Rais, Tanzania si chochote katika utalii

Rais, Tanzania si chochote katika utalii

Msumbiji na Afrika kusini wanashirikiana bega kwa bega kwenye suala la utalii. Kuna la kujifunza hapo. Mara nyingi utaskia waziri wa utalii wa Msumbiji yupo Afrika kusini. Na pia ukiwa Msumbiji utayaona magari with South African license plates. Ni mengi unaweza ukajisahau ukadhani bado umo Afrika kusini. Hawa washirika wawili tunaona hapo kwenye takwimu wapo juu kwa Afrika. Naamini tunalo la kujifunza hasa kutoka kwa Msumbiji.
Ni kweli mkuu, hata ukiwa Namibia unaweza kufikiri uko RSA kwani wa-south na magari yenye registration number za kwao ni mengi bila mfano. Nikiwa Windhoek or Wavis Bay or swakopmund natumia RAND as if niko RSA. tunapo ongelea Regional Integration Agreement or Free Trade Agreement inatakiwa iguse sectors zote za kiuchumi tukianzia na utalii. Tatizo la viongozi wetu ni bongo lala na wababe na dharau tu....Naililia nchi yangu tz..
 
Una maana gani unaposema kodi ya VAT imeshtukizwa kwa watalii waliokwisha fanya booking?

Dunia nzima hata huko wanakotoka watalii wanajua kuwa kipindi cha bajeti ya serikali huwa yanakuweko mabadiliko mbali mbali yakiwemo ya kodi.Ni kitu kinachotarajiwa kwenye bajeti zote duniani.

Huyo aliyewafanyia booking kabla ya bajeti ilibidi awaambie wazi kuwa pesa yenu nachukua lakini siwezi kuwapa guarantee kuwa bei itakuwa ni hii sababu kutakuwa na bunge la bajeti hivyo bei zaweza badilika.

Huwezi kumwahidi mtalii kuwa bei itakuwa ni hiyo wakati hujui kwenye bajeti kuna nini.
Bajeti ikishapita unakuwa na uhakika sasa na unaweza endelea kupokea hizo pesa zao za booking.

Bajeti ya nchi sio kitu cha kushtukiza hata wao wanajua hadi miezi ya bajeti
Link UCHAMBUZI: Kodi mpya ya VAT itavuruga sekta ya Utalii

Link2. TAARIFA KWA UMMA - MALIPO YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) KATIKA SHUGHULI ZA UTALII | Ministry of Natural Resources and Tourism

Link3. Maghembe: Tanzania Haitegemei Kenya Kupanga Kodi Zake | MPEKUZI
 
Zimbabwe, daaaaaah. Najilaumu kwa nini sikulibeba lile gazeti aisee, lilionyesha Zimbabwe ilipokea Watalii laki 8+ kwa mwaka 2014. Wengi wao wanakuja kutokea Afrika Kusini na kurudi siku hiyo hiyo, ni 35% tu wanaolala kwenye hotel za pale Victoria Falls na Whange National Park.
 
Hio Vat bwana ingewekwa kwenye kila kilo ya GOLD wanayo safirisha Barrick na wenzake inge make sence sana......
Lakini ukija kwenye madini sijui Ccm wana kigugumizi gani wallah..mpaka unajiuliza kuna nini ?
Nao tungewambia unataka lipa huta tuachie Dhahabu yetu
 
Yaani nchi yetu hii watu wake ni majanga kabisa. Sasa mtu kaanza kwa kulalamika, kaandika zaidi ya maneno 10000 kukosoa na mwisho eti Rais ampe mbinu za kuongeza mapato na kuifanya nchi kivutio kikuu cha utalii. Kweli?????!!!!!!
Hivi nguvu yote hiyo aliyotumia mpaka kutafuta takwimu za nani anaongoza ktk utalii, ameshindwa kabisa kutafuta hata wazo moja la kushauri nini kifanyike??
Siku hii nchi watanzania tutaacha kulalamika na kuanza tumia akili zetu kutoa mawazo boresho hakika tutasonga mbele.
Uzi wake umelamikia kodi ya VAT kwenye utalii, maana yake anashauri kodi hiyo iondolewe. Hakuna ushauri mwingine zaidi ya huo.
 
Hauna akili....so baada ya kuambiwa haya au baada ya kusoma hayo ukaamini kuwa ndio yako sahihi.....inawezekanika kabisa akija mtu aki convince kuwa mzazi wako uliye naye siyo mzazi wako utakubali...nakushauli ubadilike..pia jifuze ku judge mambo
 
Hivi nchi hii ina wachumi katika Vyuo vyetu UDSM, MZUMBE.....IFM..

Mbona wako kimya?

Hawa Wasomi wa Tanzania ni waoga (wachumi) kwa nini wako kimya? Ushauri wao kuhusu VAT on Tourism ni nini?

