HeartFelt Story: Awabaka na kuwaambukiza UKIMWI Watoto Yatima 35

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,349
2,000
Source: ProPublica

Dunia katili! Tafsiri ya msemo huu, unaweza kuipata kupitia mkasa huu wa kusikitisha, unaomhusu Justine Macintosh aliyewabaka na kuwaambukiza Virusi vya Ukimwi watoto zaidi ya 35 waliokuwa wakilelewa katika kituo cha More Than Me.

Shamrashamra zinasikika katikatika ya Jiji la Monrovia, Liberia, nyimbo mbalimbali zinasikika, muziki unapigwa na kila mmoja anaonesha kuwa na furaha! Ni sherehe za uzinduzi wa Kituo cha Kusaidia Wasichana Walioathiriwa na Vita, cha More Than Me, kilichoanziwa na mwanadada wa Kimarekani, Katie Meyler.

Kutokana na uzito wa tukio lenyewe, Liberia ikiwa imeathirika sana na vita ya wenyewe kwa wenyewe, mgeni rasmi katika tukio hilo ni mheshimiwa rais, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.

Jengo ambalo sasa limekarabatiwa na kuwa jipya kabisa, ambalo ndiyo linalozinduliwa siku hii, ni lile ambalo miezi michache iliyopita, Rais Sirleaf, alimkabidhi Katie Meyler baada ya kufurahishwa na jitihada zake za kuwasaidia wasichana walioathirika na vita.

Aliamua kumkabidhi jengo hilo, ili aweze kutanua shughuli zake zaidi, aweze kuwasaidia wasichana wengi zaidi kutokana na athari za kivita. Ikumbukwe kwamba, katika mazingira ya vita, wanawake na watoto ndiyo kundi linaloathirika zaidi kutokana na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na askari, hasa waasi wanapokuwa mitaani.

Athari kubwa iliyokuwa imewakumba wanawake wa Liberia, hasa wasichana wadogo, ilikuwa ni ubakaji uliokithiri. Wasichana wadogo mpaka wenye umri wa chini ya miaka kumi, walikuwa wakibakwa kila kukicha kwenye vichochoro vya Monroviana kwenye miji mingine ya Liberia.

Hata baada ya vita kuisha, idadi ya wasichana wadogo waliokuwa wameathirika kwa ubakaji ilizidi kuongezeka, wengine wakaamua kujitoa fahamu na kujiingiza moja kwa moja kwenye biashara ya ukahaba baada ya kuwa wameshabakwa sana na waasi.

mjhousefb-720_477-1024a8.jpg

Macintosh, mwanaume anayetuhumiwa kwa ukatili huo.

Haikuwa kazi nyepesi kuwasaidia wasichana hawa walioathiriwa vibaya na vitendo vya uibakaji, wakaweza kusimama tena, wakarudi shule na kuendelea kuzifukuzia ndoto zao. Hii ndiyo kazi aliyokuwa anaifanya Katie Myler na kuzigusa hisia za watu wengi na ndiyo maana hata siku hiyo ya uzinduzi, mheshimiwa rais alikuwa mgeni rasmi.

Kuweka mambo sawa, ni kwamba kituo hiki kilikuwa kimejengwa maalum kwa ajili ya kutoa hifadhi kwa wasichana walioathirika na vitendo vya ubakaji, wasiendelee kubakwa tena, na wale ambao hawajawahi kubakwa lakini kutokana na athari za vita, wapo kwenye hatari ya kufanyiwa vitendo vya ubakaji, wabaki kuwa salama.

More Than Me Academy iligeuka na kuwa kimbilio, wasichana wengi waliokuwa wakifanya biashara ya ukahaba mitaani, wakakusanywa na kuanza kupatiwa masomo na msaada wa kisaikolojia kusahau ukatili waliofanyiwa.

Kituo hiki kilikuwa kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kurejesha furaha kwenye mioyo ya watoto wa kike Liberia, familia nyingi huko mitaani zilikuwa zikijivunia watoto wao kurudishwa shuleni, Katie alionekana kuwa kuwa ‘mungu mtu’ kwa watu wengi nchini Liberia.

Hiyo ndiyo sababu kwa hiyo tukio lililokuwa linafanyika leo, la kuzinduliwa kwa jengo jipya la kituo hicho, lenye nafasi kubwa zaidi, likiwa na uwezo wa kuchukua watoto wengi zaidi, ilikuwa ni zaidi ya mapinduzi katika harakati za kumsaidia mtoto wa kike mweusi.
Who-Katie-Meyler.jpg

Katie Myler akiwa na baadhi ya watoto aliokuwa akiwahudumia.

