014 kuhusu utalii wa kimataifa (International tourist arrivals) inaonesha kuwa hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo ilikuwa miongoni mwa nchi 10 za juu katika kutembelewa na watalii. Hii inaonesha kuwa watalii hawa wa kizungu wanapendelea zaidi kwenda kwenye mabara mengine kuliko Afrika.

In 2014, there were 1.133 billion international tourist arrivals worldwide, with a growth of 4.3% as compared to 1.087 billion in 2013.[1] The top 10 international tourism destinations in 2014 were

1. France Europe 83.7 million
2. United States North America 74.8 million
3. Spain Europe 65.0 million
4. China Asia 55.6 million
5. Italy Europe 48.6 million
6. Turkey Europe 39.8 million
7. Germany Europe 33.0 million
8. United Kingdom Europe 32.6
9. Russia Europe 29.8 million
10. Mexico North America 29.1

Katika Afrika, Tanzania haipo hata katika 10 bora

In 2014, there were over 55.7 million international tourist arrivals to Africa, the top ten African destinations were
1. Morocco 10.2 million
2. Egypt 9.6 million
3. South Africa 9.5 million
4. Tunisia 6.0 million
5. Algeria — 2.7 million
6. Mozambique — 1.8 million
7. Zimbabwe 1.8 million
8. Kenya — 1.4 million
9. Uganda — 1.2 million
10. Namibia — 1.1 million

Jambo la kusikitisha ni kwamba, nchi inayoongoza kwa kutembelewa na watalii wageni katika Afrika ambayo ni Morocco, idadi ya watalii inaowapokea ni chini ya watalii wanaotembelea nchi ya mwisho ya 10 bora ya Ulaya.

In 2014, there were over 582 million international tourist arrivals to Europe, an increase of 3.0% over 2013. In 2014, the top ten destinations were

1. France 83.7 million
2. Spain 65.0 million
3. Italy 48.6 million
4. Turkey 39.8 million
5. Germany 33.0 million
6. United Kingdom 32.6 million
7. Russia 29.8 million 28.4
8. Austria 25.2 million
9. Greece 22.0 million
10. Poland 16.0 million

Ukija kwenye mapato ya utalii, Tanzania na Afrika si lolote na si chochote. Idadi kubwa ya watalii inawianika kwa kiwango kikubwa na mapato ya utalii. Hayo maneno ya kusema kuwa unaweza kuwa na watalii wachache halafu mapato yakawa makubwa ni ndoto za alinacha zinazootwa na maprofesa wa Tanzania pekee.

International tourism receipts grew to US$1,245 billion in 2014, corresponding to an increase in real terms of 3.7% from 2013.[11] The World Tourism Organization reports the following countries as the top ten tourism earners for the year 2014, with the United States by far the top earner.
1
23px-Flag_of_the_United_States.svg.png
United States North America $177.2 billion
2
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Europe $65.2 billion
3
23px-Flag_of_the_People%27s_Republic_of_China.svg.png
China Asia $56.9 billion
4
23px-Flag_of_France.svg.png
France Europe $55.4 billion
5
23px-Flag_of_Macau.svg.png
Macau Asia $50.8 billion
6
23px-Flag_of_Italy.svg.png
Italy Europe $45.5 billion
7
23px-Flag_of_the_United_Kingdom.svg.png
United Kingdom Europe $45.3 billion
8
23px-Flag_of_Germany.svg.png
Germany Europe $43.3 billion
9
23px-Flag_of_Thailand.svg.png
Thailand Asia $38.4 billion
10
23px-Flag_of_Hong_Kong.svg.png
Hong Kong Asia $38.4 billion

Kwa mapato ya utalii wa kimataifa katika Afrika, nchi inayoongoza ni Afrika Kusini ($9.4 billion) ikifuatiwa na Misri ($7.2 billion), Morrocco ($7.1 billion) na Tunisia ($2.3 bilion). Kwa ujumla yule anayeongoza kwa mapato ya utalii katika Afrika hayupo katika 10 bora za Dunia, na ni chini ya mapato ya nchi ya mwisho ya 10 bora katika mabara mengine.

