VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Rais Magufuli alipeleka mbele sherehe za Uhuru na Jamhuri ya Tanganyika hapo tarehe 9/12/2015 hadi 9/12/2016. Badala yake, siku hiyo ikawa ni siku ya kazi na ikatumika kufanya usafi wa kitaifa. Tarehe 12/1/2016 ni siku ya Mapinduzi ya Zanzibar. Rais Shein wa Zanzibar, unaonaje ukafuata nyayo za Rais wa Tanzania, Dr. Magufuli?
Nawe ipeleke mbele siku ya Mapinduzi na kuifanya siku ya kazi. Halafu, siku hiyo itumike kujadili mustakabali wa Zanzibar kufuatia mkwamo wa kikatiba na kisheria baada ya kufutwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar. Siku hiyo itumike kutafuta muafaka wa kitaifa.
Ni hayo tu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam