Rais SIRLEAF kutua TANZANIA...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Rais wa Liberia,Mwanamama Hellen Johnson Sirleaf,atatua Tanzania siku ya Jumatano ijayo tarehe 18/7/2012 kuitikia mwaliko wa Wanawake wa UDSM.Amealikwa pia na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho,Dr.Asha-Rose Migiro.Dr.Migiro anaoonekana kujipanga kisiasa katika ziara hii.Anataka kuwaaminisha watanzania kuwa wanawake wanaweza.

Nyaraka zinaonesha kuwa safari ya Rais huyo itaratibiwa na Wanawake wa UDSM,na si Serikali. Hatahivyo,Itifaki itazingatiwa. Rais Sirleaf ni mmoja kati ya Marais wawili wa kike Barani Afrika.Mwingine ni Rais Joyce Banda wa Malawi.Ni mwendo wa kinyonga wa Dr.Migiro?
 

Attachments

  • 220px-Ellen_Johnson-Sirleaf,_July_2012.jpg
    220px-Ellen_Johnson-Sirleaf,_July_2012.jpg
    16.3 KB · Views: 52
migiro hata afanyeje ..hawezi kuwa rais wa nchi..huyu si ndio katimuliwa ki-utu uzima huko UN!!!!? muacheni apake rangi upepo...
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kumbukeni tuna kazi ya kuandika katiba 2 kwa sasa, Wazanzibar wanasema wanataka serikali ya tanganyika iwepo ndiyo tujadili muungano.Asha Rose sijaelewa anagombea Tanganyika au ile serikali ya muungano??? kama ni ya tanganyika hapo asahau labda ile ya muungano sijajua itaitwaje!!!!!!!!!!!!!!!!! hapo patamu wajameni
 
Anataka kuwa rais wa nchi ipi? maana mi najua kuna nchi 3
1.Tanganyika
2.Zanzibar
3.Tanzania
 
labda awe rais wa mumewake na watoto siyo tanzania wala tanganyika eidha akubali kuvua gamba na kuvaa gwanda ili sifa yake ionake kudogo
 
Mmh hakuna muda naogopa kama tukitembelewa na RAIS mwanamke sababu lazima atongozwe chezea sisi wakwere wewe.
 
Huyu mama aelewe kamba tangu aondoke ni mda wa miaka mitano, amekuta siasa za Tanzania zimebadilika sana siyo vile alivyoacha sasa siasa ni full kuchafuana, atangaze nia ya kuingia kwenye kinyang`anyilo chochote kiwe cha Ubunge au URAISI aone atakovyochafuliwa . Amwulize mwenzie Anna Abdalla kwenye kampeni za temeke alivyokutana na shehe Mtopea alitajiwa wanaume zake wote aliozaa nao ,Ana ABDALA alipotea hakurudi tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom