Rais Samia umeruhusu hii? Ichukulie hatua kali

Rais Samia umeruhusu hii? Ichukulie hatua kali

Kumbuka huyo ni mwenyekit wa ulinzi na usalama ukibishana naye hapo basi umeitafuta shari na jeshi la polisi katika eneo lake nanwaweza kupotea kabisa
Huu sasa ndiyo woga wenyewe tena wa kijinga. Mwenyekiti wa ulinzi na usalama anaruhusiwa kupiga watu viboko? Kama ana kosa atumie sheria. Narudia tena. Ingekuwa ni mimi basi pengine ungekuwa ndiyo mwisho wangu na yeye wa kuishi hapa duniani.
 
Imagine mtoto wako anakuona baba unachapwa viboko na mtoto mdogo kihongosi
 
Ila na sisi watanzania tumezidi ukondoo. Hii nisingekubali kwa hali yoyote na pengine ndiyo ingekuwa mwisho wangu na yeye. Ujinga gani! Hapa Samia pamoja na ubaya wake lakini hahusiki kwa vyovyote.
Uhusika wake ni poor vetting process. Unaweka madarakani hata vichaa
 
Wakuchukua hatua hawezi kuwa huyo uliye mtaja , hanaga muda na hayo mambo huyo
Yaani hata wewe unaogopa kumtaja Samia unaishia kusema 'huyo....huyo' pamoja na kwamba unatumia jina bandia!
Kumtawala mtanzania ni rahisi sana kwa vile wengi hawajui haki zao za msingi.
 
Halafu utegemee hao ndio wafundishe watoto wetu kujisimamia, wakati jitu zima limeshindwa kujisimamia! WTF
 
Uhusika wake ni poor vetting process. Unaweka madarakani hata vichaa
Nakuhakikishia siyo kichaa na jamaa ni mzima kweli kweli ila anajua hawa wananchi ni manyumbu. Kwa hiyo unaweza kusema sisi wananchi ndiyo vichaa wa ujinga.
 
Kihongosi ni mafia, mjeuri, mjivuni, huku akijifanya mchamungu.
Japo namkubali pia. Lol

Leo ni RC huko huko Chuga, na tukio lilitokea wakati akiwa DC.
 
sie ngozi ya taa call sijui tuna shida gani...
mungu aepushe maana mi nadhani hapo ndo itakua mwisho wa maisha yangu siku hiyo
 
Imagine mtoto wako anakuona baba unachapwa viboko na mtoto mdogo kihongosi
Haikua sahihi kabisaa, hili lingetokea kwetu, mbona hadi sahivi huyo Kihongosi angekua mavumbini km sio ana kilema cha kudumu maishani kwake.

Hatutaki utani sisi kule kwetu, tunamalizana kwa namna tunayoweza sisi.
 
Mkuu, hii ni ya zamani sana. Wakati huo Kihongosi alikuwa DC Arusha. Kwasasa amekuwa RC hukohuko.

Kimsingi, kitendo kilichofanyika kilikuwa ni kinyume cha sheria, taratibu na kanuni. Sijui kwanini waathiriwa hawakumburuza mahakamani.
Mpaka leo kawa RC. Inamaana mamlaka ziliona anachokifanya ni sahihi maana huwezi mpromote mtu mpuuzi kama huyu anaenda kinyume na sheria,taratibu na kanuni afu mara paap unasikia ni RC
 
Ukweli ni kwamba KILA MTANZANIA (Hasa WANAUME) alipaswa kula hii mikwaju kasoro LISSU tu.
 
Back
Top Bottom