Rais Samia weka mkazo kwenye Kilimo

Chakwale

JF-Expert Member
May 17, 2015
1,068
1,542
Serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati JPM suala la Ajira lilikuwa si kipaumbele chake.

Ndio maana katika kipindi chake chote cha miaka mitano na miezi kadhaa,kitakwimu ajira zilizotolewa ni chache mnoo ukilinganisha na idadi ya Maelfu ya vijana wanaomaliza vyuo vikuu, vyuo vya ufundi stadi/ Veta, vyuo vya ualimu nk nk.

Ukifanya ulinganisho huo kati ya ajira zilizotolewa na uhitaji unaweza sema ni kama serikali haija ajiri tu.Mbaya zaidi hata wale baadhi waliokuwa kwenye ajira kwa muda mrefu na wenye uzoefu waliondolewa kwa vigezo mbalimbali ikiwemo vyeti feki,Elimu ndogo nakadhalika.

Ukichukua hayo mambo mawili pekee ya serikali kutoajiri katika kipindi cha miaka mitano na kufukuza wale waliokuwa kazini wakifanya kazi kwa kigezo cha vyeti feki utaona ni namna gani mtaani kumejaa idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Hata hili ongezeko la Machinga tunaoona mtaani ni matokeo ya vijana wasomi walioamua kujitafutia ridhiki kwa njia ya Umachinga baada ya kukosa ajira rasmi zile walizosomea.

Kwa muktadha huo basi, kama Nchi tunazalisha kundi kubwa LA vijana wasio na kazi kitu ambacho ni hatari kwa ustawi mzuri wa taifa.Mana hawa ni rahisi kujiingiza ktk makundi ya kihalifu ikiwemo wizi,unyang'anyi,ujambazi,Ukahaba maarufu kama Dadapoa.

Hawa pia ni rahisi kushawishiwa na Wanasiasa wenye tamaa za madaraka kwa kutumiwa kama mtaji wa kisiasa na kuiingiza nchi kwenye machafuko kama tulivyoona ARAB SPRING kwenye nchi kama Tunisia,Misri,Algeria na Libya.

Kwa vile sasa Nchi inapitia kipindi kigumu cha mdororo wa uchumi uliosababishwa na janga LA Uviko19 na miradi kubwa ya kimkakati ikiwemo ya SGR na Bwawa LA Mwalimu Nyerere nk hivyo mzuunguko wa fedha kuwa Mdogo na kushindwa kutoa ajira kwa vijana wote wanaomaliza vyuoni na mashuleni.

Nashauri Serikali ijikite zaidi katika Kilimo cha kibiashara na Chakula,kwa kuwawezesha Vijana mitaji ya Kilimo wakiwa ktk makundi.Kwa mfano Rais Samia unaweza kuwaagiza wakuu wote wa mikoa Nchini kuwa kila mkuu wa mkoa awe na idadi ya vijana elfu moja wasio na ajira na walio tayari kwa kilimo ambao watawaweka kwenye makambi ya mikoa yao na serikali iwape vitendea kazi kama trekta, mbegu, mbolea,nk nk.

Hii Nchi yetu ina Eneo kubwa la Ardhi tupu ambalo halitumiki, huku Vijana wengi wakiwa hawana ajira na tuna nchi nyingi zinatuzunguka ambazo zina uhaba mkubwa wa Chakula ikiwemo Kenya, Somalia, Sudani, Comoro na nyinginezo kutaja kwa uchache wake ambazo tukizalisha Chakula cha kutosha tutawauzia wao.

Nchi yetu imezungukwa na Bahari,MaZiwa,mito na mabwawa ambayo muda wote maji yanapatikana.Tutakuwa tunamlaumu Mungu kila siku kuwa hatuna ajira ili hali tumezungukwa rasilimali.

Hizi pesa tunazotumia magari ya kifahari MaV8 ya Polepole tungezitumia ktk kununulia matrekta na magali ya kuchimbia visima,mana V8 moja unapata trekta si chini ya NNE or tano.

Kilimo hiki kitasimamiwa na wakuu wa mikoa na wilaya na mazao yatakayozalishwa yatategemea Jiografia ya kila mkoa na ustawi wake kwa kutegemea pia aina ya udongo na aina ya zao linalokubali mkoa husika.Serikali itanunua mazao yatakayopatikana baada ya kuwakopesha mitaji ya kulimia Vijana na yenyewe kwenda kuuza kwa bei kubwa zaidi nje ya Nchi yetu.

Si Lazima tujikite katika Kilimo tu, tunaweza kutanua wigo kwa njia hiyohiyo ya kukusanya Vijana na kuwapa kazi hata za kufyatua tofali za kuchoma na kujengea Nyumba za Walimu, Madarasa, Zahanati, Vituo vya afya, Vituo vya polisi, Nyumba za polisi mana nao wanaishi ktk mazingira magumu mnoo..

Wapo Vijana wanaopenda kufanya kazi na kutumia nguvu zao ktk kulijenga taifa letu huku nao wakiwezeshwa kwa namna fulani ktk kutafuta mitaji wapate kufanya biashara zao. Kufanya hivi kwa uchache wake Serikali itapunguza idadi kubwa ya Vijana wasio na ajira, pia itapunguza idadi kubwa ya Vijana wanaokimbilia mijini hivyo kuondoa msongamano usio na ulazima.

Tukiweka siasa kando kwa kila kitu tunachokifanya tutafika.
 
Nakumbusha tu saiv bei ya mbolea kwa mfuko wa 50kg ni 100k na vijisenti kadhaa kutoka 50k mwaka jana
Hili nalo ni tatizo kubwa lingine ambalo lina athiri kilimo,haiwezekani gunia moja LA mahindi liwe na bei ndogo kuliko mfuko wa mbolea..Serikali iangalie namna ya kupunguza or kuondoa kabisa kodi zinazotokana mbolea.

Istoshe sisi wenyewe tunaweza kujenga viwanda vya mbolea ili kupunguza gharama za upatikanaji wake.

Tuna taka nyingi zilizozagaa mijini na kuchafua miji yetu kwa kuweka madapo kila mahali. Tukijenga viwanda hivi vitasaidia kuchakata taka hizo kuwa mbolea wakati huohuo tukisafisha miji yetu.
 
Viongozi wengine wanaona raha tuendelee kuwa maskini Mana ndo mtaji wao huo wa kuingia madarakani,hatujawahi kupata viongozi wa maana...
 
Gunia la Mahindi elf 35. Yaani unauza magunia matatu ili ununue mfuko mmoja wa mbolea
Hili kwakweli halikubaliki hata kidogo.Ndio maana vijana tunakimbilia mijini na kukidharau kilimo kuona kama hakina tija mana MTU unatumia nguvu nyingi,mtaji mkubwa na unachokuja kukipata hakiendani na uhalisia wa gharama ulizozitumia.
Vijana kukimbilia mijini sio kuwa wanapenda sana Bali ni walau kutafuta unafuu wa maisha.Huwezi kuwafukuza Machinga halafu hujawawekea mpango mbadala wa kuwafanya waendelee kufanya shughuli zao.Serikali ikitaka kuwaondoa bila bughdha waboreshe Kilimo kwa ujumla wake waone kama kuna watu watabaki mjini.
 
Siajabu shida ni huko kumtaja mama samia, kuna wanaomchukia ndg'angu....acha tu!
Lakini ndie mwenye dhamana na ndie anaeongoza Serikali,so kutomtaja ni kujidanganya mwenyewe tu..Namtaja yeye ili huu ushauri wangu wa mwanaNchi wa chini kabisa uweze kumfikia pengine washauri wake wanampotosha ndio mana anafanya hayo wanayodhani anakosea..so njia sahihi ni kusema ili ajue kununa na kumkasirikia haisadii kitu Mkuu
 
Haters wanajifanya hawajui hilo
 
Viongozi wengine wanaona raha tuendelee kuwa maskini Mana ndo mtaji wao huo wa kuingia madarakani,hatujawahi kupata viongozi wa maana...
Tujaribu kuwashauri namna bora zaidi ya sisi wananchi tungependa kuongozwa,pengine huwa wanapitiwa na kujisahau tujipe jukumu LA kuwakumbusha tu.
 
Hili kwakweli halikubaliki hata kidogo.Ndio maana vijana tunakimbilia mijini na kukidharau kilimo kuona kama hakina tija mana MTU unatumia nguvu nyingi,mtaji mkubwa na unachokuja kukipata hakiendani na uhalisia wa gharama ulizozitumia.
Vijana kukimbilia mijini sio kuwa wanapenda sana Bali ni walau kutafuta unafuu wa maisha.Huwezi kuwafukuza Machinga halafu hujawawekea mpango mbadala wa kuwafanya waendelee kufanya shughuli zao.Serikali ikitaka kuwaondoa bila bughdha waboreshe Kilimo kwa ujumla wake waone kama kuna watu watabaki mjini.
Dogo unaumiza kichwa chako bure kuandika mambo unayofikir wewe ni yamsingi.!
 
Dogo unaumiza kichwa chako bure kuandika mambo unayofikir wewe ni yamsingi.!
Mkuu kuna kosa lolote la mm kufanya hivyo?au ungependa nifikiri na kuandika vitu gani ambavyo ww unafikiri ni sahihi?niandike namna nilivyokataliwa na kina Mariam na Salome?niandike kama ile penati ya Simba Jana dhidi ya Polisi Tanzania kama ni sahihi or si sahihi?
Mkuu kile unachokiona cha maana kwako kwa mwingine ni utopolo na kinyume chake.kuhusu kuumiza kichwa usikonde Mkuu ni heri niumize kichwa kuliko kuumiza mwili.
So relax Mkuu.
 
Nakumbusha tu saiv bei ya mbolea kwa mfuko wa 50kg ni 100k na vijisenti kadhaa kutoka 50k mwaka jana
Niko Katavi ekari moja ya mpunga, pamoja na bei ya mbolea na mengine bado mtu anavuna gunia 20. Sasa piga hesabu kila gunia elfu 50 je kama kijana kalima ekari tatu au nne hajatoboa na kumuacha mmachinga anakimbizana na migaamboo??
 
Mkuu kuna kosa lolote la mm kufanya hivyo?au ungependa nifikiri na kuandika vitu gani ambavyo ww unafikiri ni sahihi?niandike namna nilivyokataliwa na kina Mariam na Salome?niandike kama ile penati ya Simba Jana dhidi ya Polisi Tanzania kama ni sahihi or si sahihi?
Mkuu kile unachokiona cha maana kwako kwa mwingine ni utopolo na kinyume chake.kuhusu kuumiza kichwa usikonde Mkuu ni heri niumize kichwa kuliko kuumiza mwili.
So relax Mkuu.
Pambana, japo sauti yako ipo chini sana kuweza kuyazungumza mambo ya msingi mpaka Samia akakusikia na akafanyia kazi.
 
Back
Top Bottom