Hata hivyo, ndani ya mioyo ya watoto wengi waliokuwa wakilelewa kwenye kituo hiki, siri kubwa imejificha, ndani kabisa ya mioyo yao. Hakuna ambaye yupo tayari kuitoa siri hii, kwa sababu wameshatishiwa kwamba yeyote atakayethubutu kusema chochote, atafukuzwa chuoni hapo na kukosa fursa ya kuendelea na masomo.

Ni nani aliyekuwa tayari kurudi mitaani, kwenda kuteseka tena? Hakuna, kwa hiyo siri ikaendelea kuwa sirini. Siri hii inamhusu mwanaume ambaye amekuwa bega kwa bega na Katie Meyler kuanzia wakati wanaanzisha kituo cha kuwasaidia watoto hao.

Amekuwa si tu mtu muhimu kwa Katie, bali muhimu kwa kila msichana mdogo kituoni hapo, yeye ndiye huongoza misafara ya kwenda kuwatafuta watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, yeye ndiye anayejua madanguro wanakopatikana watoto wadogo wanaojiuza na hakika amekuwa mtu muhimu sana.

Jina lake anaitwa Johnson Macintosh, mwanzilishi mwenza wa Kituo cha More Than Me Academy na siku hiyo ya uzinduzi, alikuwa amekaa jirani kabisa na Katie, tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake. Tabasamu hili lilikuwa limeficha dhambi kubwa mno, lilikuwa ni tabasamu la muuaji.

Macintosh, kihistoria amewahi kupigana sana vita nchini Liberia. Mwenyewe anaeleza kwamba alikamatwa akiwa kijana mdogo, akafundishwa kutumia bunduki, akafundishwa kuvuta bangi na baadaye, akafundishwa kuua kwa kutumia bunduki.

Baada ya vita kuisha, aliamua kubadilika na kuwa mtu mwema kwa jamii, na kila aliyekuwa akimfahamu, alikuwa akimsifu kwamba kweli amebadilika na kuwa raia mwema. Hata alipofanikiwa kumleta Katie eneo hilo, na kumtambulisha kwa wenyeweji, sifa zake zilizidi kuongezeka, akawa anaheshimika na kila mtu aliyekuwa akimuona.

Hata hivyo, nyuma ya pazia, kulikuwa na ushetani mkubwa uliokuwa ukiendelea kituoni hapo, ukimhusisha Macintosh na wasichana waliokuwa wakilelewa kwenye kituo hicho. Mwanaume huyu, alikuwa akiwabaka kwa zamuzamu wasichana hao wadogo, wengi wakiwa na umri wa chini ya miaka kumi na mbili.

Alikuwa akiwapa fedha, kiasi cha wastani wa dola moja ya Kimarekani, huku akiwatishia kwamba yeyote ambaye atasema, basi atahakikisha anamfukuza kituoni hapo, au hata kumuua, huku akijitapa kwamba akiwa vitani ameshaua watu wengi kwa hiyo haoni hatari yoyote kumuua mtu yeyote atakayesema alichokuwa anawafanyia.

Alikuwa akiwabaka kuanzia kwenye mabweni ndani ya kituo hicho, kwenye madarasa, stoo na kila mahali palipokuwa na ukimya, hakuishia hapo, wengine alikuwa akienda kuwabaka nyumbani kwake, ambako mkewe alishamkimbia kutokana na ugomvi uliokuwa umeibuka kati yao, chanzo kikiwa ni tabia za Macintosh.

Yote tisa, kumi ni kwamba Macintosh huyu, pia amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Katie, mwanzilishi wa kituo hicho ingawa haikuwa ikifahamika ni kitu gani kilichokuwa kimetokea mpaka wakaachana.

Uhusiano wake wa kimapenzi na Katie, ni sababu nyingine iliyofanya watu waliokuwa wanajua kilichokuwa kinaendelea kati ya Macintosh na watoto hao, washindwe cha kufanya kwa sababu isingekuwa rahisi Katie kuwaamini ambacho wangeelezwa.

Jinsi siri hiyo ilivyokuja kufichuka, ni simulizi nyingine ya kusisimua mno, lakini kama wahenga walivyosema, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, hatimaye ukweli ulikuja kufahamika.

Mtu wa kwanza kugundua mchezo huo, alikuwa ni nesi wa kituo hicho, ambaye wasichana hao wadogo walikuwa wakienda kutibiwa naye kila walipokuwa wakiugua.
KY64GQHYEZAY3BCW2K373YGQY4.jpg

“Nilishangazwa baada ya binti mmoja kuja hapa akilalamikia maumivu makali ya tumbo, baada ya kumpima niligundua kwamba alikuwa na maambukizi mapya ya ugonjwa wa zinaa. Nilishtuka sana kwa sababu kwa umri wake, alikuwa mdogo sana na usingeweza kuamini kwamba anashiriki katika ngono.

“Baada ya kumbana sana, alinieleza ukweli kwamba Macintosh amekuwa akimuingilia mara kwa mara, kweli nilipomchunguza sehemu zake za siri, alikuwa ameharibiwa vibaya. Ilibidi niwaite wenzangu na tukaanza kushauriana nini cha kufanya, lakini kabla hatujapata majibu, kulitokea tena kesi kama ile ya kwanza.

“Wasichana wengine kadhaa, walikuja wakiwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na baada ya kuwabana, kila mmoja kwa wakati wake, wote walikuwa wakieleza kwamba aliyekuwa akiwaingilia ni Macintosh na wote walikuwa wameharibika vibaya sehemu zao za siri na mmoja kati yao, alikuwa mjamzito,” anasimulia Iris Martor, nesi aliyebumburua ishu nzima na kuongeza:

“Ni katika kipindi hicho, Macintosh pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Katie, bosi wetu kwa hiyo kila mmoja aliogopa hata kumfuata na kumweleza chochote kwa sababu tunajua jinsi mapenzi yalivyo na nguvu, hakuna aliyekuwa tayari kupoteza kazi yake.

“Kwa kuwa kituoni hapo kulikuwa na walimu na wafanyakazi wengine wa Kizungu, ndugu zake Katie waliotoka Marekani, tuliamua kuwatumia hao kufikisha ujumbe lakini pia nao walikuwa wagumu kuchukua hatua, idadi kubwa ya wasichana wakawa wanaendelea kukutwa na magonjwa ya zinaa na wengine kupata ujauzito. Hali ilikuwa inatisha, sisi kama wazazi tuliumia sana na tukawa tunajiapiza kwamba ipo siku tutavunja ukimya.

“Baadaye Macintosh na Katie walitengana, tukaona huo ndiyo wakati mzuri wa kutoa dukuduku kwenye mioyo yetu, tukawapa taarifa polisi wa Liberia.”
download - Copy.jpg

Baada ya polisi kupewa taarifa, walifika shuleni hapo na kumkamata Macintosh na hapo ndipo mambo mengi zaidi maovu aliyokuwa akiyafanya yalipofichuka.

Makachero wa polisi waliueleza uongozi, akiwemo Katie mwenyewe kuhusu kilichosababisha Macintosh akamatwe, akapigwa na butwaa akiwa ni kama haamini, huku akiwalaumu sana wafanyakazi wenzake kwa kumficha kuhusu ushetani uliokuwa ukifanywa na Macintosh.

Wasichana wote waliokuwa wakilelewa shuleni hapo, walianza kuhojiwa faragha, mmoja baada ya mwingine na matokeo yalimshangaza kila mmoja. Walionusurika na ushetani wa Macintosh, walikuwa ni wale wadogo zaidi, wenye chini ya miaka nane ambao nao walitoa ushuhuda wa jinsi mwanaume huyo alivyokuwa akiwachezea sehemu zao za siri na kuwasifia jinsi walivyo wazuri.

Wengine wote waliokuwa wakionekana wakubwawakubwa, walikuwa wamebakwa kwa nyakati tofauti na Macintosh, wengine mara moja au mara chache, huku wengine akiwageuza kama wake zake kwa kuwaingilia mara kwa mara kila alipokuwa akijisikia.

Kibaya zaidi ni kwamba alikuwa hachagui sehemu za kufanyia ukatili huo, wapo aliowabaka madarasani juu ya madawati, kwenye vyoo vya shule, kwenye ofisi za walimu, hasa nyakati za jioni na wengine alikuwa akienda kuwafanyia mchezo huo nyumbani kwake na ilikuja kubainika kwamba mkewe alikuwa akijua mchezo huo ndiyo maana aliamua kufungasha kila kilichokuwa chake na kurudi kwao, akiogopa kuwa sehemu ya ushetani huo.

Gazeti la Pro-Publica ndiyo lililokuwa la kwanza kufichua uozo huo kwenye jamii baada ya vyombo vya habari vya Liberia, kuonekana kama kuliogopa suala hilo kwa lengo la kulinda heshima ya Katie Myler na kituo hicho kwa sababu ukiachilia mbali dosari hiyo, kilikuwa kikifanya kazi kubwa ya kuwasaidia wasichana walioathirika na vita, lakini pia kilikuwa kikiungwa mkono na rais wa nchi hiyo, mwanamama Ellen Johnson Sirleaf.

Ripoti nyingine kutoka Pro- Publica zinaonesha kwamba Katie, baada ya kugundua tatizo hilo, alijaribu ‘kuwanunua’ waandishi wa habari ili wasifukue zaidi kilichokuwa kimetokea, zaidi wamhoji yeye kuhusu jinsi alivyolipokea tatizo hilo na hatua anazopanga kuzichukua ili kuhakikisha halijirudii tena kwa lengo la kujisafisha.

Baada ya Pro-Publica kuitoa habari hiyo katika mfumo wa ‘documentary’ kupitia mtandao wao, likiwa limechimba sana na kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho, akiwemo nesi aliyekuwa mstari wa mbele kufichua suala hilo, wanafunzi waliotendewa ukatili huo, wazazi wa watoto waliothirika na mke wa Macintosh, taharuki kubwa iliibuka.

Dunia nzima ni kama ilitingishika, kila aliyeiona alilaani vikali kilichofanywa na Macintosh na kuilaani serikali kwa kuchelewa kuchukua hatua, huku pia Katie akishutumiwa kwa uzembe mkubwa alioufanya, ikiwemo kuchanganya mapenzi na kazi na kuwaamini watu asiowajua pamoja na kutaka kulifukia suala hilo.

Wafadhili wakubwa wa More Than Me Foundation, waliokuwa sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo mfuko wa Gates and Melinda Foundation, Moondance Foundation, JP Morgan Chase, The Novo Foundation, The U.S. state department, US-AID, Global Giving na kadhalika, walitangaza kusitisha kuisaidia More Than Me mpaka watakapopewa ufafanuzi wa nini hasa kilichotokea.

Inaelezwa kwamba wafanyakazi karibu wote wa kituo hicho, hasa wale waliokuwa wakitokea nchini Marekani, walijiuzulu nafasi zao na kurejea kwao, na kumuacha Katie peke yake, ambaye muda mwingi alikuwa akilia huku akishikilia msimamo wake kwamba lengo lake la kuanzisha kituo hicho halikuwa baya na kwamba atasimama imara mpaka mwisho kuwasaidia wote waliodhalilishwa na kunyanyaswa na Macintosh.

Gumzo liliendelea kuwa kubwa, shinikizo la Macintosh kupewa adhabu kali likawa kubwa lakini akiwa gerezani, kabla hata kesi yake haijatolewa hukumu, Macintosh alifariki kwa HIV/AIDS, huku wafungwa wenzake wakieleza kwamba katika siku za mwisho za uhai wake, alidhoofika mno na kubaki mifupa mitupu.

Hofu ikazuka upya, ikabidi wasichana wote walioripotiwa kubakwa na Macintosh wakapimwe Ukimwi na habari ya kusikitisha ni kwamba, 35 kati yao, walikutwa wakiwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Mpaka hapo, Katie alishindwa kuendelea na kazi yake kwa sababu sasa tatizo halikuwa kubakwa pekee, bali pia kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa watoto ambao yeye ndiye aliyepewa dhamana ya kuwalinda. Hata hivyo, baadaye alirejea tena kuendelea na kazi yake, ikiwa ni pamoja na kuwasimamia wale wote waliopata madhara huku akiwa pia na timu ya wataalamu kuhakikisha kilichotokea hakijirudii tena.

Hashpower7113.
 
hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
42,730
2,000
Serikali na jamii kwa ujumla wote walikosea kumuamini huyo Macintosh "

Kwa sababu history yake ya maisha ya nyuma inaonyesha jinsi ambavyo alivyo kuwa ni katili hivyo basi ni wazi kwamba alikuwa ameathirika ki psychology na aina ya maisha ambayo aliyapitia .

Ni ngumu Sana kwa mtu aliyepitia maisha kama yake " kuja kubadilika kabisa " na kuwa na mfano bora wa kuigwa .. hata ajitahidi kubadilika vipi ..lazima maisha yake yatakuwa na upande wa pili wa sarafu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu, ndiyo maana watu wakitoka vitani lazima wapewe kwanza counselling
 
Mao Tanzania

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
211
250
Source: ProPublica

Dunia katili! Tafsiri ya msemo huu, unaweza kuipata kupitia mkasa huu wa kusikitisha, unaomhusu Justine Macintosh aliyewabaka na kuwaambukiza Virusi vya Ukimwi watoto zaidi ya 35 waliokuwa wakilelewa katika kituo cha More Than Me.

Shamrashamra zinasikika katikatika ya Jiji la Monrovia, Liberia, nyimbo mbalimbali zinasikika, muziki unapigwa na kila mmoja anaonesha kuwa na furaha! Ni sherehe za uzinduzi wa Kituo cha Kusaidia Wasichana Walioathiriwa na Vita, cha More Than Me, kilichoanziwa na mwanadada wa Kimarekani, Katie Meyler.

Kutokana na uzito wa tukio lenyewe, Liberia ikiwa imeathirika sana na vita ya wenyewe kwa wenyewe, mgeni rasmi katika tukio hilo ni mheshimiwa rais, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia.

Jengo ambalo sasa limekarabatiwa na kuwa jipya kabisa, ambalo ndiyo linalozinduliwa siku hii, ni lile ambalo miezi michache iliyopita, Rais Sirleaf, alimkabidhi Katie Meyler baada ya kufurahishwa na jitihada zake za kuwasaidia wasichana walioathirika na vita.

Aliamua kumkabidhi jengo hilo, ili aweze kutanua shughuli zake zaidi, aweze kuwasaidia wasichana wengi zaidi kutokana na athari za kivita. Ikumbukwe kwamba, katika mazingira ya vita, wanawake na watoto ndiyo kundi linaloathirika zaidi kutokana na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na askari, hasa waasi wanapokuwa mitaani.

Athari kubwa iliyokuwa imewakumba wanawake wa Liberia, hasa wasichana wadogo, ilikuwa ni ubakaji uliokithiri. Wasichana wadogo mpaka wenye umri wa chini ya miaka kumi, walikuwa wakibakwa kila kukicha kwenye vichochoro vya Monroviana kwenye miji mingine ya Liberia.

Hata baada ya vita kuisha, idadi ya wasichana wadogo waliokuwa wameathirika kwa ubakaji ilizidi kuongezeka, wengine wakaamua kujitoa fahamu na kujiingiza moja kwa moja kwenye biashara ya ukahaba baada ya kuwa wameshabakwa sana na waasi.

View attachment 1048200
Macintosh, mwanaume anayetuhumiwa kwa ukatili huo.

Haikuwa kazi nyepesi kuwasaidia wasichana hawa walioathiriwa vibaya na vitendo vya uibakaji, wakaweza kusimama tena, wakarudi shule na kuendelea kuzifukuzia ndoto zao. Hii ndiyo kazi aliyokuwa anaifanya Katie Myler na kuzigusa hisia za watu wengi na ndiyo maana hata siku hiyo ya uzinduzi, mheshimiwa rais alikuwa mgeni rasmi.

Kuweka mambo sawa, ni kwamba kituo hiki kilikuwa kimejengwa maalum kwa ajili ya kutoa hifadhi kwa wasichana walioathirika na vitendo vya ubakaji, wasiendelee kubakwa tena, na wale ambao hawajawahi kubakwa lakini kutokana na athari za vita, wapo kwenye hatari ya kufanyiwa vitendo vya ubakaji, wabaki kuwa salama.

More Than Me Academy iligeuka na kuwa kimbilio, wasichana wengi waliokuwa wakifanya biashara ya ukahaba mitaani, wakakusanywa na kuanza kupatiwa masomo na msaada wa kisaikolojia kusahau ukatili waliofanyiwa.

Kituo hiki kilikuwa kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kurejesha furaha kwenye mioyo ya watoto wa kike Liberia, familia nyingi huko mitaani zilikuwa zikijivunia watoto wao kurudishwa shuleni, Katie alionekana kuwa kuwa ‘mungu mtu’ kwa watu wengi nchini Liberia.