Mapato ya utalii ya Tanzania kwa mwaka 2014 yalikuwa $1.95 billion, chini kuliko mapato ya Singapore ($19.20 billion), Turkey ($37.37 billion), Qatar (10.58 billion) au Misri ($7.21 billion). Singapore, Turkey, Qatar na Misri hawana twiga wala tembo lakini wanatuzidi kwa idadi ya watalii na kimapato mara dufu.

Profesa Maghembe, Rais wetu na Watanzania, wanatakiwa kufahamu kuwa vivutio vya utalii ni zaidi ya idadi ya tembo, fisi, twiga, pundamilia na ngiri tulio nao. Utalii mkubwa ni akili, yaani unaweza kufanya nini kwa kutegemea mazingira yako ili watu wa mataifa mengine waje kushuhudia na kustarehe katika mazingira yako.

Watanzania, kwa ujinga wetu, tunaamini kuwa kwa sababu tu tuna nyumbu wengi, twiga na tembo basi watu wengi, Dunia nzima wanahangaika ili waje watazame sura ya twiga. Watalii hawana haja na sura ya pundamilia wala mbwa mwitu bali wanataka kuona mazingira ya kuvutia yaliyo tofauti na mahali pengine, na sisi tunaweza kuwatumia wanyama hao kuweza kuyafanya mazingira yetu kuwa ya kuvutia zaidi kuliko Misri ambako mapiramidi na chuo kikuu cha kwanza cha Alexandria, vimetosha kuizidi Tanzania kimapato.

Ushauri wangu kwa Rais, fukuza kazi prof. Maghembe maana amekupotosha kwa kueleza kuwa hakuna uhusiano wa mapato katika utalii na idadi ya watalii. Waziri unayetakiwa kuwa naye ni yule ambaye ataihakikishia Tanzania inapata ongezeko kubwa la watalii na siyo upungufu wa watalii. Bila ya kujali kama ongezeko la idadi ya utalii na mapato ya utalii vitategemea kupungua kwa kodi au kuondoa baadhi ya kodi, au kuongeza mbinu za kujitangaza au kuboresha miundombinu na huduma za kitalii, ukweli ni kwamba tunahitaji ongezeko la idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii ambavyo vinaenda sambamba hata kama siyo kwa uwiano 1:1

Rais Magufuli hatutakuelewa kama pamoja na vyote tulivyo navyo, lakini mapato ya utalii yataendelea kuwa chini kuliko ya Afrika Kusini, Misri, Morocco, Tunisia na Kenya, huku wewe mwenyewe ukisema tuna vivutio vingi vya utalii. Tuna vivutio vya utalii visivyovutia watalii.

Mheshimiwa Rais, hotuba zako za mara kwa mara za kuelezwa nchi hii imeibiwa sana tumekwishazisikia kiasi cha kutosha, sasa tunahitaji kusikia kutoka kwako juu ya mbinu za kuongeza mapato ya utalii (siyo kodi za utalii bali mapato), mbinu za kuongeza mauzo ya mazao yetu nje ya nchi, mkakati wa kujenga uchumi wa viwanda, na namna rasilimali nyingine kama gas na madini zinavyoweza kubadilishwa kuwa mapato ya wananchi na Taifa. Mheshimiwa Rais tunataka mbinu na mikakati ya kuongeza mapato ya Watanzania.

Sisi wengine daima tutazidi kueleza pale tunapoona mbinu siyo sahihi. Tunaamini una dhamira njema lakini tuna mashaka makubwa katika mbinu.

