Nipe Maji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 335
- 190
Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO), Ndg. Geofrey Kiliba, ametoa wito kwa wanafunzi wa vyuo na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanaendeleza amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza leo Aprili 13, 2025 jijini Dodoma katika ziara yake ya kukutana na viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu nchini, Kiliba amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda misingi ya utulivu ambayo imeijengea taifa heshima na mshikamano wa kipekee.
Pia soma Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amewahimiza viongozi wa wanafunzi kuwa mabalozi wa amani na kuendelea kuelimisha wenzao kuhusu umuhimu wa kushiriki mchakato wa uchaguzi kwa njia ya kistaarabu na yenye kujenga taifa.
Ziara hiyo ya Kiliba inalenga kuimarisha mshikamano baina ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini, pamoja na kujadili nafasi yao katika kulinda amani, mshikamano na maendeleo ya taifa hasa katika kipindi hiki nyeti cha kisiasa.