Wachumi wasomi wetu, mmepigwa na butwaa gani...Mtatumbuliwa bila kosa?

Tunataka uchambuzi kutoka wachumi wa UDSM na MZumbe kuhusu VAT on tourism
 
Watanzania ni watu wenye bahati mbaya sana maana mara nyingi wanaaminishwa kuwa wao ni bora katika kila kitu. Wengi wao, kwa ujinga tu, nao wameyabeba maneno hayo na kuyaweka katika vichwa vyao.

1.Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote Duniani, ambao ni uwongo, lakini wao wanaamini

2. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa tuna gas nyingi kuliko nchi yoyote, ambao ni uwongo

3. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ina madini ya kila namna na ina madini mengi kuliko nchi yoyote Duniani/Afrika, ambao ni uwongo

4. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye amani kuliko nchi zote za Afrika, ambao ni uwongo

5. Wapo Watanzania wanoamini kuwa nchi yetu ina demokrasia, utawala wa sheria na uongozi mzuri kuliko nchi yoyote ya kiafrika, nao ni uwongo lakini wanaamini

6. Wapo Watanzania wanaoaminishwa kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana ambayo kila mwanadamu angependa kuja na kuishi, nao ni uwongo lakini wengi wanaamini hivyo

7. Wapo Watanzania wanaoamini kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi na mazingira mazuri ya utalii ambayo hayapo mahali pengine popote Duniani, ambao ni uwongo mkubwa.

Takwimu za mwaka 2014 kuhusu utalii wa kimataifa (International tourist arrivals) inaonesha kuwa hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo ilikuwa miongoni mwa nchi 10 za juu katika kutembelewa na watalii. Hii inaonesha kuwa watalii hawa wa kizungu wanapendelea zaidi kwenda kwenye mabara mengine kuliko Afrika.

In 2014, there were 1.133 billion international tourist arrivals worldwide, with a growth of 4.3% as compared to 1.087 billion in 2013.[1] The top 10 international tourism destinations in 2014 were

1. France Europe 83.7 million
2. United States North America 74.8 million
3. Spain Europe 65.0 million
4. China Asia 55.6 million
5. Italy Europe 48.6 million
6. Turkey Europe 39.8 million
7. Germany Europe 33.0 million
8. United Kingdom Europe 32.6
9. Russia Europe 29.8 million
10. Mexico North America 29.1

Katika Afrika, Tanzania haipo hata katika 10 bora

In 2014, there were over 55.7 million international tourist arrivals to Africa, the top ten African destinations were
1. Morocco 10.2 million
2. Egypt 9.6 million
3. South Africa 9.5 million
4. Tunisia 6.0 million
5. Algeria — 2.7 million
6. Mozambique — 1.8 million
7. Zimbabwe 1.8 million
8. Kenya — 1.4 million
9. Uganda — 1.2 million
10. Namibia — 1.1 million

Jambo la kusikitisha ni kwamba, nchi inayoongoza kwa kutembelewa na watalii wageni katika Afrika ambayo ni Morocco, idadi ya watalii inaowapokea ni chini ya watalii wanaotembelea nchi ya mwisho ya 10 bora ya Ulaya.

In 2014, there were over 582 million international tourist arrivals to Europe, an increase of 3.0% over 2013. In 2014, the top ten destinations were

1. France 83.7 million
2. Spain 65.0 million
3. Italy 48.6 million
4. Turkey 39.8 million
5. Germany 33.0 million
6. United Kingdom 32.6 million
7. Russia 29.8 million 28.4
8. Austria 25.2 million
9. Greece 22.0 million
10. Poland 16.0 million

Ukija kwenye mapato ya utalii, Tanzania na Afrika si lolote na si chochote. Idadi kubwa ya watalii inawianika kwa kiwango kikubwa na mapato ya utalii. Hayo maneno ya kusema kuwa unaweza kuwa na watalii wachache halafu mapato yakawa makubwa ni ndoto za alinacha zinazootwa na maprofesa wa Tanzania pekee.

International tourism receipts grew to US$1,245 billion in 2014, corresponding to an increase in real terms of 3.7% from 2013.[11] The World Tourism Organization reports the following countries as the top ten tourism earners for the year 2014, with the United States by far the top earner.
1
23px-Flag_of_the_United_States.svg.png
United States North America $177.2 billion
2
23px-Flag_of_Spain.svg.png
Spain Europe $65.2 billion
3
23px-Flag_of_the_People%27s_Republic_of_China.svg.png
China Asia $56.9 billion
4
23px-Flag_of_France.svg.png
France Europe $55.4 billion
5
23px-Flag_of_Macau.svg.png
Macau Asia $50.8 billion
6
23px-Flag_of_Italy.svg.png
Italy Europe $45.5 billion
7
23px-Flag_of_the_United_Kingdom.svg.png
United Kingdom Europe $45.3 billion
8
23px-Flag_of_Germany.svg.png
Germany Europe $43.3 billion
9
23px-Flag_of_Thailand.svg.png
Thailand Asia $38.4 billion
10
23px-Flag_of_Hong_Kong.svg.png
Hong Kong Asia $38.4 billion

Kwa mapato ya utalii wa kimataifa katika Afrika, nchi inayoongoza ni Afrika Kusini ($9.4 billion) ikifuatiwa na Misri ($7.2 billion), Morrocco ($7.1 billion) na Tunisia ($2.3 bilion). Kwa ujumla yule anayeongoza kwa mapato ya utalii katika Afrika hayupo katika 10 bora za Dunia, na ni chini ya mapato ya nchi ya mwisho ya 10 bora katika mabara mengine.

