My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,283
Rais Samia, wala usihofu, hatuoni wapi ambako viatu vya Hayati Magufuli vimekupwaya, unapodai eti havijakufaa hivyo viatu wakati tangu Mungu alipomtwaa Magufuli kila kitu kipo vile vile ndo kwanza unaboresha.
Wakati Magufuli akiwa madarakani,Sukari kg moja ilikuwa Tsh3,000,na haijashuka hadi sasa.
Nyama ilikuwa Tsh 7,000 na haijashuka hadi sasa.
Kipande cha sabuni kilikuwa Tsh 400, sasa kimepanda hadi Tsh 500.
Mafuta ya kula yalikuwa Tsh 5000 kwa lita sasa hivi yamepanda hadi Tsh 7000 kwa lita.
Demokrasia haikuwepo,na hata sasa haipo, Mbowe kudai katiba mpya,ikawa nongwa mkampa kesi ya Ugaidi.
Uhuru wa Habari haukuwepo na hata sasa haupo.
Magufuli alinunua ndege ambazo hazina Tija kwa Taifa,na wewe umeendelea kununua ndege,ni kichekesho kweli,tangu lini Serikali ikafanya Biashara?
Yaani viatu vya Magufuli vimekufaa hadi kupitiliza,ndo kwanza umezidi kuyafanya maisha ya Watanzania kuwa magumu kwa kuleta Tozo za miamala ya simu.
Wapi ambako viatu vya Hayati Magufuli havijakufaa?