Rais Samia, taasisi ya Urais itaheshimiwa endapo anayeiongoza atajiheshimu, atatenda HAKI, ataheshimu Katiba na Sheria

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,414
74,063
Jana katika mkutano wako na wateule wa uwaziri na manaibu, mojawapo ya mambo uliyoyakazia ni kuheshimu taasisi ya Urais.

Umekwenda mbali na kusema kama anayeikalia taasisi hiyo humpendi/ humheshimu, basi iheshimu taasisi hiyo.

Mh. Rais, taasisi inakuwa defined na mtu aliyeikalia. Huwezi kutenganisha taasisi ya Urais na mwenye mamlaka ya taasisi hiyo.

Tabia na matendo ya anayeikalia taasisi hiyo ndiyo KIOO cha Heshima ya taasisi hiyo.

Ukitenda haki na wewe ukajiheshimu, utaheshimiwa bila kudai kuheshimiwa. Hàya ya kesi ya Mbowe na wenzake, hayawezi, kwa mtu mwenye akili timamu akaiheshimu taasisi ya Urais. Ni hayo kwa leo.

Kazi njema.
 
Nampenda rais ila ameonyesha ndimi mbili katika baraza la mawaziri aliloteua

Alisema anawapiga panga wanaotaka urais ila amewaonea wasio na hatia amewaacha wanaotaka
 
Jana katika mkutano wako na wateule wa uwaziri na manaibu, mojawapo ya mambo uliyoyakazia ni kuheshimu taasisi ya Urais.

Umekwenda mbali na kusema kama anayeikalia taasisi hiyo humpendi/ humheshimu, basi iheshimu taasisi hiyo.

Mh. Rais, taasisi inakuwa defined na mtu aliyeikalia. Huwezi kutenganisha taasisi ya Urais na mwenye mamlaka ya taasisi hiyo.

Tabia na matendo ya anayeikalia taasisi hiyo ndiyo KIOO cha Heshima ya taasisi hiyo.

Ukitenda haki na wewe ukajiheshimu, utaheshimiwa bila kudai kuheshimiwa. Hàya ya kesi ya Mbowe na wenzake, hayawezi, kwa mtu mwenye akili timamu akaiheshimu taasisi ya Urais. Ni hayo kwa leo.

Kazi njema.
Heshima hutoka moyoni, ni zao la haki na upendo wa kweli, kama riziki hutiririka HUJA yenyewe.
Malaika wa Burigi, MUDA WOTE alitimia vitisho na maguvu makubwa ya dola kukandamiza watu, aliishia kujijazia unafiki na wanafiki.
Ikiwa Chief Hangaya hakujifunza wakati ule, ni dhahiri kuwa kama kiongozi mkuu, HAFAI.
 
Wao wanaomba heshima ila wanaadhibu wengine ili waendelee kubaki madarakani wapewe ile heshima wanayo itaka
 
Rais fisadi anaehamasisha ufisadi kwa serikali yake tena kupitia TV ya Taifa hawezi kuheshimiwa wala Taasisi yake ya uraisi haiwezi kuheshimiwa wala nchi anayoongoza haiwezi kuheshimiwa wala wananchi wake hawawezi kuheshimiwa.
 
View attachment 2080533
 
Viongozi wengi wa Africa, hujiona wao Ni last say, top of all, brainy than all, knowing than all, right than all. Wao ndio Nchi, ndio katiba, ndio sheria, ndio Mahakama, ndio Bunge.
 
Back
Top Bottom