Hiyo ndiyo sababu kwa hiyo tukio lililokuwa linafanyika leo, la kuzinduliwa kwa jengo jipya la kituo hicho, lenye nafasi kubwa zaidi, likiwa na uwezo wa kuchukua watoto wengi zaidi, ilikuwa ni zaidi ya mapinduzi katika harakati za kumsaidia mtoto wa kike mweusi. View attachment 1048202
Katie Myler akiwa na baadhi ya watoto aliokuwa akiwahudumia.

Hata hivyo, ndani ya mioyo ya watoto wengi waliokuwa wakilelewa kwenye kituo hiki, siri kubwa imejificha, ndani kabisa ya mioyo yao. Hakuna ambaye yupo tayari kuitoa siri hii, kwa sababu wameshatishiwa kwamba yeyote atakayethubutu kusema chochote, atafukuzwa chuoni hapo na kukosa fursa ya kuendelea na masomo.

Ni nani aliyekuwa tayari kurudi mitaani, kwenda kuteseka tena? Hakuna, kwa hiyo siri ikaendelea kuwa sirini. Siri hii inamhusu mwanaume ambaye amekuwa bega kwa bega na Katie Meyler kuanzia wakati wanaanzisha kituo cha kuwasaidia watoto hao.

Amekuwa si tu mtu muhimu kwa Katie, bali muhimu kwa kila msichana mdogo kituoni hapo, yeye ndiye huongoza misafara ya kwenda kuwatafuta watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, yeye ndiye anayejua madanguro wanakopatikana watoto wadogo wanaojiuza na hakika amekuwa mtu muhimu sana.

Jina lake anaitwa Johnson Macintosh, mwanzilishi mwenza wa Kituo cha More Than Me Academy na siku hiyo ya uzinduzi, alikuwa amekaa jirani kabisa na Katie, tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake. Tabasamu hili lilikuwa limeficha dhambi kubwa mno, lilikuwa ni tabasamu la muuaji.

Macintosh, kihistoria amewahi kupigana sana vita nchini Liberia. Mwenyewe anaeleza kwamba alikamatwa akiwa kijana mdogo, akafundishwa kutumia bunduki, akafundishwa kuvuta bangi na baadaye, akafundishwa kuua kwa kutumia bunduki.

Baada ya vita kuisha, aliamua kubadilika na kuwa mtu mwema kwa jamii, na kila aliyekuwa akimfahamu, alikuwa akimsifu kwamba kweli amebadilika na kuwa raia mwema. Hata alipofanikiwa kumleta Katie eneo hilo, na kumtambulisha kwa wenyeweji, sifa zake zilizidi kuongezeka, akawa anaheshimika na kila mtu aliyekuwa akimuona.

Hata hivyo, nyuma ya pazia, kulikuwa na ushetani mkubwa uliokuwa ukiendelea kituoni hapo, ukimhusisha Macintosh na wasichana waliokuwa wakilelewa kwenye kituo hicho. Mwanaume huyu, alikuwa akiwabaka kwa zamuzamu wasichana hao wadogo, wengi wakiwa na umri wa chini ya miaka kumi na mbili.

Alikuwa akiwapa fedha, kiasi cha wastani wa dola moja ya Kimarekani, huku akiwatishia kwamba yeyote ambaye atasema, basi atahakikisha anamfukuza kituoni hapo, au hata kumuua, huku akijitapa kwamba akiwa vitani ameshaua watu wengi kwa hiyo haoni hatari yoyote kumuua mtu yeyote atakayesema alichokuwa anawafanyia.

Alikuwa akiwabaka kuanzia kwenye mabweni ndani ya kituo hicho, kwenye madarasa, stoo na kila mahali palipokuwa na ukimya, hakuishia hapo, wengine alikuwa akienda kuwabaka nyumbani kwake, ambako mkewe alishamkimbia kutokana na ugomvi uliokuwa umeibuka kati yao, chanzo kikiwa ni tabia za Macintosh.

Yote tisa, kumi ni kwamba Macintosh huyu, pia amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Katie, mwanzilishi wa kituo hicho ingawa haikuwa ikifahamika ni kitu gani kilichokuwa kimetokea mpaka wakaachana.

Uhusiano wake wa kimapenzi na Katie, ni sababu nyingine iliyofanya watu waliokuwa wanajua kilichokuwa kinaendelea kati ya Macintosh na watoto hao, washindwe cha kufanya kwa sababu isingekuwa rahisi Katie kuwaamini ambacho wangeelezwa.

Jinsi siri hiyo ilivyokuja kufichuka, ni simulizi nyingine ya kusisimua mno, lakini kama wahenga walivyosema, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, hatimaye ukweli ulikuja kufahamika.

Mtu wa kwanza kugundua mchezo huo, alikuwa ni nesi wa kituo hicho, ambaye wasichana hao wadogo walikuwa wakienda kutibiwa naye kila walipokuwa wakiugua.
View attachment 1048203

“Nilishangazwa baada ya binti mmoja kuja hapa akilalamikia maumivu makali ya tumbo, baada ya kumpima niligundua kwamba alikuwa na maambukizi mapya ya ugonjwa wa zinaa. Nilishtuka sana kwa sababu kwa umri wake, alikuwa mdogo sana na usingeweza kuamini kwamba anashiriki katika ngono.

“Baada ya kumbana sana, alinieleza ukweli kwamba Macintosh amekuwa akimuingilia mara kwa mara, kweli nilipomchunguza sehemu zake za siri, alikuwa ameharibiwa vibaya. Ilibidi niwaite wenzangu na tukaanza kushauriana nini cha kufanya, lakini kabla hatujapata majibu, kulitokea tena kesi kama ile ya kwanza.

“Wasichana wengine kadhaa, walikuja wakiwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na baada ya kuwabana, kila mmoja kwa wakati wake, wote walikuwa wakieleza kwamba aliyekuwa akiwaingilia ni Macintosh na wote walikuwa wameharibika vibaya sehemu zao za siri na mmoja kati yao, alikuwa mjamzito,” anasimulia Iris Martor, nesi aliyebumburua ishu nzima na kuongeza:

“Ni katika kipindi hicho, Macintosh pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Katie, bosi wetu kwa hiyo kila mmoja aliogopa hata kumfuata na kumweleza chochote kwa sababu tunajua jinsi mapenzi yalivyo na nguvu, hakuna aliyekuwa tayari kupoteza kazi yake.

“Kwa kuwa kituoni hapo kulikuwa na walimu na wafanyakazi wengine wa Kizungu, ndugu zake Katie waliotoka Marekani, tuliamua kuwatumia hao kufikisha ujumbe lakini pia nao walikuwa wagumu kuchukua hatua, idadi kubwa ya wasichana wakawa wanaendelea kukutwa na magonjwa ya zinaa na wengine kupata ujauzito. Hali ilikuwa inatisha, sisi kama wazazi tuliumia sana na tukawa tunajiapiza kwamba ipo siku tutavunja ukimya.

“Baadaye Macintosh na Katie walitengana, tukaona huo ndiyo wakati mzuri wa kutoa dukuduku kwenye mioyo yetu, tukawapa taarifa polisi wa Liberia.”
View attachment 1048204

Baada ya polisi kupewa taarifa, walifika shuleni hapo na kumkamata Macintosh na hapo ndipo mambo mengi zaidi maovu aliyokuwa akiyafanya yalipofichuka.

Makachero wa polisi waliueleza uongozi, akiwemo Katie mwenyewe kuhusu kilichosababisha Macintosh akamatwe, akapigwa na butwaa akiwa ni kama haamini, huku akiwalaumu sana wafanyakazi wenzake kwa kumficha kuhusu ushetani uliokuwa ukifanywa na Macintosh.

Wasichana wote waliokuwa wakilelewa shuleni hapo, walianza kuhojiwa faragha, mmoja baada ya mwingine na matokeo yalimshangaza kila mmoja. Walionusurika na ushetani wa Macintosh, walikuwa ni wale wadogo zaidi, wenye chini ya miaka nane ambao nao walitoa ushuhuda wa jinsi mwanaume huyo alivyokuwa akiwachezea sehemu zao za siri na kuwasifia jinsi walivyo wazuri.

Wengine wote waliokuwa wakionekana wakubwawakubwa, walikuwa wamebakwa kwa nyakati tofauti na Macintosh, wengine mara moja au mara chache, huku wengine akiwageuza kama wake zake kwa kuwaingilia mara kwa mara kila alipokuwa akijisikia.

