Rais Samia umeruhusu hii? Ichukulie hatua kali

Rais Samia umeruhusu hii? Ichukulie hatua kali

Sidhani kama utafurahia anachokifanya mteule wako. Haya tuliyaona wakati wa ukoloni, ma Dc kuwachapa weusi vibok! Usiiruhusu!
Anabonda majizi kistaarabu!

Huku mtaani tunapiga kipopopo, kisha tunachoma na moto.

Mtu mpaka kukubali kulala achapwe elewa kuna jambo kaliona linambana kisheria pindi atakapofikishwa mahakamani, hivyo kulambwa mboko ni kutaka kulimaliza jambo hilo nje ya mahakama.

Vinginevyo ni ngumu sana mtu kukubali kuburuzwa mboko kipumbafpumbaf na kirahisi namna hiyo.
 
Hii ilikuwa 2020 kwenye utawala wa dikteta uchwara wa Chato.

Alianza domo kaya Chalamila kucharaza watu viboko ndio akafuta huyo kibaka Kihongosi watu walikuwa wameshaanza kufanya viboko ni adhabu ya kisheria pengine watu wasingepaza sauti tungeona wengi zaidi wakicharazwa.

Ila cha kushangaza leo hii bado bi Mwenda anawakumbatia katika uongozi wake na wote ni RC.

Tofauti ya utawala wa bi Mwenda na Magufuli ni jinsia tu.
 
Sidhani kama utafurahia anachokifanya mteule wako. Haya tuliyaona wakati wa ukoloni, ma Dc kuwachapa weusi vibok! Usiiruhusu!
Hii nimeipenda sana yaan ifike hatua hata yeye akipananga awekwe Chini apigwe bakora za Matako sio hao tu
 
viboko kwa kutokamisha miradi ya serikali, but Mselelwa anasema ni ya zamani akiwa DC arusha and now he is the RC
Mkuu, hao waliochapwa walikuwa wafanyabiashara wa kununua vyuma chakavu.

Katika biashara yao ikatokea wameuziwa viti na meza za shule pale Arusha kama vyuma chakavu.

Walipokutwa navyo, pamoja na kujieleza mbele ya DC Kihongosi kama alivyokuwa, wakatandikwa viboko kama njia ya kuwafunza uzalendo!
 
ya muda sana ila huyo dogo kihongosi sio mtu mzuri hta kidg..ana roho mbaya sana na hawapendi wapinzan hta kidogo
 
Asingethubutu kufanya hivyo, kitendo cha kusema nilale chini anichape ingekuwa ni vita ya maji maji ya pili..

Huyo mzee alielala hapo ni pimbi, watz wengi hatujitambui.
Ndio maana CCM miaka nenda miaka rudi watatamba tu
 
Hahahahaaaa, tunasafari ndefu sana, huyu anayejiita mzalendo amechukua hatua gani dhidi ya ripoti ya ukaguzi wa mahesabu ya C.A.G 2024/2025, inayoonyesha upigaji wa wazi?
 
Aloo mimi huyo pimbi mimi hanipigi hio siku ningepigwa risas na walinzi wake angekutana na shambulio la kudhuru mwili
 
Ila na sisi watanzania tumezidi ukondoo. Hii nisingekubali kwa hali yoyote na pengine ndiyo ingekuwa mwisho wangu na yeye. Ujinga gani! Hapa Samia pamoja na ubaya wake lakini hahusiki kwa vyovyote.
Nakazia,Samia hakumtuma huyo mwenye Afya mbovu ya Akili!
 
Kumbuka huyo ni mwenyekit wa ulinzi na usalama ukibishana naye hapo basi umeitafuta shari na jeshi la polisi katika eneo lake nanwaweza kupotea kabisa
Watu wanaongea tu, geuka umshike shati ndio utajua hujui.
 
Mkuu, hii ni ya zamani sana. Wakati huo Kihongosi alikuwa DC Arusha. Kwasasa amekuwa RC hukohuko.

Kimsingi, kitendo kilichofanyika kilikuwa ni kinyume cha sheria, taratibu na kanuni. Sijui kwanini waathiriwa hawakumburuza mahakamani.
Maana yake nchi hii haina vetting. Mamlaka zinazojielewa haziwezi kuteua mtu huyu maisha
 
Back
Top Bottom