Binadamu tuna miaka michache Duniani, hatuna muda wa kufanya majaribio bali tunatakiwa kuenenda kwa namna na mbinu zilizosahihi katika kuibadilisha nchi hii iliyo maskini kupindukia lakini iliyo na fursa nyingi zilizofunikwa. Fursa ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kitalii ni kubwa sana lakini hatuna watu wa kuweza kufungua fursa hizo ili jamii iweze kuziona kwa sababu waliopewa mamlaka ya kuzifunua kwa umma wanafanya kila mbinu ya kuzifunika ili wananchi wasizione na wala wasizifaidi.
Umeandika vitu vya maana sana tena sana....

Lakini wasiwasi wangu ni kuwa hizo 'nondo' ulizoshusha zitafall under deaf ears za watawala wetu.....

Nimewasikia Profesa Maghembe na Rais Magufuli wakitoa kauli za kushangaza sana kuhusiana na ongezeko hilo la VAT kwa huduma zote za kitalii kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Alianza Profesa Maghembe ambaye aliongea kwa kiburi cha hali ya juu kuwa Tanzania haihitaji watalii 'malofa' wabeba mabegi migongoni mwao!

Akaendelea kutamba kuwa Tanzania inahitaji watalii wachache lakini wenye 'pesa zao' na hao watalii wabeba mabegi ni bora wabaki huko huko kwao Ulaya!

Naweza kuiita kauli hiyo ni ya masikini jeuri!

Kwa kuwa haiingii akilini kwa hao hao wazungu ambao siku zote sisi huwa tunatembeza bakuri la omba omba kwao, leo tukajigeuza sisi ndiyo matajiri na hatuna haja ya hao wazungu 'malofa' waje kutalii nchini kwetu!

Rais wetu naye katoa kauli jana inayofanana na ya Waziri wake kwa kusema yeye anachotaka watalii hao walipe hiyo kodi iliyokuwa introduced July mosi bila kutoa visingizio vyovyote na Rais akaenda mbali zaidi kwa kusisitiza kuwa ni bora kuwa na watalii laki 5 wanaolipa kodi kubwa kuliko kuwa na watalii milioni 2 wanaolipa kodi kidogo!

Hivi Rais anataka kusema kuwa keshasahau ile principle inayosema haba na haba hujaza kibaba?

Hata hivyo hii serikali ya awamu ya 5 inaelekea kuwa si sikivu hata kidogo......

Tukumbuke hoja ya msingi kabisa waliyotoa Tour Operators ni kuwa hizo bookings za hao watalii ambao walikuwa waanze kuja mwezi huu wengi wao bookings zao walizifanya zamani toka mwaka jana wakati hiyo VAT ilikuwa bado haijawa introduced.

Tukumbuke kuwa mifumo ya maisha ya wenzetu wazungu huwa wanapenda wakati wote kufanya bajeti ya mambo yao mapema.

Sasa wanaiona nchi hii ya ajabu sana kwa staili yake ya kukurupuka....

Hivi serikali hii ilishindwa nini kuintroduce hiyo VAT yao kuanzia July mwaka 2017, na kipindi chote hiki hadi mwakani Tour Operators wetu wafanye kazi ya kuwajulisha watalii wetu ili wajiandae na mabadiliko hayo yatakayoanza mwakani?

Sasa hivi ndiyo naelewa ni kwa nini serikali yetu imepiga STOP kuonyeshwa Bunge LIVE, sababu kuu kumbe ni kuwa serikali hii haitaki kabisa mawazo yoyote mbadala nje ya 'fikra sahihi' za watawala wetu, kwa kuwa wamejipa uwezo wa kiMungu mtu!
 
Cha kufanya tutumie vizuri hicho kidogo tulicho nacho na tusijione kwamba sisi ni special sana kwamba tutabembelezwa na mataifa mengine.

Vivutio vyenyewe havifahamiki tunabembelezewa nini sasa. Mtalii kapotezea uhai Kilimanjaro, International reporters wanasema Kenya's Mt Kilimanjaro,, kazi tunayo...

Bado tunajiona tupo special, kwa lipi haswa😉😵
 
Sijuhi tutafika lini walipo wenzetu hakika twahitaji watu makini na ubunifu siyo matamko tatizo siyo Tozo wala VAT tu changamoto ni nyingi sana kwa hii Tourism?
 
Wewe mwenyewe umeshahamasishwa kujichukia nani atakupenda,na umeshavaa upofu wa kutokutaka kuona vyako nani ataviona,tunakosoa sana hatuonyeshi njia mbadala!
Usijitoe akili na acha uvivu wa kusoma.

Soma post mwanzo hadi mwisho. Au zile hesabu zinakuchanganya

Rudia tena na usome kwa umakini mwandishi ametoa solution ya nini kifanyike.
 
Good Advice But We Cannot Build Tz OverNight.
Mistakes Are Inevitable.
 
Mkuu analysis yako ni nzuri sana tena umeibackup with fact and figures, ila kama Mystery alivosema , watakuja watu and not even think and consider about what you are trying to say , even for a moment, ila watatry to punch holes in your article and that's the most disappointing part
Lakini wasiwasi ni kuwa hizo 'nondo' ulizoshusha zitafall under deaf ears........
 
Kwani Rwanda wanapata watalii wangapi na mapato kiasi gani
 
Kuna utamaduni humu wa mtu kuandika hoja fulani halafu wachangiaji wengi tu wanakosoa wakimtaka aliyeandika atoe suluhisho. Hivi kweli Watanzania wenzangu hatuwezi kujituma vichwani tukawaza na kuumiza vichwa kuchanganua hoja fulani iliyopo mezani mpaka mleta mada ndiye atoe suluhisho?
Tubadilike, mara nyingi hoja zinaletwa ili tutumie akili majibu tuyatafute wenyewe siyo kutafuniwa kila kitu. Elimu, elimu, elimu.
Hongera mleta hoja.
 
Je, watalii wanapokuja wachache, mapato ya mamlaka ya hifadhi za taifa na ngorongoro zinapungua au zinaongezeka au zinabaki pale pale?

Kama idadi ya watalii haihusiani na mapato ya fedha za utalii, kwa nini huko nyuma Serikali imejitahidi kuvutia watalii wengi?

Kama idadi ya watalii haihusiani na mapato ya fedha za utalii, kwa nini mojawapo ya targets za utalii zimejikita katika idadi ya watalii?
 
Je, watalii wanapokuja wachache, mapato ya mamlaka ya hifadhi za taifa na ngorongoro zinapungua au zinaongezeka au zinabaki pale pale?

Kama idadi ya watalii haihusiani na mapato ya fedha za utalii, kwa nini huko nyuma Serikali imejitahidi kuvutia watalii wengi?

Kama idadi ya watalii haihusiani na mapato ya fedha za utalii, kwa nini mojawapo ya targets za utalii zimejikita katika idadi ya watalii?


Kuna mambo unapswa uelewe kuhusu Utalii wetu na hili pia Raisi Maguduli ameliongelea, ni kwamba hatutaki cheap mass tourism bali tunataka watalii ambao hawataharibu Mali asili zetu, Hifadhi zetu, tunataka Serengeti ibakie kuwa Serengeti mwaka 2070 na hii ndiyo moja kati ya sababu kwa nini Utalii Tanzania siku zote ni aghali klk nchi nyingi za Kiafrika, kupanda Ml.Kili peke yake ni karibu USD 700 wkt kupanda Ml.Kenya ni USD 70, kwenda Serengeti au Ngorongoro ni aghali ukilingansiha na nchi nyingine na kuna sababu kwa nini imefanywa hivi na hili siyo kwa kwa sababu tu Serikali inataka iwe hivyo bali wadau wa mazingira wa ndani na nje ya nchi pia wengi wanataka Serengeti, Ngorongoro zibakie kuwa ghali ili kuzinusuru na cheap mass tourism ambapo huaribu Mazingira na hifadhi!

Leo hii kwa mfano Kenya, Masai Mara imekwisha na imeharibiwa kabisa kwa sababu ya cheap mass tourism hata kuna kipindi wanyama waligoma kwenda huko upande wa Kenya, hivyo sisi TanZania tunataka watalii na kufanya utalii lkn ambao ni endelevu na kuwa klk kupata mamilioni ya Watalii halafu baada ya miaka 20 hakuna Serengeti tena, hapana!
 
Mkuu mimi Nimependa uchambuzi wako. Kuna ukweli mwingi sana.

Sikia.
Binafsi sijaelewa why India haipo katika hizo nchi zinazoongoza, lakini wahindi wanafanya vizuri ktk utalii kuliko sisi.

Nimekaa India. Wamenizungusha katika nyanja zao za utalii kwa gharama zao. Aisee jamaa noma sanaw.

Kwa takwimu zao, pale wanapopaita TAJ MAHAL, AGGRA, INDIA, kwa siku inapokea watalii 250,000.

Mtalii mmoja analipa wastani wa India rupees 700, sawa na 22,000 Tshs.
 
Kuna mambo unapswa uelewe kuhusu Utalii wetu na hili pia Raisi Maguduli ameliongelea, ni kwamba hatutaki cheap mass tourism bali tunataka watalii ambao hawataharibu Mali asili zetu, Hifadhi zetu, tunataka Serengeti ibakie kuwa Serengeti mwaka 2070 na hii ndiyo moja kati ya sababu kwa nini Utalii Tanzania siku zote ni aghali klk nchi nyingi za Kiafrika, kupanda Ml.Kili peke yake ni karibu USD 700 wkt kupanda Ml.Kenya ni USD 70, kwenda Serengeti au Ngorongoro ni aghali ukilingansiha na nchi nyingine na kuna sababu kwa nini imefanywa hivi na hili siyo kwa kwa sababu tu Serikali inataka iwe hivyo bali wadau wa mazingira wa ndani na nje ya nchi pia wengi wanataka Serengeti, Ngorongoro zibakie kuwa ghali ili kuzinusuru na cheap mass tourism ambapo huaribu Mazingira na hifadhi!

Leo hii kwa mfano Kenya, Masai Mara imekwisha na imeharibiwa kabisa kwa sababu ya cheap mass tourism hata kuna kipindi wanyama waligoma kwenda huko upande wa Kenya, hivyo sisi TanZania tunataka watalii na kufanya utalii lkn ambao ni endelevu na kuwa klk kupata mamilioni ya Watalii halafu baada ya miaka 20 hakuna Serengeti tena, hapana!

Watu werevu watafikiria zaidi ni kwa namna gani vivutio vyako vya utalii vitatumika kuvutia watalii wengi zaidi na kukupa mapato makubwa zaidi lakini bila ya kuviharibu. Kama Wamisri wameweza kuendelea kuvutia watalii wengi kwa mapiramidi ya miaka elfu nyingi, mapiramidi ambayo hata hayazaliani, itashindikana vipi kwa mbuga za wanyama zenye mimea inayomea kila siku na kwa wanyama wanaozaliana kila siku?

Mara nyingi ukishindwa kupata jibu siyo kwamba hakuna jibu bali huna uwezo wa kulifikia jibu.
 
Una mawazo mazuri lakini sijaona pale unapoleta suluhisho nini kifanyike bali umelalamika tu kama ilivyokawaida ya watanzania wengi ni hodari kwa kulalamika lkn wavivu kutoa suluhisho

Watu wana elimu za kutosha kwenye mawizara. Waende kujifunza watuletee mambo mapya.
 
Watu werevu watafikiria zaidi ni kwa namna gani vivutio vyako vya utalii vitatumika kuvutia watalii wengi zaidi na kukupa mapato makubwa zaidi lakini bila ya kuviharibu. Kama Wamisri wameweza kuendelea kuvutia watalii wengi kwa mapiramidi ya miaka elfu nyingi, mapiramidi ambayo hata hayazaliani, itashindikana vipi kwa mbuga za wanyama zenye mimea inayomea kila siku na kwa wanyama wanaozaliana kila siku?

Mara nyingi ukishindwa kupata jibu siyo kwamba hakuna jibu bali huna uwezo wa kulifikia jibu.


Nenda Masai Mara Kenya, jibu lipo kwanini tukimbilie Misri kwanza aliyekwambia kwamba mass tourism haijaharibu urithi wa Dunia huko Misri ni nani? kila siku watu wananyofoa vipande kwenye mapiramidi hata sanamu la Giza pua imenyofolewa!

Wakenya wenyewe wanakuja Serengeti kwetu kujifunza jinsi tunavyotunza urithi wetu Serengeti yetu iko intact wkt Masai Mara ambayo ni muendelezo tu Serengeti Watalii wameshaiharibu na karibia inakwisha wameshaanza kugawana mashamba ya kulimia!

Hivyo sisi kwetu tunataka watalii wa kiasi ambao hawataharibu urithi wetu hili hata Raisi alilisema na isitoshe Wazungu wenyewe kwa mfano frankfurt zoo ndiyo wanaoendesha Serengeti na ndiyo wanaokampenia pia kusiwe cheap mass tourism, na ndiyo maana mpaka leo hii holliday package ya Tanzania ni ghali ukilingfanisha na nchi nyingine na imefanywa hivyo kwa makusudi kabisa, kwanza hata hoteli tu Serengeti ilikuwa hairuhusiwi kujengwa mpaka Kikwete alivyokuja ndiyo akaruhusu Wamarekani wajenge lkn tulikuwa haturuhusu, hata Kiwanja cha ndege chenyewe kilileta kelele siyo tu ndani ya Tanzania bali hata nje ya Tanzania!
 
Mkuu mimi Nimependa uchambuzi wako. Kuna ukweli mwingi sana.

Sikia.
Binafsi sijaelewa why India haipo katika hizo nchi zinazoongoza, lakini wahindi wanafanya vizuri ktk utalii kuliko sisi.

Nimekaa India. Wamenizungusha katika nyanja zao za utalii kwa gharama zao. Aisee jamaa noma sanaw.

Kwa takwimu zao, pale wanapopaita TAJ MAHAL, AGGRA, INDIA, kwa siku inapokea watalii 250,000.

Mtalii mmoja analipa wastani wa India rupees 700, sawa na 22,000 Tshs.

Utalii wa kimataifa, mwaka 2014 uliingizia India $7.68 billion, mara 4 ya Tanzania.
 
mkuu kuhusu dhahabu kuna sehemu 99 nchini ambazo zimetema tayari. mark my word lakini zingeanza kuchimbwa wakati wa udalalishaji wa nchi yetu tungebakia na mashimo matupu. subiri time will tell when we start mining!
 
Tanzania hatuna data ya idadi ya watalii wanaotembelea nchi yetu. Sisi tunamu classify mtu anayekuja kwetu toka nchi nyingine kuwa mtalii kama tu atatembelea national parks zetu na pia awe mzungu (mzungu kwetu ina include mwarabu, mchina, mmarekana nk asiwe mweusi kama sisi).

Yaani ukitembelea mbuga za wanyama na wewe rangi yako ni mweupe ndipo tutakuhesabu mtalii.
Hii ni underestimation. Mtalii ni mgeni yo yote anayekuja kwetu toka nchi nyingine kwa madhumuni yo yote yale. Nchi nyinngine yo yote ninamaanisha hata Kenya na Burundi maana wanatuachia fedha za kigeni wakilala hata kwenye guest houses zetu, wakila chakula hata kwa mama ntilie wetu na kadhalika.

Hao wanaotembelea mbuga za wanyama ni subset tu na lazima walipe extra VAT ya kuona fisi zetu la sivyo hakuna kuona fisi wetu bure bure.
 
Back
Top Bottom