Mapato ya utalii ya Tanzania kwa mwaka 2014 yalikuwa $1.95 billion, chini kuliko mapato ya Singapore ($19.20 billion), Turkey ($37.37 billion), Qatar (10.58 billion) au Misri ($7.21 billion). Singapore, Turkey, Qatar na Misri hawana twiga wala tembo lakini wanatuzidi kwa idadi ya watalii na kimapato mara dufu.

Profesa Maghembe, Rais wetu na Watanzania, wanatakiwa kufahamu kuwa vivutio vya utalii ni zaidi ya idadi ya tembo, fisi, twiga, pundamilia na ngiri tulio nao. Utalii mkubwa ni akili, yaani unaweza kufanya nini kwa kutegemea mazingira yako ili watu wa mataifa mengine waje kushuhudia na kustarehe katika mazingira yako.

Watanzania, kwa ujinga wetu, tunaamini kuwa kwa sababu tu tuna nyumbu wengi, twiga na tembo basi watu wengi, Dunia nzima wanahangaika ili waje watazame sura ya twiga. Watalii hawana haja na sura ya pundamilia wala mbwa mwitu bali wanataka kuona mazingira ya kuvutia yaliyo tofauti na mahali pengine, na sisi tunaweza kuwatumia wanyama hao kuweza kuyafanya mazingira yetu kuwa ya kuvutia zaidi kuliko Misri ambako mapiramidi na chuo kikuu cha kwanza cha Alexandria, vimetosha kuizidi Tanzania kimapato.

Ushauri wangu kwa Rais, fukuza kazi prof. Maghembe maana amekupotosha kwa kueleza kuwa hakuna uhusiano wa mapato katika utalii na idadi ya watalii. Waziri unayetakiwa kuwa naye ni yule ambaye ataihakikishia Tanzania inapata ongezeko kubwa la watalii na siyo upungufu wa watalii. Bila ya kujali kama ongezeko la idadi ya utalii na mapato ya utalii vitategemea kupungua kwa kodi au kuondoa baadhi ya kodi, au kuongeza mbinu za kujitangaza au kuboresha miundombinu na huduma za kitalii, ukweli ni kwamba tunahitaji ongezeko la idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii ambavyo vinaenda sambamba hata kama siyo kwa uwiano 1:1

Rais Magufuli hatutakuelewa kama pamoja na vyote tulivyo navyo, lakini mapato ya utalii yataendelea kuwa chini kuliko ya Afrika Kusini, Misri, Morocco, Tunisia na Kenya, huku wewe mwenyewe ukisema tuna vivutio vingi vya utalii. Tuna vivutio vya utalii visivyovutia watalii.

Mheshimiwa Rais, hotuba zako za mara kwa mara za kuelezwa nchi hii imeibiwa sana tumekwishazisikia kiasi cha kutosha, sasa tunahitaji kusikia kutoka kwako juu ya mbinu za kuongeza mapato ya utalii (siyo kodi za utalii bali mapato), mbinu za kuongeza mauzo ya mazao yetu nje ya nchi, mkakati wa kujenga uchumi wa viwanda, na namna rasilimali nyingine kama gas na madini zinavyoweza kubadilishwa kuwa mapato ya wananchi na Taifa. Mheshimiwa Rais tunataka mbinu na mikakati ya kuongeza mapato ya Watanzania.

Sisi wengine daima tutazidi kueleza pale tunapoona mbinu siyo sahihi. Tunaamini una dhamira njema lakini tuna mashaka makubwa katika mbinu.

Binadamu tuna miaka michache Duniani, hatuna muda wa kufanya majaribio bali tunatakiwa kuenenda kwa namna na mbinu zilizosahihi katika kuibadilisha nchi hii iliyo maskini kupindukia lakini iliyo na fursa nyingi zilizofunikwa. Fursa ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kitalii ni kubwa sana lakini hatuna watu wa kuweza kufungua fursa hizo ili jamii iweze kuziona kwa sababu waliopewa mamlaka ya kuzifunua kwa umma wanafanya kila mbinu ya kuzifunika ili wananchi wasizione na wala wasizifaidi.
kwakweli tunadanganywa sana
 
Back
Top Bottom