Rais Samia: Vijana hawaoi na wala kuolewa kuna tatizo kwenye jamii ya kitanzania

Rais Samia Hassan ameyazungumza hayo leo katika hafla ya kusimikwa rasmi mkuu wa kanisa la KKKT Askofu Dkt Alex Malasusa katika kanisa la Azania front jijini Dar es Salaam

Rais Samia ameshangazwa kwanini tatizo la vijana kutokuoa au kuolewa linaongezeka nchini Tanzania wakati vijana wamefikia umri wa kuoa na kuolewa

Rais Samia ameshangazwa kwa sasa vijana wa kike ndio wanaohudhuria sana kwenye mambo ya kidini na kuwaacha kundi kubwa la vijana wa kiume wakipotea na hivyo kusababidha ombwe kubwa kwenye jamii

Kwa mujibu wa Rais Samia Hassan,Taarifa ya ripoti ya mahusiano ya jamii inaonyesha maeneo ya mjini tatizo la vijana kutooa na kuolewa linazidi kuwa kubwa zaidi ukilinganisha na vijijini

Aidha Rais Samia amesisitiza kuna migogoro mikubwa sana ndani ya familia hasa ndoa na hivyo kupelekea vijana kulelewa kwa kukosa maadili

Kwa mujibu wa Rais Samia zaidi ya migogoro elfu thelathini na tisa ya ndoa imeripotiwa

Rais Samia amewaomba wa Tanzania warudi kwenye misingi yetu ya asili ambapo vijana walilelewa kwa maadili makubwa sana ,Akitolea mfano enzi zao ilikuwa ngumu sana kwa mwanaume kumtongoza mwanamke na mwanamke akakubali kirahisi rahisi kwani wanawake walikuwa na misimamo tofauti na leo

Rais Samia ameiomba jamii wazazi na walezi kuwafundisha watoto maadili mema kwa kuwapeleka kwenye imani zao ili kuwajengea misingi bora ya ufahamu na maisha hapo baadae
##

Maswali ya kujiuliza kama Taifa,
1.Tatizo la vijana kuoa na kuolewa ni mambo ya maadili kama Rais Samia alivyosema au maisha magumu kwa vijana wa kiume?

2.Lakini kuna vijana wana maisha mazuri mbona hawataki kuoa au kuolewa pia?
Anajiuliza hakuna ndoa lakini hajiulizi idadi ya watoto wa mtaani na panya road kuthibitisha kwamba uchumi siyo mzuri ajira hakuna watu hata kama hawaoani lakini wanazaana.

Hajiulizi why there’s plenty of single mamas etc etc.
 
Vipi kuhusu katiba mpya?
Sikumbuki kama kuna mtu kaulizia tatizo la samaki aina ya Ningu kupungua Ziwa Victoria. Kulikoni? Wala hakuna aliyeongea juu ya pundamilia sasa wamejaa pande za Maswa na Meatu, kulikoni? Na tumehuru ya mbowe hivohivo, sikumbuki kuisikia. Totally irrelevant!
 
Wanawake kujaa makanisani si kwamba wanamjua Mungu wengi shida zao zikishaisha na kanisani wanakata mguu.
Binti akiwa na shida ya ndoa hakosi kanisani Mungu asikie kilio chake sasa kwa kumpatia Mme au kazi kanisa ugeuka kituo Cha polisi.
 
Kuna mambo mengi hayakuwapo zamani ndio mana baba zetu waliweza kuwacontrol wake zao kwa sasa kuna mambo mengi yamebadilika hasa kwa wanawake kutopenda kuanza na mwanaume from the ground kila wengi wanapenda shortcut matokeo yake wamejaa sana kwenye mabar na madanguro
 
Rais Samia Hassan ameyazungumza hayo leo katika hafla ya kusimikwa rasmi mkuu wa kanisa la KKKT Askofu Dkt Alex Malasusa katika kanisa la Azania front jijini Dar es Salaam

Rais Samia ameshangazwa kwanini tatizo la vijana kutokuoa au kuolewa linaongezeka nchini Tanzania wakati vijana wamefikia umri wa kuoa na kuolewa

Rais Samia ameshangazwa kwa sasa vijana wa kike ndio wanaohudhuria sana kwenye mambo ya kidini na kuwaacha kundi kubwa la vijana wa kiume wakipotea na hivyo kusababidha ombwe kubwa kwenye jamii

Kwa mujibu wa Rais Samia Hassan,Taarifa ya ripoti ya mahusiano ya jamii inaonyesha maeneo ya mjini tatizo la vijana kutooa na kuolewa linazidi kuwa kubwa zaidi ukilinganisha na vijijini

Aidha Rais Samia amesisitiza kuna migogoro mikubwa sana ndani ya familia hasa ndoa na hivyo kupelekea vijana kulelewa kwa kukosa maadili

Kwa mujibu wa Rais Samia zaidi ya migogoro elfu thelathini na tisa ya ndoa imeripotiwa

Rais Samia amewaomba wa Tanzania warudi kwenye misingi yetu ya asili ambapo vijana walilelewa kwa maadili makubwa sana ,Akitolea mfano enzi zao ilikuwa ngumu sana kwa mwanaume kumtongoza mwanamke na mwanamke akakubali kirahisi rahisi kwani wanawake walikuwa na misimamo tofauti na leo

Rais Samia ameiomba jamii wazazi na walezi kuwafundisha watoto maadili mema kwa kuwapeleka kwenye imani zao ili kuwajengea misingi bora ya ufahamu na maisha hapo baadae
##

Maswali ya kujiuliza kama Taifa,
1.Tatizo la vijana kuoa na kuolewa ni mambo ya maadili kama Rais Samia alivyosema au maisha magumu kwa vijana wa kiume?

2.Lakini kuna vijana wana maisha mazuri mbona hawataki kuoa au kuolewa pia?
Mam kimkaz hali ni ngumu
 
Leo mnawaambia waoe kuwapa kazi hamtaki mnasema wakafuge kuku yaani kila kitu lawama kwa vijana!!!!
Kazi zipi mkuu? Hizi ambazo MPENDWA WETU MKUU CDF ametupa alert kua zimejazwa wakimbizi
 
Back
Top Bottom