Kibaya zaidi ni kwamba alikuwa hachagui sehemu za kufanyia ukatili huo, wapo aliowabaka madarasani juu ya madawati, kwenye vyoo vya shule, kwenye ofisi za walimu, hasa nyakati za jioni na wengine alikuwa akienda kuwafanyia mchezo huo nyumbani kwake na ilikuja kubainika kwamba mkewe alikuwa akijua mchezo huo ndiyo maana aliamua kufungasha kila kilichokuwa chake na kurudi kwao, akiogopa kuwa sehemu ya ushetani huo.

Gazeti la Pro-Publica ndiyo lililokuwa la kwanza kufichua uozo huo kwenye jamii baada ya vyombo vya habari vya Liberia, kuonekana kama kuliogopa suala hilo kwa lengo la kulinda heshima ya Katie Myler na kituo hicho kwa sababu ukiachilia mbali dosari hiyo, kilikuwa kikifanya kazi kubwa ya kuwasaidia wasichana walioathirika na vita, lakini pia kilikuwa kikiungwa mkono na rais wa nchi hiyo, mwanamama Ellen Johnson Sirleaf.

Ripoti nyingine kutoka Pro- Publica zinaonesha kwamba Katie, baada ya kugundua tatizo hilo, alijaribu ‘kuwanunua’ waandishi wa habari ili wasifukue zaidi kilichokuwa kimetokea, zaidi wamhoji yeye kuhusu jinsi alivyolipokea tatizo hilo na hatua anazopanga kuzichukua ili kuhakikisha halijirudii tena kwa lengo la kujisafisha.

Baada ya Pro-Publica kuitoa habari hiyo katika mfumo wa ‘documentary’ kupitia mtandao wao, likiwa limechimba sana na kuzungumza na wafanyakazi wa kituo hicho, akiwemo nesi aliyekuwa mstari wa mbele kufichua suala hilo, wanafunzi waliotendewa ukatili huo, wazazi wa watoto waliothirika na mke wa Macintosh, taharuki kubwa iliibuka.

Dunia nzima ni kama ilitingishika, kila aliyeiona alilaani vikali kilichofanywa na Macintosh na kuilaani serikali kwa kuchelewa kuchukua hatua, huku pia Katie akishutumiwa kwa uzembe mkubwa alioufanya, ikiwemo kuchanganya mapenzi na kazi na kuwaamini watu asiowajua pamoja na kutaka kulifukia suala hilo.

Wafadhili wakubwa wa More Than Me Foundation, waliokuwa sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo mfuko wa Gates and Melinda Foundation, Moondance Foundation, JP Morgan Chase, The Novo Foundation, The U.S. state department, US-AID, Global Giving na kadhalika, walitangaza kusitisha kuisaidia More Than Me mpaka watakapopewa ufafanuzi wa nini hasa kilichotokea.

Inaelezwa kwamba wafanyakazi karibu wote wa kituo hicho, hasa wale waliokuwa wakitokea nchini Marekani, walijiuzulu nafasi zao na kurejea kwao, na kumuacha Katie peke yake, ambaye muda mwingi alikuwa akilia huku akishikilia msimamo wake kwamba lengo lake la kuanzisha kituo hicho halikuwa baya na kwamba atasimama imara mpaka mwisho kuwasaidia wote waliodhalilishwa na kunyanyaswa na Macintosh.

Gumzo liliendelea kuwa kubwa, shinikizo la Macintosh kupewa adhabu kali likawa kubwa lakini akiwa gerezani, kabla hata kesi yake haijatolewa hukumu, Macintosh alifariki kwa HIV/AIDS, huku wafungwa wenzake wakieleza kwamba katika siku za mwisho za uhai wake, alidhoofika mno na kubaki mifupa mitupu.

Hofu ikazuka upya, ikabidi wasichana wote walioripotiwa kubakwa na Macintosh wakapimwe Ukimwi na habari ya kusikitisha ni kwamba, 35 kati yao, walikutwa wakiwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Mpaka hapo, Katie alishindwa kuendelea na kazi yake kwa sababu sasa tatizo halikuwa kubakwa pekee, bali pia kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa watoto ambao yeye ndiye aliyepewa dhamana ya kuwalinda. Hata hivyo, baadaye alirejea tena kuendelea na kazi yake, ikiwa ni pamoja na kuwasimamia wale wote waliopata madhara huku akiwa pia na timu ya wataalamu kuhakikisha kilichotokea hakijirudii tena.

Hashpower7113.
Duh
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom