Rais Samia Unadanganywa!

Lazima aingizwe mkenge Ili wamuondolee uhalali wa kugombea mwakani!!sio kwa bahati mbaya japo ukweli raia ndio tunaumizwa na hiyo ishu!
 
Nimeisikiliza hotuba yote na ilikuwa nzuri, imetoka wakati sahihi, maudhui yametiririka vizuri na ujumbe umewafikia wahusika. Na ninavyopitia mitandao mbalimbali ikiwemo JF, inaonyesha kuwa walengwa wote wameielewa vizuri hotuba na kuweweseka katika majibu yao.

  • Jamii yetu hapa ndio ilipofika: Rushwa kila kona ya TZ, ukitaka kuamini kuwa CHADEMA hakuna rushwa au hakuna wauwaji, ok
  • Ukitaka kuamini kuwa kifo cha Ali Kibao (R.I.P), ni zaidi ya vifo vya toka vijana wa Panya road, watoto kutekwa na kuuwawa, mganga kufukia watu wazima kwa watoto kaburini zaidi ya 10, Ok
  • Ukitaka mahusiano yetu na Marekani yawe kama yale ya Mabutu na wao. Ndio baba, ndio baba, Ok
Ila moja ulifahamu la msingi: Tanzania itajengwa na Watanzania na kuharibiwa na Watanzania. Sio Ulaya, Urusi, China wala Marekani. Alamsiki!
 
Nionavyo mimi kwa Kiongozi Smart, mwenye kujielewa na mzalendo ukiletewa taarifa nzito ipokee ila ni vizuri ukaifuatilia na wewe kimya kimya kwa njia unazozijua wewe ili kupata usahihi hasa, kinyume na hapo utakuwa kama Sponge, maji linanyonya, Mafuta, oil nk nk.
 
Ikulu walicheza sana kuedit maneno yake kwenye ile official press release waliyoandika baada ya lile tukio!

Wasaidizi walijua hapa Bi mkubwa ameenda chaka vibaya saana! Wakalipoza kwenye press release.


Tuwashauri tu sasa wamuombee kuonana na hawa mabalozi na wamuandikie cha kuongea maana wakimuacha tu twafaaaaa.
 
Well presented. The problem is, does she visit JF? Who is honest enough to tell Her Excellency to read this?
 
Katika miaka ya 1960 serikali ya Tanzania iliingia katika aibu kubwa sana.

Serikali ilitengenezewa ushahidi feki kwamba kuna mpango wa Wamarekani wa kuipindua. Oscar Kambona akaitisha mkutano na kuelezea jambo hili. Kwamba mabeberu wanataka kuipindua serikaki ya Tanzania.

Baadaye ikaonekana kuwa nyaraka zile zilikuwa feki. Serikali iliingia aibu sana kwamba imetoa tuhuma nzito kwa nyaraka feki.

Nyerere akasema kuwa nchi yetu ni changa na haina resources nyingi za kubaini haya mambo vizuri.

Leo miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru, serikali inarudia mambo yaleyale.

Inabidi tujiulize. Huu ni ujinga tu? Nchi yetu bado ni changa? Hatujifunzi kutoka historia? Na kama ni hivyo, tuna viongozi wanaofaa?

Au, huu si ujinga, ni mkakati maalum, serikali inaamua kuweka propaganda za habari hizi kwa makusudi kupata mtaji wa kisiasa?
 
Samia anajua kuwa yote ni uongo LAKINI KWA VILE YANAMSAIDIA KU CONSOLIDATE POWER, AGRESSIVE SUPREME OF POWER, ANAYAKUBALI AKIJUA FIKA KUWA NI UONGO MTUPU
Wanyonge wanaamini ni Kwa Bahati mbaya ameshtukizwa kumbe hiyo ni Mipango pangwa Kwa ustadi na mikakati madhubuti nyuma ya Pazia.
 
Ukweli ndio Rais Samia anadanganywa na wanaomzunguka na kumgombanisha na Watanzania na hata kimataifa. Rais wangu tafuta taarifa sahihi kwa watu wasio na mgongano wa maslahi. Wengine kwenye Chama wanatamani uharibikiwe na mambo yaharibike mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…